Dec 29, 2015
Muda Sahihi Wa Mafanikio Yako Ni Huu Hapa.
Bila
shaka umewahi kuliona hili kuwa wengi wetu tumekuwa tukitafuta sana muda sahihi
wa kuweza kufanikisha mipango au malengo yetu tuliyojiwekea. Muda huu ambao tumekuwa
tukiutafuta, mara nyingi hupelekea sisi
kufanya maandalizi mengi sana ya kusubiri mambo mengi yakamilike ndio tuanze
uwekezaji ule tunaouhitaji.
Lakini
kitu kisichoeleweka kwa wengi ni kwamba siku zote hakuna wakati sahihi wa wewe
kuanza jambo unalotaka kulifanya zaidi ya sasa. Kama kuna jambo unalotaka kulifanya
au kulitimiza ni bora ukaanza kulifanya hivyohivyo sasa bila kuweka maandalizi
mengi sana kama unavyofikiri. Tambua siku zote muda sio rafiki sana na
wewe hadi ukusubiri sana.
Kosa
kubwa wanalolifanya watu wengi bila kujua ni kule kufikiri kuwa kuna vitu fulani
hawana ambavyo ni lazima wavikamilishe kwanza ndipo waanze kufanya kile
wanachokitaka kukifanya hadi kufikia mafanikio. Kama haya ndiyo mawazo yako kwa
namna fulani utakuwa unachelewa.
Kwa
sasa huhitaji kusubiri taarifa zaidi, huhitaji kusubiri muda zaidi ya ulionao
wala huhitaji eti hadi uwe una mtaji wa kiasi fulani ndiyo uanze biashara.
Unachotakiwa kufanya sasa ni kuanza na kile ulichonacho. Mambo mengine
unayofikiria sana hayajakaa sawa, yatakaa sawa wakati umeanza kufanya.
Utakuwa
unajidanganya kama utakuwa unafikiri ukijiandaa sana hutakosea na utakuwa
kamili kila eneo, makosa na kujifunza ni lazima. Kwa hiyo lilokubwa kwako ni
kuwa tayari kufanya kile ambacho unaona kitakufanikisha tena kwa haraka kuliko
ukasubiri sana.
Ukweli
wa mambo ulivyo ni kwamba hakuna muda sahihi unaokusubiri wewe wa kuanza
kufanya jambo unalolitaka kama ulionao sasa. Huu ndiyo muda sahihi kwako wa
kufanya mambo yako. Jiulize kama hutafanya sasa utafanya lini? Je, hauoni
kwamba utazidi kujichelewesha kufikia malengo yako makubwa kama utakuwa ni mtu
wa kusubiri?
Kama
umekuwa mtu wa kusubiri sana, leo tambua kitu kimoja hiyo imetosha. Sasa ni
wakati wa kuchukua hatua kwa kutumia kile kidogo ulichonacho kukufanikisha.
Acha kudharau kile ulichonacho, hata kama ni kidogo vipi kinuwezo wa
kukufanikisha. Tumia ulichonacho hadi kikupe mafanikio.
Weka
mawazo pembeni ya kushindwa na anza kujiamini kwa kile unachokifanya kuwa ni
lazima kikupe ushindi. Anza utekelezaji kwa kuchukua hatua kwa hatua kila siku
hadi uyaone mafanikio. Hivi ndivyo mafanikio yako yatakavyokuja na hakuna muda
wa kusubiri.
Kama
utaendelea kusubiri elewa kabisa unajichelewesha kwenye mafanikio yako
mwenyewe. Fanya mafanikio yako yaonekane sasa. Muda sahihi wa mafanikio yako
ni sasa. Chukua hatua siku zote hata kama ni kidogo lakini mwisho wa siku
ushindi utakuwa ni wako.
Tunakutakia
ushindi katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO
kwa kujifunza na kuelimika zaidi.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Dec 16, 2015
Je, Umefanya Nini Mwaka 2015?
Mwaka 2015 unakaribia kuisha, kwani zimebaki wiki chache mwaka kuisha na
kuingia mwaka mpya wa 2016. Kwa mtu mwenye busara atajiuliza sana maswali
mbalimbali ya msingi kuhusiana na mwaka huu.
Maswali ya Msingi ya Kujiuliza:
·
Je nini/kipi ambacho
hutasahau mwaka 2015?
·
Je mwaka 2015
umeutumia vyema?
·
Je mwaka 2015
umeutumia kivipi katika kuboresha maisha yako na kupanga malengo yako?
·
Je ni vipi unavyopaswa
kubadili au kuboresha katika mwaka unaokuja?
Ni jambo la busara
sana kutafakari. Lakini msingi mkuu ni kuhakikisha kuwa; katika matendo yako,
maneno yako, na katika tafakari zako unapaswa kuzibadilisha kwa kuhakikisha
unazidi kuendeleza hali hizo tatu na kuziboresha. Ukiweza kuboresha mawazo
yako, matendo yako na maneno yako kiusahihi utaweza kubadili maisha yako vyema.
Hivyo kaa na tafakari, mwaka 2015 umeutumia kivipi. Ikiwezekana andika hata
katika kitabu chako au diary ya kumbukumbu itakusaidia kuhakikisha unapanga
malengo mazuri na unatambua maendeleo yako ya kimaisha.
Nov 25, 2015
Mambo 5 Yatakayokusaidia Kutokuwa Na Mawazo Mengi Yaliyopitiliza.
Kati
ya tatizo ambalo huwa ni kubwa na linawakabili baadhi yetu bila kujua ni tatizo la kuwa na
mawazo mengi. Wapo watu ambao huwa wanafikiria sana matatizo yao, shida zao au changamoto
zao kiasi kwamba kwa wengine hupelekea kama kuchanganyikiwa. Natambua umeshawahi
kukutana na watu wa namna hii mara kwa mara tu.
Kuna
ambao ulipokutana nao walikuwa ni watu wa kuongea peke yao njiani. Pia kuna
wengine ambao uliwahi kukutana nao wakiwa ni watu wa kujiinamia tu muda wote.
Lakini watu hawa chanzo chao kikubwa ni nini kila ulipowafatilia, hakuna tatizo
lingine, zaidi ya hili la kuwa na mawazo mengi ambayo yapo akili mwao muda
mrefu.
Kitu
kibaya kuliko vyote kwa binadamu ni kwamba, tatizo hili kwa bahati mbaya
linapoanza kwa mtu kuisha kwake huwa sio rahisi sana. Tuchukulie kwa mfano
umekuwa una mawazo mengi ya mara kwa mara yaliyokupelekea ukaanza kuongea
mwenyewe. Tatizo kama hili likisha kuanza, kukuisha litachukua muda mwingi au linaweza lisiishe
kabisa na ukawa ndiyo umechanganyikiwa. kwa hiyo ni lazima kuepuka kutokujiweka katika hali ya kuwa na mawazo mengi hasa kutokana na ukubwa wa athari zake.
Sasa
unawezaje kutoka kwenye tatizo hili la kuwa na mawazo mengi?
1. Ishi sasa.
Wengi
wanapata tabu na kujikuta wakiwa na mawazo sana kutokana na wao kuamua kuishi
jana au kesho. Hapa ili uweze kuondokana na mawazo yanayokutesa unatakiwa
kusahau kila kitu kinachokusumbua kiwe kimetokea jana au kiwe kinakuja kesho.
Kama kuna deni unalotakiwa ulilipe kesho lisahau mara na ishi sasa kesho hiyo ikifika
itaeleweka hapo hapo.
Ruhusu
mawazo yako yafikirie pale ulipo. Acha kujibebesha mizigo mingi ambayo huwezi
kuibeba kwa pamoja. Acha kujibebesha matatizo ya jana na ya kesho halafu yote
ukawa nayo leo. Kwa hilo hutaweza zaidi utazidi kuwa na mawazo kama uliyonayo
sasa. Weka maisha yako yawe huru kwa kuamua kuishi sasa na sio kesho.
2. Jijengee mitazamo chanya.
Siri
nyingine itayokufanya uishi kwa kutokuwa na mawazo mengi sana ambapo wakati
mwingine unahisi hata kuchanganyikiwa ni kwa wewe kujijengea mtazamo chanya.
Fikiria yale mambo yanayokufurahisha na kukupa matumaini. Acha kuweka fikira
zako sana kwenye jambo linalokusumbua, hiyo itakuongezea mawazo zaidi.
Kwa
jinsi utakavyoendelea kufikiria yale mambo yanayokupa furaha, ndivyo ambavyo
utajikuta mawazo mengi ambayo ulikuwa nayo yanazidi kupungua kidogo kidogo.
Kumbuka, unapata kile unachikzingatia. Kama unazingatia furaha basi basi
utapata furaha. Kama unazingatia matatizo halikadhalika utapata hayo hayo
matatizo kwenye maisha yako.
3. Kuwa makini na mawazo yako.
Katika
kipindi ambacho unakuwa na mawazo mengi zaidi, jambo ambalo unatakiwa kuchunga
sana ni mawazo uliyonayo. Ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini na jinsi
unavyoruhusu mawazo yako yaingie akilini mwako. Wengi ukumbuke huwa tunapata
mawazo hasi pengine kutokana na maneno ya watu ambayo huwa tumeambiw. Sasa hayo ni moja ya mambo ambayo tunayotakiwa
kuwa makini nayo sana.
Hata
hivyo, kumbuka mara nyingi jamii tunayoishi ni hasi sana hivyo kuweza kuwa chanya
wakati wote inaweza ikawa ni jambo gumu zaidi. Hivyo kitu cha kufanya ni
kuhakikisha kila mara na kila wakati kama mtu akikuuzi achana naye na usipeleke
hayo mawazo kichwani mwako moja kwa moja. Hiyo itakuwa njia rahisi sana ya
kukufanya usiwe na mawazo mengi akili mwako.
4. Badilisha mazingira.
Inawezekana
ukawa unazidi kuwa na mawazo zaidi kutokana na mazingira uliyopo. Kitu pekee
cha kufanya kwako ni kuhakikisha unabadili mazingira hayo yanayokuplekea uwe na
mawazo hayo. Unaweza ukaenda katika eneo tulivu kama baharini au ziwani kupata
upepo mwanana. Kwa mazingira kama hayo ni lazima mawazo yako yabadilike.
Kwa
hiyo ni lazima uendelee kutokung’ng’ania mazingira ambayo kwako siyo rafiki
yanayokufya uendelee kuwaza mawazo yaleyale kila wakati. Kaa mbali na mazingira
hayo hiyo itakusaidia sana katika hali ya kuweza kuondokana na mawazo hasi
yanakusumbua. Ukitumia mbinu hii itakupa matokeao chanya na ya muda mfupi
kuliko unavyofikiri.
5. Fanya tahajudi(Sala).
Ni
jambo zuri sana pale unapokuwa na mawazo ikiwa utafanya tahajudi au sala. Hiyo
itakusaidia kuyaweka mawazo yako katika hali tulivu zaidi. Unaweza ukafanya hili
kwa kutafuta eneo ambalo ni tulivu na ukawa unafanya sala au tajudi angalau kwa
muda mchache sana kwa siku. Hiyo itakusaidia kujenga kupunguza mawazo mengi
uliyonayo.
Nakutakia
siku njema na endelea kujifunza kila siku ila usikose kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia
matandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Nov 24, 2015
Kama Utatumia Kanuni Hii, Mafanikio Ni Yako.
Siku
zote elewa ukweli huu, chochote unachokifanya katika maisha yako kinauwezo wa
kukufanikisha. Hiyo haijalishi kitu unachokifanya ni kidogo au kikubwa kiasi
gani. Kitu cha kuzingatia ili kupata mafanikio hayo ni kukifanya kwa juhudi
zote huku ukitumia kanuni za mafanikio. Kanuni hizi za mafanikio zinapotumika
ni lazima mafanikio hutokeo.
Bila
shaka unajua hili na ni mara nyingi tumekuwa tukiongelea juu ya umuhimu wa kutumia
mbinu na kanuni mbalimbali za mafanikio ili kutufanikisha. Sababu ya kubwa ya
kufanya hivi ni kwa sababu kila zinapotumika matokeo chanya huweza kuonekana. Leo
hii napenda nikukumbushe kanuni moja nyingine ya mafanikio ambayo ukiitumia ni
lazima ibadili maisha yako kwa sehemu kubwa.
Kanuni
hii inasema ‘fanya kama kila mtu anakuangalia’.
Kwa kila jambo unalolifanya katika maisha yako lifanye kama vile mtu
anakuangalia. Kama ni malengo panga malengo yako ukiamini kabisa pembeni yako
kuna mtu anakutazama. Kama ni kupokea simu, pokea simu ukiamini kuna mtu
anakutazama. Kwa kila tendo na mwenendo mzima fanya hivi kama unatazamwa na mtu
mwingine.
Kwa
kufanya hivi, itakusaidia sana kufanya mambo yako kwa umakini mkubwa na utakuwa bora zaidi siku zote. Hebu jaribu kufikiria
wakati ambapo ulifanya kazi zako kwa kusimamiwa, hizo kazi zako ulizifanyaje?
Bila shaka ulifanya kwa umakini sana. Na ulifanya hivi kwa sababu ya kuogopa
kuharibu kile kitu ambacho ulikuwa ukisimamiwa na kuonekana wa ajabu.
FANYA KAMA KILA MTU ANAKUANGALIA |
Hivi
ndivyo kanuni hii inavyofaya kazi. Itumie kanuni hii, kwa kujijengea picha na kujitazama
wewe kama vile unavyotazamwa na mtu mwingine ukifanya mambo yako. Kwa hili bila
shaka hutaleta mchezo ni lazima uwe makini. Fikiria jambo hili pia, kama
ingekuwa inatokea malengo yako ukayaweka hadharani ni nini kingetokea? Bila shaka
ungekomaa sana mpaka yatimie. Unajua kwa nini? Kwa sababu usingekuwa tayari
kukubali kuchwekwa kwa kushindwa kutimiza malengo yako.
Mara
nyingi wengi wetu tunaharibu katika maisha yetu kwa sababu ya kujua kwamba eti
hatufatiliwi. Jifunze kujisimamia mwenyewe kwenye maisha yako kama vile ambavyo
unasimamiwa na mtu mwingine. Kumbuka siku zote hili katika maisha yako, ili
kufikia mafanikio makubwa. FANYA KAMA
VILE MTU ANAKUANGALIA.
Kwa
umejua hili jipe ahadi mwenyewe ya kufanya kila jambo kama vile mtu mwingine
anakuangalia. Sina shaka ukiweka picha hii vizuri kichwani mwako utajituma sana
na itakusaidia sana kufanikisha mambo mengi ambayo ingekuwa siyo rahisi kwako
kuyafanikisha kama usingekuwa na picha hii vizuri.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza na
kuhamasika.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Nov 23, 2015
Kama Utashindwa Kuyatawala Mambo Haya, Huwezi Kufanikiwa Tena.
Mafanikio siku zote hayaji kama ajali. Mafanikio ni safari ambayo huwa ipo hatua kwa hatua. Mafanikio kwa kawaida hayaji leo ghafla na kusema umefanikiwa, hapana. Mafanikio mara zote yanakuwa na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ili kufanikiwa.
Taratibu
hizo au sheria hizo zinaposhindwa kufuatwa hakuna tena mafanikio yanayoweza
kujitokeza zaidi ya kushindwa. Moja ya taratibu au sheria ambayo ni lazima
uifate na ikupe mafanikio ni ‘sheria ya
kutawala’. Ni lazima yawepo mambo ya kuyatawala kwenye maisha yako ili
ufanikiwe. Bila kuyatawala mambo hayo itakuwa ngumu sana kufikia mafanikio
makubwa.
Wengi
hujikuta wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutaka kujaribu kutawala kila
kitu au kushikiria kila jambo. Kwa maisha kama hayo inakuwa ni ngumu sana
kuweza kufanikiwa. Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa ni lazima umudu kutawala
mambo haya, ukishindwa kufanya hivyo sahau mafanikio.
1. Kutawala pesa.
Huwezi
kupata mafanikio kama matumizi yako ya pesa hayako sawa. Hili ni jambo linalowatesa
wengi na kuwasumbua. Lakini ili ufanikiwe ni lazima kutawala pesa na siyo pesa
ikutawala wewe. Unapokuwa una mudu kuitawala pesa inakusaidia katika mambo
mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza. Unataka maisha yako yote uishi kiumaskini, acha
pesa ikutawale.
TAWALA MUDA WAKO VIZURI. |
2. Kutawala hamasa.
Nguvu
kubwa ya mafanikio unaipata kutokana na wewe kuwa na hamasa kila siku. Hamasa
tunaweza tukasema kama ni mafuta ya kukusaidia kusonga mele. Mara nyingi hamasa
inapokosekana inakuwa siyo rahisi sana kuweza kufanikiwa. Kwani kazi kubwa ya
hamasa ni kukupa nguvu na kichocheo cha kuendelea mbele zaidi ya ulipo.
3. Kutawala kasi ya mafanikio.
Ni
uhimu kutawala kasi yako ya mafanikio yako. Unaweza ukajiuliza kivipi?sikiliza,
kasi ya mafanikio unaitawala kwa kuhakikisha unafanya jambo linalokusogeza
kwenye mafanikio kila siku. Kwa kufanya jambo hilo kila siku hata kama ni
kidogo hapo utakuwa unaendana sawa na kasi ya mafanikio unayoitaka. Ila kama
utashidwa kuitawala kasi hii na kushindwa kufanya jambo hata dogo ni lazima
uachwe.
4. Kutawala tabia njema.
Ili
uwe na mafanikio makubwa ni lazima uwe na tabia njema zinakusogeza kwenye
mafanikio kila siku. Ukiwa na uwezo wa kutawala tabia hizi za kimafanikio uwe
na uhakika ni lazima uweze kufanikiwa. Lakini kama utatawaliwa na mambo hayo
basi tegemea anguko kubwa sana kwenye maisha yako.
5. Kutawala muda.
Muda
ni kitu muhimu sana katika mafanikio yoyote. Pamoja na umuhimu wote huu wa muda,
kwa bahati mbaya sana wengi wanatumia muda vibaya. Kwa tatizo kama hili la kutumia
muda vibaya na kushindwa kutawala muda hupelekea maisha ya wengi kuharibika. Ukitaka
kujua hili vizuri, cheza na muda wako sasa, baada ya miaka kumi utaniambia nini
ambacho kitakutokea kwenye maisha yako.
Haya
ndiyo mambo unayotakiwa kuyatawala ili kufanikiwa kama ikatokea umeshindwa
kutawala jambo mojawapo kati ya hayo basi utakuwa umejiweka kwenye wakati mgumu
wa kuweza kufanikiwa.
Nikutakie
siku njema, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waendelee kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Nov 20, 2015
Jinsi Ya Kutambua Kipaji Cha Mtoto Wako Na Kukiendeleza
Hujambo mpenzi msomaji
wa DIRA YA MAFANIKIO na karibu sana katika siku ya leo kwa ajili ya kujifunza. Leo
katika makala yetu tutajifunza namna unavyoweza kutambua kipaji cha mtoto wako na
kukiendeleza. Na tunapozungumzia kipaji huu
ni uwezo anaokuwa nao mtu wa kufanya jambo fulani bila hata kwenda kujifunza shuleni.
Najua unaelewa hili vizuri.
Mara nyingi mtu
huzaliwa na uwezo huo na anapokwenda shule inakuwa ni rahisi kuweza kuuendeleza
kipaji hicho na kufanya jambo hilo kwa ufanisi sana. Sasa wewe kama
mzazi unawezaje kutambua kipaji cha mwanao na kukiendeleza? Ili kupata majibu
hayo ya nini unachotakiwa kufanya fuatilia yafuatayo katika makala hii;-
Kama mtoto wako anaongea kupita kiasi; Kuna watoto ambao huongea
kwa spidi sana na huwa hawachoki kuongea. Watoto hawa huongea mpaka anapokwenda
kulala na wengine huwa wanaongea mpaka usingizini. Huwa na tabia ya
kusimulia visa mbalimbali au kukueleza mzazi yote yaliyotokea mchana pengine
wakati wewe umeenda kazini au kwenye shughuli zako.
KUZA KIPAJI CHA MTOTO WAKO. |
Kwa mfano unapokutana na mtoto wa aina hii, hiyo hapo ni
dalili nzuri sana kwa watoto hawa kama kipaji chao kitaendelezwa vizuri na
kutokana na mwenendo huo wanaweza kuwa wanasheria,
waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na Mc wa majukwaani.
Jinsi ya kuwasaidia watoto wa aina hii;
1. Epuka kuwakatisha
tamaa kwa yale wanayoongea na kama yanakera mfundishe kuongea yanayofurahisha.
2. Unaweza kumwambia akusimulie visa mbalimbali wakati wewe
ukimrekodi na baada usikilize pamoja nae. Hii humjengea kujiamini na
kuona kuwa anachofanya kinathaminiwa.
3. Msaidie pia aweze
kuwa msikilizaji mzuri kwa wewe kumsimulia wakati yeye akikusikiliza ana
kumwambia arudie ulichosema.
4. Mtengenezee tabia
ya kujiamini kwa kuepuka kumfokea au kumpiga mara kwa mara hususani kutokana na
kosa la yeye kuongea sana.
Asante sana mpenzi
msomaji wakati mwingine tutaangalia kipaji cha mtoto ambae kila jambo anataka
kulifanya yeye mwenyewe.
Makala hii imeandikwa na Deo Mukebezi Unaweza
kuwasilina naye kwa 0654627227
Nov 19, 2015
Nguvu Kubwa Ya Mafanikio Inapatikana Kwa Kufanya Jambo Hili Kwanza.
Habari
za siku rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka umzima wa
afya na unaendelea vyema kujifunza ili kuboresha maisha yako. Leo katika makala
yetu napenda kukushirikisha namna unavyoweza kuipata nguvu kubwa ya mafanikio
utakayoweza kuitumia kuweza kutimiza malengo yako makubwa.
Je,
umeshawahi kujiuliza nguvu kubwa ya mafanikio inapatikana wapi? Hili ni swali
muhimu sana kwako kwa sababu kuna wakati katika maisha, kwa sababu ya
changamoto mbalimbali huwa tunajikuta tunakosa nguvu na mwelekeo wa kusonga
mbele na kushindwa kujua tufanye nini? Inapofika hali hii, wengi hukata tamaa
na kusahau kuitumia nguvu kubwa ya mafanikio waliyonayo kuwafanikisha.
Kama hali hii imekukuta huna
haja ya kukata tamaa tena, unaweza kutumia nguvu hii kubwa uliyonayo kukufanikisha. Je, unajajua nguvu hii inapatikanaje
hadi kukufanikisha? Sikiliza, mafanikio yoyote unayoyatafuta yapo Kwenye
Kuanza. Kama kuna jambo unataka kulifanikisha ni lazima ulianze na sio
kulisubiria. Nguvu kubwa ya kuendelea na kusonga mbele inapatikana kwa kuanza.
Unapokuwa unaanza jambo, sio tu unakuwa na nguvu ya kuweza kulifanya bali nguvu
hiyo inakuwa inaongozeka siku hadi siku.
CHUKUA HATUA MARA MOJA ILI KUFANIKIWA. |
Moja
kati ya wanasayansi waliopata kuwepo katika hii dunia, Isack Newton aliwahi
kulieleza hili vizuri katika sheria yake ya mwendo kwamba kitu chochote kikiwa
kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo huo na kitu chochote ambacho kipo
katika hali ya kutulia au utulivu, kitaendelea kutulia siku zote mpaka itokee
nguvu nje ya hapo ya kubadili hali hizo.
Tafsiri
au maana yake ni nini hapa? Ni kwamba kama utaamua kuchukua hatua juu ya maisha
yako, utazidi kupata nguvu ya kukufanikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji.
Chochote unachotaka kukifanya kwenye maisha yako hata kiwe kikubwa vipi, siri
kubwa ya kukifanikisha ipo kwenye kuanza.
Mafanikio
yote makubwa chini ya jua yalianza kwa kufanya kwanza na sio kusubiri. Kumbuka ”DO THE
THINGS YOU WILL HAVE THE POWER TO ACCOMPLISH IT.” Kama kuna jambo
unataka kulifanya, wewe lifanye tu acha kujiandaa sana, wala kusubiri sana kwani nguvu ya
kufanikisha jambo hilo itapatikana wakati unafanya. Kama ni uzoefu mkubwa utaupata kwa kuanza. Hivi ndivyo mafanikio
makubwa yanavyopatikana kwa kuchukua hatua za utekelezaji.
Tumia
kanuni hii bora ikusaidie kufanikiwa kwa viwango vya juu, kumbuka siku zote
unalo jukumu la kuhakikisha unakuwa bora kila siku.
Tunakutakia
mafanikio mema, endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku, TUPO
PAMOJA.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Nov 18, 2015
Kanuni 6 Za Mafanikio, Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.
Wengi
wetu bila shaka umeshawahi kumuona au kumsikia mcheza sinema maarufu duniani kwa
kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Gavana wa jimbo la calfornia, Anord Shwarzenegger. Enzi zake alicheza sinema
nyingi ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana. Leo hii akiwa kama Gavana, Anorld
anatushirikisha baadhi ya kanuni za mafanikio alizozitumia hadi kufikia viwango
vya juu vya mafanikio.
Zifuatazo Ni Kanuni 6 Mafanikio Za
Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.
1. Jiamini wewe mwenyewe.
Watu
wengi mara nyingi hutafuta ushauri wamafanikio kwa watu mbalimbali ili
kuwafanikisha. Ni jambo zuri. Lakini kitu cha cha muhimu hapa kwako ni
kujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Tafuta ni kipi unachokipenda,
unataka kuwa nani na kisha tekeleza kwa kujiamini kabisa, UTAFANIKIWA.
VUNJA SHERIA ZINAZOKUZUIA KUFANIKIWA. |
2. Vunja sheria zinazokuzuia
kufanikiwa.
Tunaishi
katika ulimwengu ambao unasheria nyingi nyingi za uasili zinazoweza kutuzuia
kufanikiwa. Sasa hizi ni sheria ambazo kwa vyovyote vile ni lazima zivunjwe.
Sheria hizi zinaweza zikawa ni uvuvi au mazoea fulani mabaya tuliyojijengea.
Kwa kung’ang’ania sheria hizi hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.
3. Acha kuogopa kushindwa.
Siri
kubwa ya mafanikio ni kujifunza
kutokuogopa kujaribu. Kama kuna fursa imejitokeza jaribu kufanya kwa ujasiri
mkubwa na acha kukaa katika mkao wa kuogopa hiyo haitakusaidia sana. Hautaweza
kufanikiwa kwa kukaa tu. Jitoe mhanga na hakikisha mpaka mipango na malengo
yako makubwa yatimia.
4. Acha kusikiliza maneno ya wanao kukatisha
tamaa.
Yatasemwa
mengi kwamba huwezi kufanya hili wala lile. Wasikilize kisha achana nao. Lililo
kubwa kwako jiamini mwenyewe kuwa utafika kule unakotaka kufika na kisha
endelea mbele. Najua ni mara nyingi umewahi kusikia kauli hizi zikija kwako. Jambo
la kufanya zipuuze kauli hizo, halafu fanya kile unachoamini kitakupa
mafanikio.
5. Fanya kazi kwa bidii sana.
Hiyo
ni nguzo kubwa ya mafanikio yako. Fanya kazi kwa bidii kwa kuamua kujituma na
kulipia gharama zote za mafanikio. Hakuna mafanikio ambayo yatakuja kwako bure
zaidi ya wewe kuwekeza nguvu na uwezo wako wote mkubwa kwenye kufanya kazi kwa
bidii na maarifa makubwa siku zote. Hapa ndipo mafanikio makubwa
yanapopatikana.
6. Kumbuka kutoa.
Mafanikio
yoyote utakayokuwa umeyapata , hakikisha unatoa kwa jamii yako kiasi fulani kama sehemu ya shukrani. Hii ni sheria au
kanuni ya asili ambayo itakusidia kufikia mafanikio makubwa siku zote.
Hizo
ndizo kanuni za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa,
kama zilivyotolewa na Arnold
Shwarzenegger, Gavana wa jimbo la Calfornia marekani.
Nikutakie
siku njema, ansante kwa kupitia makala hii na endelea kuashirikisha wengine kwa
ajili ya kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Nov 17, 2015
Vifungo Ambavyo Jamii Inakufunga.
Leo napenda kusema msemo mmoja, "JARIBU KUJIFUNZA KUTOKA NJE YA PULIZO". Pulizo ni kama vile puto au Bubble kwa kingereza. Ukilitazama
pulizo, hewa ikiwa ndani yake haitoki tena nje. Hivyo kuwa ndani ya pulizo au
puto kunamaanisha kuwa kifungoni. Hivyo kauli hiyo inamaanisha jifunze kutoka
kifungoni katika kutafuta dhumuni lako la maisha.
Kifungoni ni wapi? Je ni kama mahabusu? Hapana, nikisema kifungo ninakuwa ninamaanisha pale ambapo panakunyima uhuru au unapokosa nafasi ya kuwa wewe kama wewe. Pulizo ni kama vile kifungo cha kidunia ambacho kila mmoja wetu anakuwa ndani yake. Mfano kifungo hicho kinaweza kuwa ni:-
·
Wasiwasi wa wakati ujao,
·
Dhana unayoifahamu juu ya
mafanikio katika maisha,
·
Kulazimisha kupendwa na kila
mtu,
·
Kulazimisha kumfurahisha kila
mtu,
·
Kulazimisha kuwa mkamilifu,
·
Maneno ya watu,
·
au Imani ambayo hauna uhuru au
uhakika nayo.
TOKA KWENYE KIFUNGO HIKI. |
Kila mmoja wetu katika jamii ambayo amekulia, kuna mengi ambayo
jamii imemfundisha na kumuambia kuwa ndio jamii inavyopaswa. Mfano
·
Jinsi ya kuishi,
·
Jinsi ya kuvaa,
·
Jinsi ya kula,
·
Kipi cha kula na kipi cha
kutupa,
·
Dini/Imani gani ipo sahihi,
·
Wewe ni nani na kwanini upo
hapa,
·
Miziki, Television na vyombo
vingine vya habari visemavyo,
·
Matangazo yakikuambia kipi cha
kununua au cha muhimu na bora kuliko vingine,
·
Maana ya mafanikio ni nini,
·
Kazi gani ni ya maana kuliko
nyingine na mengi ambayo jamii imeona ni mazuri kwao basi nao hupenda yawe
mazuri kwako.
Ni jambo zuri sana kwani ni jamii inajitahidi kukujali na
kukufundisha kile ambacho inaona ni haki. Lakini je wewe utajuaje kama jamii
ipo sawa? Je kama ni kutokana na kutofahamu kwao ndio kunapelekea mitazamo
hiyo? Ni vyema kuisikiliza jamii inasema nini lakini pia nawe ni vyema
kuutafuta ukweli wewe kama wewe, na ndio maana upo hapa ulimwenguni. Kama
hakuna umuhimu wa wewe kuwepo ni kwanini upo? Lazima kuna sababu ya msingi.
Jamii inatuweka kwenye pulizo, hivyo ni vyema kutoka nje ya pulizo ili kuufahamu ukweli. Ukweli hauwezi kuufahamu kwa kuambiwa tu bali nawe unapaswa uuthibitishe. Je aliyeanzisha ukweli huo aliambiwa na nani? Kwanini na wewe usiutafute? Kwa kuacha kulazimisha mambo unaweza ukajikuta unajifunza mengi sana kuhusiana na maisha kwa ujumla, na ikakusaidia kutafuta dhumuni lako la maisha.
Kama unatafuta dhumuni lako la maisha kwa kutegemea jamii
ikuchagulie dhumuni la kuishi utamaliza maisha yako hujaishi maisha yako bali
unaishi maisha ya wenzako. Ili kuijua safari yako ina malengo gani toka nje ya
pulizo na chunguza ndani mwako unapenda nini na jamii inakuambia nini. Mfano
kuna anayependa kuwa daktari lakini wazazi wanamwambia awe fulani. Sio kwamba
wazazi wamekosea, nao wapo sahihi. Jitahidi uwaelewe kwani kuna wakati mtu
hukuchagulia maamuzi kwa kukulinda na kwa kutumia akili aliyonayo yeye, hivyo
nawe unapaswa kutambua ni kwanini mtu anakupa mtazamo fulani na kisha amua
mtazamo wako kiusahihi na bila kubishana au kumdharau mtu. Heshimu kila mtu na
tambua mchango wa kila mtu katika maisha yako.
Makala
hii imeandikwa wa Apolinary Protas wa JITAMBUE SASA BLOG. Kama una maoni au ushauri
wasiliana na Waandishi wa makala hii kwa email jitambuesasa@gmail.com
Nov 16, 2015
Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
Kwa
kila safari yoyote ya mafanikio duniani ni lazima iwe na changamoto zake.
Hakuna mafanikio ambayo yanakuwa yanakuja moja kwa moja bila kukutana na
changamoto. Mara nyingi changamoto hizi zinapotokea kwa wengine hupelekea
kushindwa kufanikiwa kwa kile kitu ambacho wanakifanya.
Inapotokea
ukashindwa kufanikiwa kwa kile unachokifanya kutokana na changamoto yoyote, ni
nini ambacho huwa unafanya? Hapa ndipo ule umuhimu wa kujifunza kutokana na
makosa huwa unakuja. Najua umewahi kusikia sana juu ya kujifunza kutokana na
makosa pale unapokosea. Lakini je, umeshawahi kujiuliza ni mambo gani
unayotakiwa kujifunza?
Yafuatayo Ni Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa
Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
1.
Mafanikio hayaji mara moja.
Kwa
lugha rahisi naweza nikasema kwamba mafanikio yote yanakuja hatua kwa hatua.
Hakuna mafanikio yanayokuja mara moja. Kwa hiyo kushindwa kwa lile jambo
unalolifanya ni ishara inayo onyesha kwamba ili kufanikiwa ni lazima kujaribu tena
na tena mpaka kufanikiwa, ikiwa lakini umefanya kwa mara ya kwanza na
kushindwa.
Itakuwa
haina maana kwako na utakuwa hupo makini na mafanikio ikiwa utaka tamaa mara
moja baada ya kushindwa. Ukishindwa jambo tambua huo siyo mwisho wako, bali
ndio mwanzo wa mafanikio kwa sababu mafanikio hayaji mara moja. Ukijua hivyo
mafanikio hayaji mara moja hutakaa ukisikitika pale unaposhindwa, zaidi
utaongeza juhudi na uzoefu.
JIFUNZE KITU KUTOKANA NA MAKOSA YAKO. |
2. Kujenga mafanikio inahitaji muda.
Pia
unaposhindwa kufanikiwa katika jambo unalolifanya kwa mara ya kwanza, hiyo
inatuonyesha kwamba mafanikio yanahitaji muda kuyajenga. Mafanikio sio kitu cha
kutokea tu mara moja kama wengi wanavyofikiri. Unatakiwa ujipe muda wa kujaribu
tena na tena mpaka matokeo chanya yatokee.
Watu
wote wenye mafanikio, walitumia muda mwingi kuwekeza kwenye mafanikio yao.
Hakuna mkato juu ya hilo, inabidi ujitume na kuwekeza muda wako vya kutosha ili
ufanikiwe. Kama kuna jambo unalifanya usihisi kama vile unapoteza muda kama
hupati matokeo ya haraka. Kumbuka siku zote kujenga mafanikio inahitaji muda.
3. Siyo rahisi kufanikiwa kama jambo
unalolifanya hulipendi.
Kama
kuna jambo unalifanya halafu ukawa hulipendi sana, elewa ukishindwa huo ndio
utakuwa mwisho wako. Kanuni au sheria za mafanikio zinatufundisha kwamba ili
uweze kufanikiwa ni lazima ulipende lile jambo unalolifanya kwa moyo wote.
Unapofanya
jambo unalolipenda hata unapokosea inakupa nguvu ya kusonga mbele kwa kuweza
kujaribu tena na tena. Hili ni jambo ambalo unatakiwa kulielewa kuwa utajifunza
kutokana na makosa yako kama jambo hilo unalipenda kweli kutoka moyoni. Kinyume
cha hapo haitawezekana kwako.
4. Kushindwa kwako ni ishara ya
kwamba umechukua hatua.
Ni
sawa umeshindwa kwa kile unachokifanya, lakini yote hiyo inakuonyesha kwamba
umechukua hatua. Kama usingechukua hatua ya kufikia mafanikio yako, basi ni
wazi ungebaki kama ulivyo. Kwa kuwa umelijua hilo endelea kuchukua hatua kwa
kusonga mbele. Usihofie kukosea kwako, huo pia ni msingi wa mafanikio yako.
Ansante
kwa kusoma makala hii, kumbuka kushindwa kwa kile unachokifanya ni njia
mojawapo ya kukupeleka kwenye mafanikio ikiwa utajifunza. Usifanye kushindwa
kwako kukakurudisha nyuma.
Ni
kipi unachojifunza wewe pale unaposhindwa kwa mara ya kwanza kwa jambo
unalolifanya? Unaweza ukanishirikisha machache hapo chini kwenye maoni,
tukajifunza kwa pamoja.
Nikutakie
ushindi katika safari yako ya mafanikio, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine
waweze kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika.
Tupo
pamoja katika safari ya kuyafikia mafanikio makubwa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)