Aug 15, 2018
Habari Njema Na Kubwa Ya Kimafanikio Kwa Zama Hizi Ni Hii Hapa.
Habari njema katika zama hizi ambazo tunazo ni kwamba, yapo mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa, zipo fursa nyingi ambazo zinatikiwa kufanywa, kikubwa kwako ni kutuliza akili yako sana na kuamua kufanya fursa moja tu ambayo umeichagua.
Hata
kama kuna wakati unajihisi kama umechanganyikiwa vile, yaani nikiwa na maana
unajiona huna cha kufanya, kitu cha kufanya tuliza akili yako, na chagua fursa
moja makini na matata kwako ifanye na acha kutangatanga kwani fursa zipo za
kutosha.
Kitu
cha msingi kwako sasa, zingatia ile hatua ya kwanza, fanya kitu sasa, chukua
hatua ya kwanza katika utendaji. Kuongea sana usiendelee kuongea, wewe ongelea
kwenye hatua na hilo litakusaidia kusonga mbele sana kuliko unavyowaza.
Kama
unaona kwako ni shida kuanza, anza na hatua ndogo kabisa, kama wewe ni
mwandishi anza na kuandika sentensi ya kwanza, kama unataka kufanya biashara
anza na mteja wa kwanza, chochote kile anza na kidogo.
Kama
ni kukaa, umekaa vya kutosha yaani ukiwa unasitasita kwa kutokujua hujui nini
cha kufanya. Chagua kitu chochote na anza kukifanya kitu hicho mara moja, kwani
kama nilivyosema zipo fursa nyingi za kufanya kwa nyakati hizi uamuzi ni wako.
Pia uelewe
fursa hizo zipo za kila aina ya mtaji, zipo fursa za mtaji mdogo kabisa na zipo
fursa unaweza ukaanza nazo ambazo hata hazina mtaji ni wewe tu kuamua
kuzichangamkia na kuzifanya mara moja.
Kama
bado unazile fikira za kuanza biashara na mtaji mkubwa sana unajichelewesha, wewe anza na mtaji mdogo tu
na kwa kuanza huko utaendelea kukua polepole na mwisho utafika utafanikiwa kwa
viwango ambavyo unavyotaka.
Lengo
la makala haya si kukutajia fursa hizo, bali ni nikukumbusha kwamba upo kwenye
kipindi ambacho kina fursa nyingi tena na za kutosha. Najua wewe ni shahidi
kwenye hilo na unaona fursa hizo kwenye maisha zinavyokuzunguka.
Ili uweze
kuzifaidi fursa hizo huhitaji kutoa sababu, fanya chochote hata kama ni kidogo.
Upo kwenye kipindi ambacho una fursa kibao na unatakiwa kipindi hicho ukitumie
vizuri ili kuweza kufanikiwa kwa kutumia fursa hizo kikamilifu.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.