Aug 26, 2021
Hizi Ndizo Biashara Kubwa Tatu, Ambazo Ukizifanya Lazima Uwe BILIONEA.
Zipo biashara kubwa tatu, ambazo ukizifanya lazima uwe BILIONEA ikiwa utajipa muda. Hizi ni biashara ambazo hazijawahi kumtupa yeyote.
Kwa nini nimekwambia hivyo, kwa sababu hizo ndio biashara ambazo
zimetengeneza mabilionea wengi barani Afrika na duniani kote.
Moja, biashara ya viwanda vidogo na vikubwa.
Ikiwa kweli umejikuta kwenye biashara za viwanda, lazima uwe tajiri. Hiyo iko hivyo kwa sababu, wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza, faida kupata kwako ni lazima na huwezi kukwepa.
Tunaposema viwanda hatumaanishi lazima uwe na mabilioni ya pesa ndio uanze, vipo viwanda vidogo, ambavyo hata havihitaji mtaji mkubwa sana na unaweza ukaanza navyo.
Kwa mfano, mashine ya kutengeneza sabuni ya unga, gharama zake hazizidi MILIONI tatu. Zipo mashine nyingi za kutengeneza bidhaa ambazo gharama zake ziko chini sana.
Kama una wazo la kutaka kuuza bidhaa fulani hivi, acha kuwaza tu kuwa mlanguzi, waza utawezaje kutengeneza bidhaa hizo nakupata mauzo makubwa ya kujaza pesa mfuko.
Mbili, biashara ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.
Kama utaweza kumudu kuagiza bidhaa nje ya nchi kama China, Dubai, Uturuki na kwingineko, basi ipo fursa kubwa sana ya kupata pesa nje nje na za kutisha kuliko unavyofikiria.
Matajiri wengi Tanzania, wamejipatia pesa kwenye fursa hii ya kuagiza. Siri iliyopo unapoagiza bidhaa nje unapata bidhaa kwa bei nafuu sana ambapo ikiletwa huku lazima upige faida iliyosimama.
Huhitaji kulaza damu ni kuamua kuchangamkia fursa, na kujifunza juu ya kuagiza, eidha iwe kwa njia ya mtandao au kuamua kwenda kabisa kama China ikiwa pesa mfukoni ipo.
Nakuhakikishia ukifanya kazi hii tu peke yake ya kuagiza bidhaa nje kwa muda wa miaka mitano mfululizo na ukawa 'siriaz, haswa, kama usipokuwa tajiri basi utakuwa umelogwa sana.
Tatu, biashara ya kilimo biashara.
Ikiwa kama kweli utajikuta kwenye kilimo biashara, iwe kilimo wazi au kilimo Cha hema, uhakika mkubwa wa kufanikiwa na kuwa tajiri upo na tena kwa uhakika wote mkubwa.
Uzuri wa Tanzania ardhi bado kubwa na pia kuna maeneo ambayo mvua inanyesha mara mbili na kilimo kinakubali kama Tanga, pwani na mikoa ya kusini, pia kuna mito mingi sana ya maji.
Lakini hata hivyo hata mwenye maeneo ambayo hayana mvua ukifanya kilimo kama cha bustani kwa kumwagilia pia uwezekano wa kufaulu upo sana. Kikubwa kwako ni kujiwekea mikakati.
Jifunze kwa waliofanikiwa kupitia kilimo biashara watakupa Siri zitakazoweza kukutoa kwenye umaskini wako. Acha kuwa mbishi eti kilimo hakifai kumbe ulilima mara moja na kukimbia.
Hizi, ndio biashara ambazo ukizifanya kaa ukijua utajiri hauwezi kuukwepa. Ni jukumu lako kuchukua hatua na kufanyia kazi yote ukiyojifunza kwenye makala haya.
Kwa mahitaji ya mashine yoyote au bidhaa yoyote ya kuagiza nje
ya nchi, kwa mahitaji ya msaada wowote wa kimawazo usisite kuwasiliana nasi kwa
0687449428.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.