Jul 25, 2018
Jinsi Umaskini Unavyomaliza Maisha Yako.
Na Eryne Banda,
Dar es salaam.
Umaskini ni kutokuweza kumiliki kitu chochote katika maisha iwe
ni nyumba, gari, shamba, ardhi na kadhalika. Ni kuishi kwa kusaidiwa na watu.
Hapa mtu anakuwa hana uwezo wa kujisimamia, anaishi kwa kuombaomba.
Nikumbushe kwamba umaskini umechangia familia nyingi kutikisika
kiuchumi, zingine zikisambaratika kabisa. Umaskini umesababisha afya mbaya
katika baadhi ya familia huku wengine wakishindwa kuwapa elimu bora watoto wao.
Pamoja na hayo kabla hatujaingia kwenye somo jinsi umaskini
unavyoweza kukumaliza, naomba tuangalie kwanza, aina mbalimbali za umaskini
ambazo zimetuzunguka na zinaendelea kutesa wengi pasipo kujua chanzo chake.
Umaskini wa mawazo.
Huu ni umasikini mbaya sana. Watu wengi wana fedha lakini hawana
mawazo mapya. Umaskini wa mawazo ni mbaya kuliko umaskini wa mali. Jamaa mmoja
aliwahi kusema “mwisho wa mawazo yako ndio mwanzo wa matatizo yako”. Tatizo la
matajiri wengi ni kutokuwa na mawazo mapya japokuwa wana fedha nyingi.
Yapo mapepo yaliyofunga akili za watu ili wasiwe na mawazo
mapya. Mawazo mapya yanatoka kwa Mungu, hivyo tunapaswa kumuomba Mungu kwa
bidii ili atupe mawazo mapya. Je, jiulize hapo ulipo upo tayari kujenga mawazo
mapya kwa kiasi gani au bado unataka kuendelea na mawazo yako yaleyale?
Umaskini wa tabia.
Mtu mmoja aliwahi kusema; karama itakupeleka juu lakini tabia
itakufanya uendelee kubaki chini. Watu wengi wana karama nzuri, vipawa vizuri
lakini wameshindwa kwenye tabia. Watu wengi wamefukuzwa kazi kwa sababu ya
tabia zao mbaya huku wengine wakipewa majina mabaya sababu ya tabia zao.
Ni vema sote tukaelewa kwamba; tabia yako ndiyo
inayokutambulisha kwa watu; ndiyo itakayokupa kibali; ni wakati upo peke yako;
yale mambo unayoyafanya wakati wengine hawakuoni. Tabia yako ndiyo
itakayokufanya uendelee kuwa maskini au uwe tajiri; ndiyo inayokufanya
udharauliwe au uheshimiwe.
Ni muhimu sana kumuomba Mungu abadilishe tabia yako ili iwe
nzuri na ndipo utakapofanikiwa. Usiposhughulikia tabia yako, tabia
itakushughulikia wewe. Watu wengi watakupenda kwa sababu ya tabia yako nzuri.
Kumbuka: Utajiri wa tabia ni zaidi ya utajiri wa fedha/mali. Maisha ndivyo
Yalivyo.
Umaskini wa marafiki.
Mafanikio yanahitaji uwe na watu wazuri na hakika, huwezi
kufanikiwa peke yako. Watu wengi wamekosa kuwa na marafiki wazuri ndiyo maana
wameshindwa kufanikiwa. Umaskini wa marafiki ni kuunganishwa na marafiki wabaya
ambao ni chanzo cha kuangamiza hatma yako.
Kwa mfano, ili Daudi awe mfalme, Mungu alimuunganisha na
Yonathani ili aje kuwa mfalme. Bila ya Yonathani, Daudi asingekuwa mfalme hata
kama alikuwa amepakwa mafuta.
Alihitaji mtu wa kumshika mkono na kumfikisha kwenye kiti chake
cha ufalme. Soma andiko la Mungu katika 1Samweli 18: 3, “Nao Yonathani na Daudi
wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.”
Mpenzi msomaji, wapo watu ambao Mungu amewaandaa ili waweze
kukufikisha kwenye hatma yako. Mungu anaweza kukuunganisha na mtu mmoja tu na
maisha yako yakabadilika.
Tazama marafiki zako ulio nao, ndipo unapoweza kufanikiwa kwani
huwezi kufanikiwa peke yako. Ni lazima uwe na watu wazuri wa kukusaidia. Muombe
Mungu akuunganishe na marafiki wazuri, watu wenye bidii kuliko wewe.
Naamini msomaji wangu umejifunza jambo hapo. Tuishie hapa hadi
wiki ijayo ambapo nitaendeleza kidogo mada hii muhimu kwa kutaja aina zaidi za
umaskini ili uweze kujijua kinachokusibu hapo ulipo.
Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya
kujifunza na kumasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Makala hii imeandikwa
na Eryne Banda wa Dar es salaam,
Tanzania.
Jul 24, 2018
Mzazi Jijengee Utaratibu Huu Kwa Wanao Ili Kuleta Kizazi Chenye Tija.
Ewe mzazi mwezangu,
najua una majukumu mengi katika sayari hii, ila nakuomba usome hili ambalo lipo katika makala haya,
kwani ni la muhimu sana zaidi ya hata uzaniavyo. Lengo la kuandika walaka huu
ni kwamba mara kwa mara macho yangu
yamekuwa yakiona tabia hii ikizidi
kukithiri kwa wazazi wengi.
Wazazi wengi tumekuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wetu wanapata huduma zote zile za
msingi. Tumekuwa tukihakikisha watoto zetu wanapata elimu, chakula pamoja
malazi , halikadharika na afya bora. Katika hili niwapongeze wale wote
ambao huwa wanalitimiza hili hili kwa moyo wote pasipo kupindisha shingo.
Lakini pamoja na
kuendelea kuwapa mahitaji hayo ya msingi, wengi wetu tumesahau ya kwamba watoto
wetu wanahitaji mambo mengine mbali na hayo niliyoaanisha hapo juu. Wengi wetu
tumekuwa tupo bize na utafutaji wa fedha muda mwingi, kuliko kukaa na familia
zetu husasani watoto zetu.
Wapo baadhi ya wazazi nimekuwa
nikiwasikia wakisema wapo bize katika kuhakikisha wanatafuta ugali wa watoto,
wamekuwa wakitoka majumbani mwao muda wa asubuhi ambapo hata watoto hao
wanakuwa bado wamelala, Hata muda wa kurudi nyumbani wamekuwa wakichekewa, na
kukuta watoto wamekwisha lala, na tabia hii huenda ukaona mzazi upo sawa,
lakini ukweli unakosea sana.
Walee watoto wako katika misingi iliyobora. |
Kwa mtindo huu unadhani
haya ndiyo malezi bora kwa mtoto? Bila shaka kama wewe ni mmoja wa mzazi mwenye
tabia kama hii ni vyema ukatafakari na kuona jukumu lako kama mzazi ni lipi? Na
madhara ya kufanya hivyo ni yapi?
Kwani binafsi naamini
mtoto kama mtoto anahitaji muda wa kuweza kubadilishana mawazo pamoja na mzazi
wake achilia mbali na marafiki zake. Kwani katika dunia hii kumekuwa na mambo
mengi ambayo yamekuwa si mazuri na mengine ni mazuri. Na kwa kuwa mtoto hapati
muda wa kukaa na wazazi wake ili wamueleze yapi ni mazuri na yapi ni mabaya,
mtoto amekuwa akiyatenda yote kwa sababu amekuwa haoni uhimizo wowote kutoka
kwa wazazi wake.
Kwa kufanya hivyo wazazi
wamekuwa wanashtuka dakika za mwisho mambo yakiwa yamekwisha kuharibika kabisa,
na wazazi hao hao mwisho wa siku huwanyoshea vidole watoto hao na kusema ya kwamba wameharibika na hawafai.
Huku wamesahau wazazi hao ndiyo chanzo cha kumomonyoka kwa maandili kwa watoto
hao, na hii ni kwa sababu wazazi wamekuwa wakijitenga na jukumu la kufuatilia mienendo
na tabia za watoto hao kiujumla.
Hivyo ni jukumu la kila
mzazi kutenga muda walau hata kwa wiki mara tatu kuweza kuzungumza na mwanae
elimu zote za afya, jamii, mahusiano na elimu zinginezo. Wazazi wengi wamekuwa
wakiona aibu kutoa elimu hizo kwa watoto zao, huku wakiamini kufanya hivyo ni
sawa nakwenda kinyume na maadili.
Lakini ukweli ni kwamba
mzazi una jukumu la kumuelimisha mwanao mambo yote. Pia ewe mzazi ukumbuke ule
usemi usemao ”kukonda kwa mbwa si aibu kwa mbwa bali ni kwa mfuga mbwa”.
Mwanao akajiingiza
katika makundi mabaya yaliyopo hivi sasa aibu haitakuwa kwa mwanao bali itakuwa
ni aibu ya kwako mzazi. Hivyo mzazi mwenzangu ni heri ukawajibika kila sekta
katika kuhakikisha watoto wako unawaelea katika misingi inayoelewa, kwani pindi
utakaposhindwa kuwalea watoto zako, dunia hii ipo kwa ajili ya kuwafunza wale wote
ambao wameshindwa kufunzwa na mamaye.
Mwisho nimalize kwa
kusema “mzazi simama imara katika kusimamaia maadili mema ya mwanao kila
wakati, ili tujenge kizazi chenye tija”.
Ndimi afisa mipango: Benson Chonya,
0757909942.
Jul 23, 2018
Hivi Ndivyo Utofauti Ulipo kati Ya Mwanaume na Mwanamke Katika Hisia Za Kimapenzi.
Katika
ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina
nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana na nguvu hiyo ya
mahusino, watu wengi hufikiri mwanaume ndio ambao wanaathiriwa kwa kiwango kikubwa
na nguvu hiyo.
Watafiti wa
masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume kila baada ya dakika
tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana wanaume wengi
hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndio maana ukichunguza kwa
makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia zaidi katika kutazama jinsia hii ya
kike mahali popote walipo.
Hivi hujawahi
ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite mwanamke mzuri mbele
ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda? Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia
wakisema kwa minong'ono aaah angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia
wakisema mcheki chura huyo. Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio
chanzo kikubwa cha kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu
huyo.
Lakini ukweli
ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi huingia katika matamanio
ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo
mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno
mengine tunaweza kusema matamanio ya hisia za mwanamke yapo katika kuona zaidi
kuliko kitu chochote.
Lakini
ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti sana
ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia
za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso katoka kwa mwanaume. Hisia
za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na
mwanaume.
Mwanamke
huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume, kwa mfano
mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mwanamke
huamini hivyo,hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa katika kuziteka hisia
za mwanamke.
Lakini pia
kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale anapoguswa na mwanaume,
hivyo ndio maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza ataka usimguse
katika mwili wake, hii ina maana mguso wa mwanaume una nguvu sana katika
kuamsha hisia mwili wa mwanamke.
Hivyo kama
ndivyo hivyo basi hii ni utofauti mkubwa ulipo kati ya mwanaume na mwanamke
katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa ambacho huongoza hamasa na
kudumu katika mahusiona ya kimapenzi ni "mawasiliano", mawasiliano
ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu
katika mahusiano yenu hakikisha unakuwa na mawasilino bora kati yako na mwenzi
wako.
Asante kwa
kuendelea kutembelea blog hii ya DIRA YA
MAFANIKIO, TUPO PAMOJA.
Ndimi afisa
mipango; Benson Chonya,
0757909942.
Jul 22, 2018
Mawazo Yakinifu Ya Mafanikio Endelevu Kwako.
Mafanikio yoyote yanaanza na mawazo. Hakuna mafanikio yanazaliwa nje ya mawazo. Kwa jinsi unavyokuwa na mawazo bora ndivyo unavyozidi kuwa na mafanikio bora kwako. Mawazo bora unayapata vipi, unayapata kwa kujifunza.
Kupitia
makala haya, nakukaribisha tujifunze pamoja mawazo yakinifu ya mafanikio yako
endelevu. Naamini kupitia mawazo haya, utajifunza kitu ambacho kitakutoa hatua
moja na kwenda hatua nyingine, karibu tujifunze.
1.Unaweza
ukaendelea kuteseka kila siku na maisha na kuteseka kila na kila aina ya
ugonjwa, lakini hiyo yote inaweza ikasababishwa na ujinga ambao umeushikilia. Ujinga ni adui mkubwa sana wa
mafanikio yako.
Fanya
ufanyalo, futilia mbali ujinga wote ambao upo kwako. Ukifuta ujinga utakuweka
huru na utaishi maisha ya mafanikio. Wajinga ndio waliwao na ujinga
haumfanikishi mtu, tadhari usiwe kichaka cha ujinga, UTAKWAMA.
2. Kwa
mawazo uliyonayo ujue kabisa yanatengeza dunia yako, yanatengeneza maisha yako
au yanaumba maisha yako. Swala la kuwa makini sana kwako ni nini ambacho
unakiwaza kila wakati.
Kama
unawaza upuuzi mwingi, ujue kabisa ndio maisha yako unayabomoa na kuyaharibu
kabisa. Kuwa makini na kile ukiwazacho maana hicho kitaleta matokeo ya maisha
yako hata kama matokeo hayo huyapendi.
3. Kama
unaona matokeo ya nje yanaathiri maisha yako kwa namna moja au nyingine, basi
huhitaji sana kulalamikia matokeo hayo ya nje, bali unachotakiwa kufanya ni
kuweka juhudi za kutawala mawazo yako.
Msingi
wa maisha yako unaanza na mawazo yako, ukianza kutawaka mawazo yako kwa uhakika
na vitu vingine vya nje utavitawala kwa uhakika. Anza kutawala mawazo yako
kikamilifu ili ufanikiwe.
4. Kila
kitu kinaanzia kwenye mawazo, uzuri au ubaya wa kitu unaanzia kwenye mawazo
yako. Kama unaona kitu fulani ni kibaya kwako, kuna mwingine anaonaona kitu
hicho ni kizuri kabisa.
Akili
yako inaona kutokana na wewe jinsi unavyoamua akili hiyo iweze kuona. Kama
unaiona bahari ni sehemu mbaya, wengine wanaona bahari sehemu nzuri ya kuvua
samaki, ni suala la mtazamo wako tu.
5. Furaha
ni kitu ambacho unakipata kwanza ndani yako. Furaha kwa lugha nyingine ni
uchaguzi ambao wewe unaamua kwamba sasa nataka kuwa na furaha ya namna hii.
Furaha si kitu ambacho kinatoka nje yako. Furaha ni wewe unayoiumba ndani yako.
Kama
unasubiri hadi ukamilishe mambo fulani hivi, halafu ndio uwe na furaha, hapo utakuwa ni sawa na kujidanganya. Kwa
nini ninasema hivyo ni kwa sababu, furaha ni kitu ambacho ni matokeo ya wewe na
si nje yako, fikiri hili na tengeneza furaha yako.
6. Pamoja
na kwamba maisha yanaonekana ni magumu,
lakini kipo kitu ambacho unaweza ukafanya
na kitu hicho kikabadili maisha yako na kuwa bora kabisa. Acha kuendelea
kukazana kusema maisha ni magumu, fanya kitu.
Kuendelea
kukaa tu na kujiimbia wimbo wa maisha ni magumu, hiyo haitakusaidia sana. Amka kutoka
kwenye usingizi, amua kuchukua hatua kwa kufanya kitu ambacho kitakutoa kwenye
ugumu wa maisha uliopo.
7.
Mara nyingi mafanikio makubwa yoyote yale yanakuja kutokana na kufanya mambo
ambayo watu wengi hawawezi kufanya. Kama jambo unalolifanya kila mtu
analifanya, kufanikiwa kwake inakuwa ni ngumu kwa sababu ya ushindani wake
unakuwa mkubwa pia.
Kuwa
mtu ambaye unathubutu, kuwa mtu ambaye utajitoa mhanga kufanikisha jambo lile
ambalo kila mtu anasema hawezi. Huhitaji maarifa ya ziada au kitu kingine
tofauti, ni wewe tu kuamua kujitoa na kusema moyoni mwako kwamba nafanya na
naweza pia, DO WHAT CAN’T BE DONE.
8..
Mara nyingi mategemeo bora ya maisha
yako ya kesho yanatokana na uzoefu
ulionao. Kama kwa siku za hivi karibuni umekuwa na uzoefu mbaya wa kupitia
katika hali ngumu ni wazi na lazima utategemea mabaya tu katika maisha yako. Ikiwa
lakini umekuwa ukipitia mambo chanya , mategemeo yako yatakuwa pia yapo vizuri.
Dawa
pekee itakayoweza kukusaidia wewe uwe na mategemeo mazuri ni kuamua kujilisha
dozi kubwa sana ya mambo chanya kwenye maisha kila siku. Kwa kadri unavyozidi
kuwa chanya ndivyo mategemeo yako yanazidi kuwa bora. Hakuna mtu ambaye anaweza
kuwa na mategemeo bora kama hayuko chanya.
Fanyia
kazi mawazo haya yakinifu na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 21, 2018
Zifahamu Sura Mbili Ziletazo Mafanikio.
Habari ya muda huu mpenzi msomaji wa blogu hii ya DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nikuarike jamvini tuweze kujifunza kwa pamoja sura mbili zitakazo kuletea mafanikio.
kila kitu unachokiona katika dunia
hii kipo katika mwenekano wake. Na mwenekano huo ndio ambao hufanya viumbe
vyenye akili viweze kutambuana kwa kutumia muonekanao huo. Pia mwonekano huo
ndiyo hutumika kijenga picha kamili ya kitu halisi.
Kama ndivyo hivyo basi katika
kuyasaka mafanikio inahitajika mtu husika aweze kuvaa sura mbili ili kuyanasa
mafanikio hayo. Na sura hizo mbili ndizo zitakazokufanya wewe uweze
kujitofautisha na watu wengine.
Huenda ukawa hujanielewa bado
usipate shida ipo hivi sizingumzii umbo wala muonekano ulionao ndio
utaokupa mafanikio laa hasha. Bali nazungumzia ya kwamba ili uweze kupata
mafaniko yako unatakiwa kuwa na sura ya Mwalimu na sura Mwanafunzi pia.
Ninapozungumzia suala la kuvaa sura
ya mwalimu, kwanza tambua ya kwamba mwalimu si yule anayefundisha darasani
pekee yake la hasha, bali mwalimu mzuri ni yule aliyelewa kisha kuyafanyia kazi
yale ambayo amelewa kisha kuwafundisha wengine.
Hii ina maana ya kwamba kile kidogo
ambacho unakifahamu kisiwe siri yako bali weka mikakati thabiti ambayo watu
wengine wataweza kunufaika na hicho unakijua. Huenda kwako ukakiona ni kidogo
sana ila tambua ya kwamba wapo baadhi ya watu kwa hicho unachokijua japo wewe
unakiona ni kidogo kwao ni kitu kikubwa sana. Hivyo kila wakati jifunze
kuwa mwalimu kwa watu wengine.
Sura ya pili ambayo unatakiwa kuwa
nayo ni sura ya mwanafunzi. Pamoja na kuwa mwalimu lakini elimu haina mwisho
hivyo endelea kuwa mwanafunzi , huku ukizingatia ya kwamba mwanafunzi bora ni
yule ambaye yupo tayari kujifunza katika mazingira yeyote yale.
Lakini mwanafunzi huyu ili awe
mwanafunzi ni lazima pawepo na utayari kutoke ndani ya nafsi ya mtu husika,
kwani kama mtu atalazimishwa kujifunza atashindwa kuyafanyia kazi yale ambayo
amejifunza.
Lakini pia mwanafunzi makini ni yule
mwenye kutambua ni nini maaana ya uanafunzi, yaani awe tayari kulipa gharama ya
pesa na gharama ya muda kwa kitu anachotaka kukifahamu. Kufanya hii ndiyo nguzo
ambayo kila unayemuona ana mafanikio imemsadia kwa namna moja ama nyingine kuwa
hivyo alivyo leo.
Kila kitu ambacho unakiona mbele ya
macho yako tambua kuwa kuna mtu aliwekeza gharama fulani katika kitu hivho,
hadi kupelekea kitu hicho kuwa hivyo kilivyo leo.
Hivyo ndugu yangu naomba nikwambie
ya kwamba mafaniko ya kweli yanajengwa na sura hizo mbili ambazo nimekwisha
kukueleza yaani kuwa mwalimu lakini pia kuwa mwanafunzi. Ukiyazingatia hayo
utaishi maisha yenye tija katika sayari hii ya dunia.
Ndimi: Benson Chonya
Jul 20, 2018
Dalili Tano (5) Zitakazokuonyesha Kwamba Upo Kwenye Njia Sahihi Ya Mafanikio Yako.
Kila mtu mwenye nia ya kutafuta mafanikio, kuna wakati anakuwa ana shaka kwamba je, ‘kweli nipo kwenye njia sahihi ya kufanikiwa au hapana.’ Hali hii hujitokeza kwa sababu, njia ya mafanikio inakuwa in changamoto nyingi sana.
Kuna
wakati inafika kutokana na changamoto hizo, wengi huanza kukata tamaa na kuanza
kujiuliza maswali kweli njia hiyo au hicho wakifanyacho kinawafikisha kwenye
mafanikio yao, au kinawatoa nje kabisa ya mafanikio.
Hali
kama hii inajitokeza kwa wengi sana si kwako tu, bali hata kwa watu waliofanikiwa ikiwemo pamoja na
mamilionea hufika wakati wakijiuliza je, kwa kile wakifanyacho kwa wakati huo
kinawafikisha kwenye mafanikio mengine ya juu zaidi au hapana.
Kitu
cha kujiuliza zaidi, utajuaje kwamba upo kwenye njia sahihi ya mafanikio yako?
Hiki ndicho kitu ambacho nataka ujifunze kupitia makala haya ili tena usiwe na
shaka. Kama utakosa dalili hizo kabisa miongoni mwa hizi ujue upo nje ya
mafanikio.
Zifuatazo
Dalili Tano (5) Zitakazokuonyesha Kwamba Upo Kwenye Njia Sahihi Ya Mafanikio.;-
1. Kama wewe ni king’ang’anizi.
Mafanikio
kila wakati yanawapendelea na kwenda kwa watu ambao ni ving’ang’anizi na ambao wana nidhamu ya kujua kile
wakitakacho na kukifanya kwa muda mrefu. Hakuna mafanikio yanayokwenda kwa mtu
ambaye si king’ang’anizi.
Mfumo
na njia unayoipitia ya ung’anganizi ndio inayotabiri kwamba wewe unakwenda
kufanikiwa. Nafasi yako ya kufanikiwa itakuwa kubwa sana kama ni
king’ang’anizi, tofauti na yule ambaye si king’ang’anizi kwani mtu huyo lazima
atashindwa.
Ukishajua
kile unachokitaka vizuri, ni vyema ukawa king’ang’anizi kwani ni dalili tosha
ya kwamba kitu hicho ukitakacho utakipata. Ukikosa ung’ang’anizi, ujue kabisa
hautaweza kufanikiwa hata kama ungeweka juhudi kubwa sana.
2. Kama una mahusiano sahihi na pesa.
Mahusiano
hayaishii tu kwa watu lakini pia ili kufanikiwa, unatakiwa kuwa na mahusiano
sahihi na pesa. Si kwa sababu unapata pesa ukaamua kuzitumia pesa hizo hovyo
hovyo na kufanya vitu vya ‘biashara
kichaa’ ambazo hata hazieleweki.
Mahusiano
sahihi yanakuja kwa wewe kutuliza akili yako, kwa kila pesa unayoipata kuiwekea
akiba hata kama ni kidogo sana, kuwekeza kwa busara na mengine kama haya.
Unapokuwa hauna mahusiano sahihi na pesa, huwezi kufanikiwa.
Unatakiwa
ujikague na kujitathimini, je unayo mahusiano sahihi na pesa. Kila unapoangalia
matumizi yako, je, yamekaa sawa? Kama ukiona una mahusiano sahihi na pesa, basi
ujue upo kwenye njia sahihi ya kuweza kufikia mafanikio yako.
3. Kama una mahusiano sahihi na watu
sahihi.
Kupata
mafanikio kunategemea mambo mengi sana, ikiwemo mojawapo la msingi sana ni kuwa
na watu sahihi. Kuwa na mahusiano na watu sahihi ni kitu cha muhimu sana katika
kukupa mafanikio uyatakayo maishani mwako.
Watu
sahihi wanakuwa wanakupa chachu na hamasa kubwa ya kukupeleka mbele
kimafanikio. Unapowakosa watu hao unakuwa unatoka nje ya mafanikio yako na
mwisho wa siku utashangaa umeshindwa vibaya sana.
Jiangalie
wewe mwenyewe na ujiulize je, una timu sahihi inayokuzunguka ya watu ambao
watakusaidia kukupa mafanikio yako? Kama huna timu hiyo itafute, kwani dalili
mojawapo inayoonyesha kwamba utafanikiwa ni watu sahihi ulionao.
4. Kama unajua mapema kile kinachofanya
kazi.
Watu
wenye mafanikio wanajua mapema sana yale mambo yayofanya kazi kwao na yale
ambayo hayafanya kazi. Kama kuna jambo wanalifanya, wakigundua jambo hilo
linawapeleka eneo ambalo si sahihi hukimbia sana na kutafuta kitu kingine.
Kile
kitakachokufanya ujijue pia uko kwenye njia sahihi ya kutafuta mafanikio yako
ni kule kuwa makini na kujua kile unachokifanya kama kinafanya kazi yaani
kinaleta matunda ambayo unayataka na kwa muda mwafaka unaoutaka wewe.
Ni
jukumu lako kukagua kile unachokifanya na kujiuliza maswali ya msingi, je, hiki
nikifanyacho kinafanya kazi au hakifanya kazi, kujiuliza maswali haya
itakusaidia sana kujua njia ya mafanikio unayopita ipo sahihi au haipo sahihi.
5. Kama una imani ya kufikia mafanikio
yako.
Imani
ni moja ya kitu kikubwa sana ambacho kinaweza kikakufikisha kule kwenye
mafanikio yako. Kila unapofikiria ndoto yako kama una imani kuna kitu ambacho
unajiambia ni lazima nitafanikisha hili au ni lazima nitafanya jambo lile.
Ile
imani unayojiambia wakati unatafuta mafanikio, hiyo ndio imani unayatakiwa kuwa
nayo. Imani hii ya kuweza haiji kwa bahati mbaya, bali inakuja pale unapokuwa
na mipango imara na kutambua jinsi unavyoweza kufikia ndoto zako.
Nikuulize
hapo ulipo una imani ya kuamini kwamba utafikia ndoto zako. Imani hii hata kama
huna, unatakiwa ujue jinsi ya kuweza kuimiliki ili ikusaidia kufika kule
unakotaka kufika. Mafanikio yako yanahitaji sana uwe na imani hii ya msingi.
Kwa
maelezo haya yakinifu, hizi ndizo dalili za msingi za kujua kama upo kwenye
njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio. Fanyia kazi hiki ulichojifunza na
chukua hatua mathubuti zitakazoweza kukusaidia kufikia ndoto zako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa
mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767
048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 19, 2018
Sababu Nne (4) Kwa Nini Hutakiwi Kujilinganisha Na Watu Wengine.
Hapo ulipo hebu jiulize swali hili? Bado unaendelea kujilinganisha na watu wengine? Inawezekana ukawa unajilinganisha na watu wa familia yako, rafiki zako au jirani zako. Tabia hii ya kujilinganisha ipo sana kwa wengi.
Kwa
bahati mbaya sana tabia hii ya kujilinganisha chanzo chake kikubwa kimeanzia
tokea ukiwa mtoto. Ukiwaangalia watoto wanajilinganisha sana na wenzao kwa
mambo mengi kama kwenye mavazi waliyonayo, midoli wanayochezea, nyumba wanayoishi
na vinginevyo.
Kwa
sababu hiyo hujikuta inapelekea unapokuwa mtu mzima unaanza kusema siwezi hiki
au siwezi kile au mimi si bora katika jambo lile, lakini hapa unaona yote hiyo
inatokana na kujilinganisha. Tabia hii
ya kujilinganisha kwa maendeleo ya mafanikio yako si nzuri.
Kivipi
tabia hii si nzuri ya kujilinganisha na wengine, zifuatazo ni sababu za msingi
ambazo unatakiwa ujue kwa nini kujilinganisha hakufai.
1. Kujilinganisha na wengine, inakupozea
furaha yako.
Kwa
jinsi unavyozidi kujinganisha na watu wengine, hiki ni kitu ambacho kitakupotezea
furaha yako pasipo kujua. Kuna maeneo ambayo unatakuwa unajiona hufai ama umepungukiwa
vitu fulani hivi kwa sababu ya kujilinganisha.
Siri
ya kuweza kudumisha furaha yako, acha kujilinganisha sana na watu wengine. Ishi
maisha yako na kimbia mbio zako mwenyewe ambazo utaziona mbio hizo zitakusaidia
kuweza kufanikiwa na kufikia mafanikio yako makubwa.
2. Kujilinganisha na wengine, inakuzuia
usisonge mbele sana.
Unapokuwa
unajilinganisha na watu wengine badala ya kuweka juhudi za kukusaidia kusonga
mbele, juhudi hizo unazimaliza kwa kujilinganisha. Matokeo yake unajikuta
unadumaa badala ya kusonga mbele sana unaishia palepale.
Hata
ikitokea unajilinganisha na wengine na ukafanikiwa kusonga mbele, pia hutasogea
sana, badala yake utajikuta unaishia katika eneo lile lile ambalo wale unajilinganisha nao wamefika
katika eneo hilo.
3. Kujilinganisha na wengine, hakuwezi
kukubadili wewe.
Kuna
watu ambao wanakuwa wanajilinganisha sana katika eneo la sura, hasa kwa wanawake.
Hata ukijilinganisha vipi, lakini elewa utabaki wewe kuwa wewe. Hakuna
kitakachobadilika, hautaweza kubadili sura yako.
Kama
unajilinginisha kwa hivi, unatakiwa kujua unajipotezea muda. Kazana na mambo
yako na usiendelee na mambo ya wengine au uzuri wao. Kazana sana kubadili yale yaliyo yako na si kukazana
kujibadili wewe kupitia wengine ni hatari kwako.
4. Kujilinganisha na wengine,
kunakupotezea ubora wako.
Utaupata
ubora wako na utaboresha maisha yako, kama unakazana kuwa bora wewe kuliko
ilivyokuwa jana yako. Kujilinganisha na wengine utajipotezea sana ubora wako,
maana utafanya kama wale unaojilinganisha nao na hautavuka sana.
Hizi
ndizo sababu za msingi za kwanini hutakiwi kujilinganisha na wengine. Fanyia
kazi sababu hizi na kuanzia sasa anza kuishi maisha yako wewe kama wewe.
Ukumbuke kuendelea kujilinganisha na wengine huko ni kujipoteza.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 18, 2018
Kama Utatumia Mambo Haya Hovyo, Utakwama Sana.
Muda wako ulionao, nguvu zako ulizonazo na umakini wa mambo ulionao, ni moja ya mambo ambayo yana nguviu sana katika kubadili maisha yako au kuharibu maisha yako kwa namna ambayo hata wewe inaweza kukushangaza.
Jukumu
lako kubwa ulilonalo, ni kufanya juu chini na kuyatumia mambo hayo kwa
ukamilifu wake ili yakupe maisha unayoyahitaji, hapa nikiwa na maana maisha ya
mafanikio. Kama ila utayatumia mambo hayo hovyo, hakuna ubishi utashindwa sana.
Pengine
jiulize je, kuna kitu ambacho katika hali si ya kawaida kinakuingilia na
kukupotezea muda wako, nguvu zako na umakini wako wa kuelekea kwenye ndoto
zako? Kama kitu hiki kipo tafuta namna jinsi utakavyoweza kuachana nacho.
Kama
utaendelea kung’ang’ana na kitu ambacho kinakupotezea muda, nguvu na umakini
wako pasipo manufaa yoyote, nikwambie tu hapo unajitafutia balaa au njia ya
kwenda kwenye shimo la kushindwa kwako vibaya kimaisha.
Tumia muda ulionao, nguvu ulizonazo na umakini wako kukusaidia kufanikiwa. |
Waangalie
watu wote wanaoshindwa kwa kitu chochote. Watu hao wanaoshindwa wanasifa moja
kubwa sana ambayo ni kufanya mambo ambayo yanapoteza muda wao, nguvu zao na
umakini wao katika kuelekea mafanikio wayatakayo.
Haya
ni mambo yanaonekana kwa juu juu hayana athari kubwa katika maisha yako, lakini
kiuhalisia mambo haya ndio yanaua ndoto za watu wengi na kujikuta ni kilio cha
kuishi maisha yasiyo ya mafanikio sana karibu wakati wote.
Ukitaka
kubadili hali hii na iwe ya manufaa kwako, kuanzia leo anza kutumia muda wako, nguvu
zako na umakini wako wote katika mambo
ambayo unaamini yatakusaidia wewe kukubadilisha na kukupeleka sehemu nyingine
ya mafanikio.
Ikiwa
unachukua hatua, hakikisha unachuka hatua ambazo hazikupozei muda wako, nguvu
zako na umakini ulionao katika kuelekea mafanikio yako. Ikitokea unachukua
hatua ambazo zinakupotezea mambo hayo, basi kushindwa kunakuhusu sana wewe.
Ikiwa
pia unawaza, una panga mikakati yako, hakikisha sana, kuwaza kwako kusiwe unawaza tu kwa sababu wewe
ni binadamu. Jitahidi kuwaza kule ambako
kunakuletea manufaa na si kukupotezea muda wako, nguvu zako na umakini.
Kitu
ninachotaka unielewe hapa kwa umakini ni kwamba muda ulionao, nguvu ulizonazo na
umakini ulionao, ndivyo vitu ambavyo vitakutambulisha wewe kama unafanikiwa au
unashindwa na hiyo yote inatokana na jinsi unavyovitumia vitu hivyo.
Kila
wakati, tumia vitu hivi viwe daraja la kukusaidia kufanikiwa kwako na si
kukuangusha. Kama nilivyosema mwanzoni, kama utatumia vitu hivi hovyo kwenye
maisha yako ya sasa, basi andika utashindwa sana na hautafanikiwa kwa sehemu
kubwa maishani mwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa
mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767
048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 16, 2018
Maisha Yatakuwa Bora Na Mazuri Sana Kwako Kama Utafanya Mambo Haya…
Maisha yatakuwa mazuri kwako, kama utajiruhusu kuishi maisha mazuri kwa kufanya yale yaliyo ya msingi na yanayoweza kujenga maisha yako yakawa mazuri.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako, kama nguvu zako nyingi za uzingativu unaziweka kwenye
mambo chanya na ambayo yanaleta mabadiliko kwako na kwa wengine.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako kama unaweka nguvu zako za uzingativu pia katika kutoa
matokeo chanya, ambayo yanakubadilisha wewe na yanawabadiisha watu wengine pia.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako kama utaondoa mitazamo yako potofu uliyonayo, pamoja na
kinyongo kwa wengine na kuanza kuuona usawa kwa wote.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako, kwa sababu, leo hii unayo tena nafasi na fursa ya kuishi
na kufanya chochote ukitakacho pasipo kuzuiliwa na kitu cha aina yoyote.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako, kwa kuona mazuri kwa wengine na kubali kujifunza
kutokana na mazuri hayo na si kubaki wewe kama wewe.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako, ikiwa utakubali kujifunza kutokana na makosa na kukubali
kujirekebisha na kisha kusonga mbele kwa mafanikio.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako, kwa wewe kukubali kuwasaidia watu wengine kuweza kufikia
ndoto zao na kwa kufanikiwa kwao na wewe utajikuta ukipiga hatua.
Maisha
yatakuwa mazuri kwako na ya Baraka, kama utaamua kuwa mtu wa shukrani na sio
mtu wa kunung’unika kila wakati kama ilivyo mazoea ya wengi.
Ruhusu
siku ya leo iwe maalumu kwa ajili ya kutengeneza maisha yako ya kesho na yakawa
bora na ya mafanikio makubwa.
Hata
siku moja usikubali kubaki hapo ulivyo kwa kuwa king’ang’anizi kwa mambo
yanayoharibu maisha yako ya leo na kesho.
Nguvu
ya kuumba maisha yako na kuwa bora unayo. Kikubwa kwako ni kuweka juhudi na
kujiruhusu ili uwe na maisha ya namna hiyo kwako.
Ikiwa
utajiruhusu kufanya maisha yako yawe bora na huku ukichukua hatua, ndivyo
itakavyokuwa na maisha yako yatakuwa bora vivyo hivyo siku zote.
Boresha
maisha yako, kwa kuruhusu yale yaliyo mema yatokee kwako, na amini hilo unaweza
na hakuna shaka, anza sasa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)