google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 24, 2021

Hili Ndilo Tatizo Kubwa Ulilonalo Linalokukosesha Furaha Na Mafanikio.

No comments :
Unaweza ukawa unakosa sana furaha yako na pia hata kukosa mafanikio kwa sababu moja tu ya wewe kushindwa kuweka utulivu kwenye eneo moja. Watu wengi si wazuri sana katika kuweka akili zao eneo moja. Hawa ni watu wanaoishi jana, au ni watu wanaoishi kesho na kusahau leo yao iliyo ya msingi.
Kwa sababu hiyo hapa ndipo linapoibuka tatizo linawakosesha watu wengi furaha na mafanikio, tatizo hilo si lingine bali  ni la kutokuishi sasa. Watu wengi hawaishi sasa, ni watu wanaotaka kuishi jana au kesho zaidi. Wakati nguvu kubwa ya mafanikio inatengenezwa sasa na kila tukio linatokea sasa.
Ukiwafatilia watu wengi kwa sasa hawako tayari kuweka mawazo yako kwa kile wanachokifanya kwa asilimia mia moja. Utakuta mtu anafanya jambo la aina fulani sasa, lakini mawazo yake yapo kwenye jambo lingine la kesho au jambo la jana pengine ambalo lilimuuza, lakini utakuta mtu huyu analiwaza jambo hilo.

Inapotokea ukahamisha mawazo yako sasa na kuwaza jana au kesho na kushindwa kuitumia sasa yako kwa vizuri, ni wazi si rahisi mtu wa namna hii kuwa na furaha wala mafanikio makubwa sana. Kuwa na mawazo ya nyuma kama kuna vitu ulifanya vibaya yanaweza yakakuhuzinisha na mawazo ya mbele pia yanaweza yakakutia hofu kubwa.

Mpaka hapo unaona siri ya wewe kuwa na furaha na mafanikio mazuri kwako, ni kwa wewe kuishi sasa. Kama nilivyosema, ipo nguvu kubwa sana ya kuishi sasa kwani hapo ndipo nguvu kubwa ya  kimafanikio inapozaliswa. Jaribu kujiuliza kama kuna kitu kinazalishwa nje ya sasa, utagundua kila kitu au kila jambo ni lazima liweze kuanzia sasa.
Hata majibu ya changamoto zetu tunazozipitia unatakiwa kukumbuka zinapatikana sasa. Huwezi kupata majibu ya changamoto hizo kwa kesho au kesho kutwa, bila kuanza kuishughulisha akili yako sasa. Kila majibu ya changamoto yanaanza kupatikana kwanza sasa. Unatakiwa kuishi sasa, kwa kuweka mawazo yako eneo moja na utashangaa ukiona mafanikio makubwa sana yakitokea kwako.
Ikiwa kila wakati unawaza sana kesho inayokuumiza au kuwaza mambo yaliyopita, na kusahau sasa uliyonayo hapo ujue akili yako inakuwa inakutawala na wewe huitawali akili. Ili uweze kuitawala akili yako vizuri, hutakiwi kuyumba hata kidogo, akili yako unatakiwa kuielekeza kwenye sasa yako kwa usahihi sana.
Kuna wakati kuendelea kuwaza vitu vya kesho vinavyokupa hofu au jana ni kutengeneza matatizo yetu wenyewe. Kitu cha msingi kwa wewe ni kutuliza akili yako na kuhakikisha kila wakati unashughulika na sasa yako kwa uhakika sana. Acha kuyumbishwa mawazo yako, waza sasa kwa manufaa ya maisha yako.
Kabla sijaweka kalamu chini nikukumbushe, ukiitumia sasa yako vizuri, ukiishi sasa vizuri, utafanikiwa. Tambua, kila mmoja anaweza kufikia mafanikio yake ikiwa mtu huyo atahitaji mafanikio hayo. Na ikumbukwe hatma ya maisha yetu tunayo sisi, maisha yetu yawe ya namna gani uchaguzi ni wetu. Kwa nini basi tusichagua maisha ya mafanikio ya kweli? Ishi sasa na ufanikiwe zaidi.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.