Jul 20, 2018
Dalili Tano (5) Zitakazokuonyesha Kwamba Upo Kwenye Njia Sahihi Ya Mafanikio Yako.
Kila mtu mwenye nia ya kutafuta mafanikio, kuna wakati anakuwa ana shaka kwamba je, ‘kweli nipo kwenye njia sahihi ya kufanikiwa au hapana.’ Hali hii hujitokeza kwa sababu, njia ya mafanikio inakuwa in changamoto nyingi sana.
Kuna
wakati inafika kutokana na changamoto hizo, wengi huanza kukata tamaa na kuanza
kujiuliza maswali kweli njia hiyo au hicho wakifanyacho kinawafikisha kwenye
mafanikio yao, au kinawatoa nje kabisa ya mafanikio.
Hali
kama hii inajitokeza kwa wengi sana si kwako tu, bali hata kwa watu waliofanikiwa ikiwemo pamoja na
mamilionea hufika wakati wakijiuliza je, kwa kile wakifanyacho kwa wakati huo
kinawafikisha kwenye mafanikio mengine ya juu zaidi au hapana.
Kitu
cha kujiuliza zaidi, utajuaje kwamba upo kwenye njia sahihi ya mafanikio yako?
Hiki ndicho kitu ambacho nataka ujifunze kupitia makala haya ili tena usiwe na
shaka. Kama utakosa dalili hizo kabisa miongoni mwa hizi ujue upo nje ya
mafanikio.
Zifuatazo
Dalili Tano (5) Zitakazokuonyesha Kwamba Upo Kwenye Njia Sahihi Ya Mafanikio.;-
1. Kama wewe ni king’ang’anizi.
Mafanikio
kila wakati yanawapendelea na kwenda kwa watu ambao ni ving’ang’anizi na ambao wana nidhamu ya kujua kile
wakitakacho na kukifanya kwa muda mrefu. Hakuna mafanikio yanayokwenda kwa mtu
ambaye si king’ang’anizi.
Mfumo
na njia unayoipitia ya ung’anganizi ndio inayotabiri kwamba wewe unakwenda
kufanikiwa. Nafasi yako ya kufanikiwa itakuwa kubwa sana kama ni
king’ang’anizi, tofauti na yule ambaye si king’ang’anizi kwani mtu huyo lazima
atashindwa.
Ukishajua
kile unachokitaka vizuri, ni vyema ukawa king’ang’anizi kwani ni dalili tosha
ya kwamba kitu hicho ukitakacho utakipata. Ukikosa ung’ang’anizi, ujue kabisa
hautaweza kufanikiwa hata kama ungeweka juhudi kubwa sana.
2. Kama una mahusiano sahihi na pesa.
Mahusiano
hayaishii tu kwa watu lakini pia ili kufanikiwa, unatakiwa kuwa na mahusiano
sahihi na pesa. Si kwa sababu unapata pesa ukaamua kuzitumia pesa hizo hovyo
hovyo na kufanya vitu vya ‘biashara
kichaa’ ambazo hata hazieleweki.
Mahusiano
sahihi yanakuja kwa wewe kutuliza akili yako, kwa kila pesa unayoipata kuiwekea
akiba hata kama ni kidogo sana, kuwekeza kwa busara na mengine kama haya.
Unapokuwa hauna mahusiano sahihi na pesa, huwezi kufanikiwa.
Unatakiwa
ujikague na kujitathimini, je unayo mahusiano sahihi na pesa. Kila unapoangalia
matumizi yako, je, yamekaa sawa? Kama ukiona una mahusiano sahihi na pesa, basi
ujue upo kwenye njia sahihi ya kuweza kufikia mafanikio yako.
3. Kama una mahusiano sahihi na watu
sahihi.
Kupata
mafanikio kunategemea mambo mengi sana, ikiwemo mojawapo la msingi sana ni kuwa
na watu sahihi. Kuwa na mahusiano na watu sahihi ni kitu cha muhimu sana katika
kukupa mafanikio uyatakayo maishani mwako.
Watu
sahihi wanakuwa wanakupa chachu na hamasa kubwa ya kukupeleka mbele
kimafanikio. Unapowakosa watu hao unakuwa unatoka nje ya mafanikio yako na
mwisho wa siku utashangaa umeshindwa vibaya sana.
Jiangalie
wewe mwenyewe na ujiulize je, una timu sahihi inayokuzunguka ya watu ambao
watakusaidia kukupa mafanikio yako? Kama huna timu hiyo itafute, kwani dalili
mojawapo inayoonyesha kwamba utafanikiwa ni watu sahihi ulionao.
4. Kama unajua mapema kile kinachofanya
kazi.
Watu
wenye mafanikio wanajua mapema sana yale mambo yayofanya kazi kwao na yale
ambayo hayafanya kazi. Kama kuna jambo wanalifanya, wakigundua jambo hilo
linawapeleka eneo ambalo si sahihi hukimbia sana na kutafuta kitu kingine.
Kile
kitakachokufanya ujijue pia uko kwenye njia sahihi ya kutafuta mafanikio yako
ni kule kuwa makini na kujua kile unachokifanya kama kinafanya kazi yaani
kinaleta matunda ambayo unayataka na kwa muda mwafaka unaoutaka wewe.
Ni
jukumu lako kukagua kile unachokifanya na kujiuliza maswali ya msingi, je, hiki
nikifanyacho kinafanya kazi au hakifanya kazi, kujiuliza maswali haya
itakusaidia sana kujua njia ya mafanikio unayopita ipo sahihi au haipo sahihi.
5. Kama una imani ya kufikia mafanikio
yako.
Imani
ni moja ya kitu kikubwa sana ambacho kinaweza kikakufikisha kule kwenye
mafanikio yako. Kila unapofikiria ndoto yako kama una imani kuna kitu ambacho
unajiambia ni lazima nitafanikisha hili au ni lazima nitafanya jambo lile.
Ile
imani unayojiambia wakati unatafuta mafanikio, hiyo ndio imani unayatakiwa kuwa
nayo. Imani hii ya kuweza haiji kwa bahati mbaya, bali inakuja pale unapokuwa
na mipango imara na kutambua jinsi unavyoweza kufikia ndoto zako.
Nikuulize
hapo ulipo una imani ya kuamini kwamba utafikia ndoto zako. Imani hii hata kama
huna, unatakiwa ujue jinsi ya kuweza kuimiliki ili ikusaidia kufika kule
unakotaka kufika. Mafanikio yako yanahitaji sana uwe na imani hii ya msingi.
Kwa
maelezo haya yakinifu, hizi ndizo dalili za msingi za kujua kama upo kwenye
njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio. Fanyia kazi hiki ulichojifunza na
chukua hatua mathubuti zitakazoweza kukusaidia kufikia ndoto zako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa
mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767
048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.