Jul 24, 2018
Mzazi Jijengee Utaratibu Huu Kwa Wanao Ili Kuleta Kizazi Chenye Tija.
Ewe mzazi mwezangu,
najua una majukumu mengi katika sayari hii, ila nakuomba usome hili ambalo lipo katika makala haya,
kwani ni la muhimu sana zaidi ya hata uzaniavyo. Lengo la kuandika walaka huu
ni kwamba mara kwa mara macho yangu
yamekuwa yakiona tabia hii ikizidi
kukithiri kwa wazazi wengi.
Wazazi wengi tumekuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wetu wanapata huduma zote zile za
msingi. Tumekuwa tukihakikisha watoto zetu wanapata elimu, chakula pamoja
malazi , halikadharika na afya bora. Katika hili niwapongeze wale wote
ambao huwa wanalitimiza hili hili kwa moyo wote pasipo kupindisha shingo.
Lakini pamoja na
kuendelea kuwapa mahitaji hayo ya msingi, wengi wetu tumesahau ya kwamba watoto
wetu wanahitaji mambo mengine mbali na hayo niliyoaanisha hapo juu. Wengi wetu
tumekuwa tupo bize na utafutaji wa fedha muda mwingi, kuliko kukaa na familia
zetu husasani watoto zetu.
Wapo baadhi ya wazazi nimekuwa
nikiwasikia wakisema wapo bize katika kuhakikisha wanatafuta ugali wa watoto,
wamekuwa wakitoka majumbani mwao muda wa asubuhi ambapo hata watoto hao
wanakuwa bado wamelala, Hata muda wa kurudi nyumbani wamekuwa wakichekewa, na
kukuta watoto wamekwisha lala, na tabia hii huenda ukaona mzazi upo sawa,
lakini ukweli unakosea sana.
Walee watoto wako katika misingi iliyobora. |
Kwa mtindo huu unadhani
haya ndiyo malezi bora kwa mtoto? Bila shaka kama wewe ni mmoja wa mzazi mwenye
tabia kama hii ni vyema ukatafakari na kuona jukumu lako kama mzazi ni lipi? Na
madhara ya kufanya hivyo ni yapi?
Kwani binafsi naamini
mtoto kama mtoto anahitaji muda wa kuweza kubadilishana mawazo pamoja na mzazi
wake achilia mbali na marafiki zake. Kwani katika dunia hii kumekuwa na mambo
mengi ambayo yamekuwa si mazuri na mengine ni mazuri. Na kwa kuwa mtoto hapati
muda wa kukaa na wazazi wake ili wamueleze yapi ni mazuri na yapi ni mabaya,
mtoto amekuwa akiyatenda yote kwa sababu amekuwa haoni uhimizo wowote kutoka
kwa wazazi wake.
Kwa kufanya hivyo wazazi
wamekuwa wanashtuka dakika za mwisho mambo yakiwa yamekwisha kuharibika kabisa,
na wazazi hao hao mwisho wa siku huwanyoshea vidole watoto hao na kusema ya kwamba wameharibika na hawafai.
Huku wamesahau wazazi hao ndiyo chanzo cha kumomonyoka kwa maandili kwa watoto
hao, na hii ni kwa sababu wazazi wamekuwa wakijitenga na jukumu la kufuatilia mienendo
na tabia za watoto hao kiujumla.
Hivyo ni jukumu la kila
mzazi kutenga muda walau hata kwa wiki mara tatu kuweza kuzungumza na mwanae
elimu zote za afya, jamii, mahusiano na elimu zinginezo. Wazazi wengi wamekuwa
wakiona aibu kutoa elimu hizo kwa watoto zao, huku wakiamini kufanya hivyo ni
sawa nakwenda kinyume na maadili.
Lakini ukweli ni kwamba
mzazi una jukumu la kumuelimisha mwanao mambo yote. Pia ewe mzazi ukumbuke ule
usemi usemao ”kukonda kwa mbwa si aibu kwa mbwa bali ni kwa mfuga mbwa”.
Mwanao akajiingiza
katika makundi mabaya yaliyopo hivi sasa aibu haitakuwa kwa mwanao bali itakuwa
ni aibu ya kwako mzazi. Hivyo mzazi mwenzangu ni heri ukawajibika kila sekta
katika kuhakikisha watoto wako unawaelea katika misingi inayoelewa, kwani pindi
utakaposhindwa kuwalea watoto zako, dunia hii ipo kwa ajili ya kuwafunza wale wote
ambao wameshindwa kufunzwa na mamaye.
Mwisho nimalize kwa
kusema “mzazi simama imara katika kusimamaia maadili mema ya mwanao kila
wakati, ili tujenge kizazi chenye tija”.
Ndimi afisa mipango: Benson Chonya,
0757909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.