Aug 13, 2018
Mambo Matano Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawapotezi Muda Wao Kuyafanya.
Yapo mambo ya wazi ambayo watu wenye mafanikio hawayafanyi kabisa kwenye maisha na kwa kutokufanya mambo hayo huwapeleka kila siku kuendea kuchanja mbuga ya kukaribia mafanikio yao kwa ukaribu sana.
Ukilinganisha
na watu ambao hawana mafanikio, wao hufanya sana mambo hayo lakini watu wenye
mafanikio hawafanyi mambo hayo na wala hata hawashuguliki nayo sana kuyafikiria
kuyafanya na ndio siri ambayo huwaweka karibu na kufanikiwa.
Je,
unataka kujua ni mambo gani ambayo watu wenye mafanikio hawafanyi na kwa
kutofanya ndio siri kubwa inawapa na kuwasogeza kwenye mafanikio makubwa.
Twende pamoja kujifunza kupitia makala haya muhimu kwako.
1. Hawapotezi muda wao kuwa na watu
hasi.
Hata
siku moja watu wenye mafanikio hawapotezi muda wao wa thamani kuwa na watu
hasi. Kwa kawaida watu hasi wana kawaida moja kubwa ya kuongea vitu ambavyo
havina msaada wa kimaisha kama vile kukatisha tamaa.
Watu
wenye mafanikio kwa sababu wanawajua watu hasi jinsi walivyo na hawana mchango wao
basi, hujikuta huwakwepa kwa namna fulani watu hawa hasi na inafika muda kuwapotezea kabisa na
kufata maisha yao.
2. Hawapotezi muda wao kufanya kazi bila
kuwa na mpango.
Hakuna
kitu kibaya kama kuanza asubuhi yako pasipo kuwa na mpango, yaani unamka tu na
hujui ni wapi ambako unakoelekea na matokeo yake unajikuta unapoteza muda
mwingi huelewi ni kipi cha kufanya.
Watu
wenye mafanikio hawafanyi kosa hili hata siku moja. Hawa ni watu wa kuangalia vitu
vyao mapema sana na kujua ni kipi kifanyike wapi na lini na wakati upi. Kwa
kupangilia kwao huko mambo inawapa nguvu sana ya kufanikiwa.
3. Hawapotezi muda wao kuhofia mambo
ambayo hawawezi kuyatawala.
Kuna
mambo ambayo hata ukiyahofia vipi huwezi kuyatawala. Dawa ya kusonga mbele na
kuachana na mambo haya ni kuyaacha kama yalivyo. Mambo haya yananaweza yakawa
kama vile habari na mengineyo kama hayo.
Sasa
watu wenye mafanikio ni watu ambao wanapuuza sana mambo kama hayo. Ni watu
ambao hawashuguliki kabisa na mambo ambayo wanashindwa kuyatawala. Kila wakati
wanahusika na mambo ambayo wanaweza wakayatawala wao wenyewe.
4. Hawapotezi muda wao kuumizwa na
mambo yaliyopita.
Kuna
msemo mmoja wa Kiswahili unasema ‘yaliyopita
si ndwele na tugange yajayo.’ Watu wenye mafanikio hawapotezi muda kuumizwa
na matokeo yaliyopita. Watu hawa kazi yao kubwa ni kufanya yale ya mbele ili
kubadili matokeo.
Ili
kufikia mafanikio watu walioa na mafanikio wanajua namna ya kucheza na alama za
nyakati za kutokuumizwa na mambo ambayo yamepita na mambo ambayo hayana msaada
kwao. Kwa kufanya hivyo hupiga hatua sana za kimaisha.
5. Hawapotezi muda kuzingatia sana yale
yanayofanywa na watu wengine.
Kuna
watu ambao wanaumizwa sana na yale ambayo wanayafanya watu wengine kwenye
maisha yao karibu kila siku. Watu hawa badala ya kukazana na juhudi zao
wanajikuta ni watu wanaokazana na juhudi za maisha ya watu wengine.
Ili
kufanikiwa unatakiwa kuishi maisha yako. Kuendelea kuishi maisha ya watu
wengine hiyo inakuwa ni sawa na kuchukua uamuzi wa kujiumiza sana wewe mwenyewe
pasipo kujua . chukua uamuzi wa kuishi maisha yako wewe.
Kwa kifupi,
hayo ndiyo mambo ambayo watu wenye mafanikio hawapotezi muda wao katika
kuyafanya, je, wewe jiulize bado unaendelea kufanya mambo haya.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.