Aug 25, 2018
Mambo Matano (5) Muhimu Yatakayokusaidia Kufikia Kilele Cha mafanikio Yako
Siri
kubwa iliyopo katika kuyafikia mafanikio yako ipo katika kuzifahamu mbinu
zitakazokusaidia kuweza kuyafikia mafanikio hayo. Wengi tumebweteka kimwili na
kiakili huku tukizani labda mafanikio chanzo chake huwa ni bahati nasibu, uchawi na mengineyo mengi
yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake.
Hata
hivyo ukweli ni kwamba yapo mambo muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kufikia
kilele cha mafanikio, na mambo hayo ni:
1. Chukua hatua kila siku.
Mafanikio
ni mchakato usiokuwa na mwisho, hivyo basi kwa kila kitu ambacho unadhani
kinakupa mwanga wa kuelekea kwenye kutimiza malengo yako ni vyema ukachukua
hatua za utekelezaji wa jambo hilo.
Watu
wengi sana ni wazuri sana wa kuwaza mambo mengi sana ya msingi ila linapokuja
sula la kuchukua hatua wamekuwa ni watu wavivu sana wakuweza kufanya hivyo na matokeo
yake watu hayo wamekuwa wakijitengenenezea ukata wao wenyewe. Hivyo kila wakati
jifunze kuchua hatua sahihi kwa kile unachokifanya au unachotaka kufanya.
2. Jifunze kuweka viupambele.
Kazi
yeyote inayofanywwa isiyokuwa na
vipaumbele ni uchafua, kama ulivyo uchafu mwingine, unashangaa wala usishangae
huo ndio ukweli.
Watu
wengi wanashindwa kutuliza kiu ya umaskini hii ni kwa sababu watu hao
wameshindwa kutambua ni kwa namna gani wanaweza kupanga viupembele kwa vile
vitu wanavovifanya.
Kupanga
vipaumbele humsaidia mtu husukia kufahamu na kutambua ni kazi gani ianze
kufanyika na ipi ifuate. Hivyo kama kweli umeuchoka umaskini jifunze kupanga
vipaumbele kwa vitu unavyofanya kwa kuangalia nini kianze kufanyika, lini na
kwa wakati gani.
3. Jifunze kuyaweka malengo yako katika
nyakati.
Malengo
uliyonayo ni lazima uyaweke katika nyakati kabla hujaanza kufanya, na nyakati
hizi ni lazima uwe ni wakati uliopo na wakati ujao.
Jambo
hili linahitaji maamuzi magumu, yaani amua kwamba jambo hili ni lazima
nitafanya wakati huu au aumua jambo hili ni lazima nitalifanya muda fulani.
Katika kipengele hiki ugopa sana tabia ya kugharisha kufanya kwani ndiyo
inayoendelea kukuua taratibu bila wewe kujua.
4. Andika kila kitu ulichokifanya au
unachotaka kufanya.
Kuandika
mambo yako uliyoyafanya au unayotaka kufanya humpa mtu hamasa za kiutendaji
kwani mara kwa mara anakuwa anakumbuka ni kitu natakiwa kufanya na kwa wakati
gani? .
Ogopa
kufanya mambo ya msingi kwa kukurupuka kwani hii ndiyo ambayo husababisha watu
wengi kutokufanya maumizi sahihi. Hivyo kila nyakati jifunze kuweka kila kitu katika maandishi ili uweze kujijengea fikra
thabiti.
5. Fahamua kile unachokitaka.
Maisha
sio bahati nasibu bali maisha ni vile unavyotaka kuwa na muamuzi wa mwisho ni
wewe, hivyo kaa chini na tafakari kwa makini ni nini hasa unachokitaka kisha
uanze kuchua hatua stahiki juu ya jambo hilo.
Lakini
pia ikumbukwe kufahamu kile unachokitaka pasipo kuchukua hatua za kiundeji ni
sawasawa na bure, hivyo amua sasa kubadilika kwa kuchukua hatua za kiutendaji
kwa kile unachokifanya.
Mwisho
naomba nihitimishe kwa kusema ya kwamba endapo ukiyazingatia hayo yote
niliyokwisha yaeleza jiandae kuishi maisha yenye tija katika hii dunia.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.