Aug 3, 2021
Kama Hutaki Kufanya Kitu Hiki, Sahau Kupata Mafanikio.
Watu wengi hawataki kufanya kazi kubwa, ila wanataka mafanikio. Ni watu ambao kila wakati wanatafuta mafanikio makubwa, lakini hawataki kuweka kazi kubwa ya kuwapa mafanikio hayo.
Hiyo inakuwa ni sawa na mtu ambae anataka kuvuna na hajapanda kitu. Kama utaka mafanikio makubwa lakini wakati unachokifanya ili kupata mafanikio hayo hakionekani, unajidanganya wewe.
Ili kupata mafanikio makubwa unayoyataka, weka kazi sawa sawa na mafanikio unayoyataka. Ukiweka kazi sawa sawa na mafanikio unayoyataka uwe na uhakika utaweza kufanikiwa. Weka kazi, mafanikio utayapata.
Hakikisha kila wakati mafanikio yako, yaendane sambamba na kazi unayoweka. Kama itakuwa kinyume cha hapo nakwambia utakuwa unajidanganya sana. Amua kuweka kazi na utapata mafanikio makubwa pia.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio
ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa
kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha
yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.