Jul 21, 2018
Zifahamu Sura Mbili Ziletazo Mafanikio.
Habari ya muda huu mpenzi msomaji wa blogu hii ya DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nikuarike jamvini tuweze kujifunza kwa pamoja sura mbili zitakazo kuletea mafanikio.
kila kitu unachokiona katika dunia
hii kipo katika mwenekano wake. Na mwenekano huo ndio ambao hufanya viumbe
vyenye akili viweze kutambuana kwa kutumia muonekanao huo. Pia mwonekano huo
ndiyo hutumika kijenga picha kamili ya kitu halisi.
Kama ndivyo hivyo basi katika
kuyasaka mafanikio inahitajika mtu husika aweze kuvaa sura mbili ili kuyanasa
mafanikio hayo. Na sura hizo mbili ndizo zitakazokufanya wewe uweze
kujitofautisha na watu wengine.
Huenda ukawa hujanielewa bado
usipate shida ipo hivi sizingumzii umbo wala muonekano ulionao ndio
utaokupa mafanikio laa hasha. Bali nazungumzia ya kwamba ili uweze kupata
mafaniko yako unatakiwa kuwa na sura ya Mwalimu na sura Mwanafunzi pia.
Ninapozungumzia suala la kuvaa sura
ya mwalimu, kwanza tambua ya kwamba mwalimu si yule anayefundisha darasani
pekee yake la hasha, bali mwalimu mzuri ni yule aliyelewa kisha kuyafanyia kazi
yale ambayo amelewa kisha kuwafundisha wengine.
Hii ina maana ya kwamba kile kidogo
ambacho unakifahamu kisiwe siri yako bali weka mikakati thabiti ambayo watu
wengine wataweza kunufaika na hicho unakijua. Huenda kwako ukakiona ni kidogo
sana ila tambua ya kwamba wapo baadhi ya watu kwa hicho unachokijua japo wewe
unakiona ni kidogo kwao ni kitu kikubwa sana. Hivyo kila wakati jifunze
kuwa mwalimu kwa watu wengine.
Sura ya pili ambayo unatakiwa kuwa
nayo ni sura ya mwanafunzi. Pamoja na kuwa mwalimu lakini elimu haina mwisho
hivyo endelea kuwa mwanafunzi , huku ukizingatia ya kwamba mwanafunzi bora ni
yule ambaye yupo tayari kujifunza katika mazingira yeyote yale.
Lakini mwanafunzi huyu ili awe
mwanafunzi ni lazima pawepo na utayari kutoke ndani ya nafsi ya mtu husika,
kwani kama mtu atalazimishwa kujifunza atashindwa kuyafanyia kazi yale ambayo
amejifunza.
Lakini pia mwanafunzi makini ni yule
mwenye kutambua ni nini maaana ya uanafunzi, yaani awe tayari kulipa gharama ya
pesa na gharama ya muda kwa kitu anachotaka kukifahamu. Kufanya hii ndiyo nguzo
ambayo kila unayemuona ana mafanikio imemsadia kwa namna moja ama nyingine kuwa
hivyo alivyo leo.
Kila kitu ambacho unakiona mbele ya
macho yako tambua kuwa kuna mtu aliwekeza gharama fulani katika kitu hivho,
hadi kupelekea kitu hicho kuwa hivyo kilivyo leo.
Hivyo ndugu yangu naomba nikwambie
ya kwamba mafaniko ya kweli yanajengwa na sura hizo mbili ambazo nimekwisha
kukueleza yaani kuwa mwalimu lakini pia kuwa mwanafunzi. Ukiyazingatia hayo
utaishi maisha yenye tija katika sayari hii ya dunia.
Ndimi: Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.