Aug 16, 2018
Sababu Nne (4) Kwanini Unapata Pesa Lakini Huna Maendeleo.
Najua unafahamu fika kuwa kuna baadhi ya watu umeanza nao kazi au biashara fulani lakini kila ukiangalia maendeleo yao mara nyingi huwa ni ya muda mfupi au kokesekana kabisa kwa mafanikio kwa watu hao na ilihali watu hao wanapesa nyingi.
Pamoja na kuwepo kwa fedha nyingi kwa watu hao lakini watu hao
hawana mafanikio, je unajua ni wapi ambapo watu hao hukosea? naomba ufatane
nami nikueleze sababu ambazo hupelekea watu hao kutokuwa na maendeleo.
1. Kutokuwa na malengoThabiti.
Kutokuwa na malengo ndo mzizi mkuu wa kukosa maendeleo.
Kutokuwa na malengo ni sawa na kuwa na nauli huku ukiwa hujui ni wapi unapotaka
kuelekea. Kama ilivyo mfano wa kuwa na nauli iko vivyo hivyo hata katika maisha
ya kimafanikio.
Agalia watu wengi
wanatafuta pesa kwa bidii lakini kwa sababu watu hao hawana malengo thabiti mwisho
wa siku wanaishia kuzitumia ovyo pesa hizo kitendo hiki kinawafanya watu hawa
wanaendelea kuwa maskini miaka nenda miaka rudi.
Hivyo ndugu yangu ili uweze kujipatia maendeleo yako unatakiwa
kuwa ni mtu wa kupanga malengo kisha kuyatekeleza kwani ukiwa hauna malengo
utaishia kulalama kwamba kila ukipata pesa hakuna cha maana unachofanya.
2. Kutaka kufanya kila
kitu kwa wakati moja.
Ni kweli una pesa na una hamu ya maendeleo, lakini huna
malengo thabiti yanayokuongoza wewe katika matumizi yako ya pesa. Watu wenye
tabia hii huwa ni watu wenye kutapatapa yaani wewe unakuwa ni mtu wa
kutazama watu wengine.
Kama hunielewi hapa kwa uzuri sikiliza, ukiona mtu kanunua
kiwanja nawe utanunua, ukiona mtu amejenga nawe utataka kujenga mwisho wa siku
utajikuta huna hata kitu cha maana ulichofanya na pesa imeisha yote na huku
ukibaki unajishangaa.
Siku zote kuwa ni mtu wa kuchagua jambo moja moja katika
utekelezaji kwani tabia ya kuiga kutoka kwa wengine itakufanya uendelee kuwa
mtumwa wa umaskini. Maisha yako ni maisha yako tu, jifunze kutliza akili na
kufanya jambo moja kwanza.
3. Kutoa zaidi kuliko
uwezo wako.
Si vibaya kutoa lakini, miongoni mwa tabia ambayo inawatafuna
watu wengi wenye kiwango kikubwa cha fedha ni vile walivyo wazuri katika sura
la kuonesha uwezo wao wa kifedha mbele ya watu wengine.
Hivi umewahi kwenda mahali fulani kisha kukawa na utoaji/
uchangiaji wa jambo fulani? je watu ambao wana fedha huwa wanakuwaje katika
suala hili? jibu baki nalo.
Kama nilivyosema, sina maana ya kwamba kutoa ni kubaya la hasha
ila maana yangu ni kwamba kila wakati jifunze kutoa kutokana na kiwango
ulichonacho, kama wewe ni wa moja basi utoe moja, maana wa moja akivaa mbili
huku ni kujitengenezea nyumba ya umaskini.
4. Kuwa na matumizi ya
hovyo.
Ni kweli una matumizi ya hovyo kwa vile huna malengo basi hata
kama una pesa ambazo si nyingi lakini utaziona nyingi sehemu ya kutembea
utapanda bajaji kisa una buku ambayo ipo ipo tu mfukoni na imezibaa.
Pengine umeshiba lakini una 200 mfukoni ambayo haina kazi
utanunua karanga huna shida ya nguo lakini una laki mfukoni isiyo na malengo
utanunua shati kwa system hiyo utaishia kuwa na pesa nyingi lakini utakosa
maendeleo kwa sababu unanunua vitu ambavyo havikuwa katika mipango yako.
Kwa leo naomba niweke nukta kwa kusema ya kwamba kama utaendelea
kuyabeba mambo hayo katika mikono yako basi neno mafanikio utaendelea kusoma na
kayasikia tu. Weka mipango au mikakati ya kukutoa hapo kikamilifu na
utafanikiwa.
Ndimi: Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.