Jul 19, 2018
Sababu Nne (4) Kwa Nini Hutakiwi Kujilinganisha Na Watu Wengine.
Hapo ulipo hebu jiulize swali hili? Bado unaendelea kujilinganisha na watu wengine? Inawezekana ukawa unajilinganisha na watu wa familia yako, rafiki zako au jirani zako. Tabia hii ya kujilinganisha ipo sana kwa wengi.
Kwa
bahati mbaya sana tabia hii ya kujilinganisha chanzo chake kikubwa kimeanzia
tokea ukiwa mtoto. Ukiwaangalia watoto wanajilinganisha sana na wenzao kwa
mambo mengi kama kwenye mavazi waliyonayo, midoli wanayochezea, nyumba wanayoishi
na vinginevyo.
Kwa
sababu hiyo hujikuta inapelekea unapokuwa mtu mzima unaanza kusema siwezi hiki
au siwezi kile au mimi si bora katika jambo lile, lakini hapa unaona yote hiyo
inatokana na kujilinganisha. Tabia hii
ya kujilinganisha kwa maendeleo ya mafanikio yako si nzuri.
Kivipi
tabia hii si nzuri ya kujilinganisha na wengine, zifuatazo ni sababu za msingi
ambazo unatakiwa ujue kwa nini kujilinganisha hakufai.
1. Kujilinganisha na wengine, inakupozea
furaha yako.
Kwa
jinsi unavyozidi kujinganisha na watu wengine, hiki ni kitu ambacho kitakupotezea
furaha yako pasipo kujua. Kuna maeneo ambayo unatakuwa unajiona hufai ama umepungukiwa
vitu fulani hivi kwa sababu ya kujilinganisha.
Siri
ya kuweza kudumisha furaha yako, acha kujilinganisha sana na watu wengine. Ishi
maisha yako na kimbia mbio zako mwenyewe ambazo utaziona mbio hizo zitakusaidia
kuweza kufanikiwa na kufikia mafanikio yako makubwa.
2. Kujilinganisha na wengine, inakuzuia
usisonge mbele sana.
Unapokuwa
unajilinganisha na watu wengine badala ya kuweka juhudi za kukusaidia kusonga
mbele, juhudi hizo unazimaliza kwa kujilinganisha. Matokeo yake unajikuta
unadumaa badala ya kusonga mbele sana unaishia palepale.
Hata
ikitokea unajilinganisha na wengine na ukafanikiwa kusonga mbele, pia hutasogea
sana, badala yake utajikuta unaishia katika eneo lile lile ambalo wale unajilinganisha nao wamefika
katika eneo hilo.
3. Kujilinganisha na wengine, hakuwezi
kukubadili wewe.
Kuna
watu ambao wanakuwa wanajilinganisha sana katika eneo la sura, hasa kwa wanawake.
Hata ukijilinganisha vipi, lakini elewa utabaki wewe kuwa wewe. Hakuna
kitakachobadilika, hautaweza kubadili sura yako.
Kama
unajilinginisha kwa hivi, unatakiwa kujua unajipotezea muda. Kazana na mambo
yako na usiendelee na mambo ya wengine au uzuri wao. Kazana sana kubadili yale yaliyo yako na si kukazana
kujibadili wewe kupitia wengine ni hatari kwako.
4. Kujilinganisha na wengine,
kunakupotezea ubora wako.
Utaupata
ubora wako na utaboresha maisha yako, kama unakazana kuwa bora wewe kuliko
ilivyokuwa jana yako. Kujilinganisha na wengine utajipotezea sana ubora wako,
maana utafanya kama wale unaojilinganisha nao na hautavuka sana.
Hizi
ndizo sababu za msingi za kwanini hutakiwi kujilinganisha na wengine. Fanyia
kazi sababu hizi na kuanzia sasa anza kuishi maisha yako wewe kama wewe.
Ukumbuke kuendelea kujilinganisha na wengine huko ni kujipoteza.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.