Sep 14, 2015
Mambo 4 Unayotakiwa Kuyajua Kuhusu Pesa, Ili Uwe TAJIRI.
Ikiwa
wewe ni mmoja wa watu wanaotaka kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuufikia
utajiri ni muhimu kujua sifa, tabia, kanuni za pesa na hata mambo mengi
yanayohusu pesa. Hilo litakusaidia sana kuweza kuitawala na kutobabaika nayo
pale inapokuwa mfukoni mwako na isitoshe kwa kujua sifa, tabia, kanuni au mambo hayo
itakusaidia wewe hata kuzilinda na kuwa nyingi zaidi.
Bila
shaka umewahi kusikia watu ambao wanapesa nyingi sana leo, lakini baada ya muda
fulani unakuja kusikia tena watu wale hawana hizo pesa katika maisha yao. Kitu kinachotokea
hapo kikubwa ni kutokana na ukosefu wa kutokujua mambo muhimu yanayoihusu hiyo
pesa na siyo kingine. Matokeo yake inakuwa ni upotevu wa pesa nyingi.
Ili
uwe tajiri, mbali na kujua mbinu za kutafuta pesa ambazo tumekuwa tukiziongelea
sana humu ndani, lakini ni lazima kwako pia kujua misingi au mambo muhimu yaliyo katika
pesa hiyo unayoitafuta katika maisha yako. Haya ni mambo ambayo yatakusaidia kukuza
uelewa wako juu ya pesa lakini si hivyo tu yatakusaidia pia kukupa nguvu ya
kuzisaka, kuzitafuta na hata kufikia mafanikio makubwa.
Yafuatayo
Ni Mambo 4 Unayotakiwa Kuyajua Kuhusu Pesa, Ili Uwe TAJIRI.
1. Pesa ni uhuru.
Hakuna
uhuru wa kweli utakoupata kwenye maisha yako kama utakuwa huna pesa. Unapokuwa
na pesa inakufanya uwe huru sana katika maisha yako. Hiyo ni kwa sababu
unapokuwa na pesa itakufanyia mambo mengi ikiwa pamoja na kupata chakula kizuri
unachotaka, utasafiri na hata kupata matibabu vizuri. Kukosa pesa ni utumwa
tena mkubwa ambao unaambatana na manyanyaso. Ni muhimu kulijua hili ili kuongeza
kasi ya kutafuta pesa zaidi na kondokana na utumwa huo.
2. Tumia pesa yako kulingana na
kipato chako.
Haina
maana katika maisha yako kama utakuwa unatumia kiwango kikubwa cha pesa kuliko
kile unachokipata. Kitu ambacho unatakiwa kuhakikisha ni kutumia pesa sawasawa
na kipato chako. Kama yapo matumizi yasiyo ya lazima yaondoe. Kwa kulijua hili
itakupelekea kutunza pesa nyingi ambazo zitakusaidia kuwekeza katika maeneo
mengine.
3. Itumie pesa yako katika uwekezaji.
Kila
pesa unayoipata, fanya kila uwezalo nyingine iweke pembeni kwa ajili ya suala
zima la uwekezaji. Acha kutumia pesa yako yote katika kula tu peke yake. Ikiwa
utatumia pesa yote katika kula na kusahau kuwekuza tambua kabisa
unajitengenezea njia mwenyewe ya kuelekea kwenye umaskini. Hili ni jambo muhimu
pia kulijua kuhusu pesa litakusaidia kuwa makini sana katika matumizi kwa
ujumla.
4. Wekeza pesa yako katika maeneo
tofauti.
Katika
uwekezaji ambao tumetoka kuongelea hapo juu, usiwekeze pesa zako katika eneo
moja tu. Kwa jinsi utakavyozidi kuendelea kukua kifedha wekeza katika maeneo
taofauti tofauti ili kuwa na vitega uchumi vingi vitakavyokuingizia pesa. Ikiwa
utawekeza katika eneo moja ikitokea umekwama basi mambo yote yanakuwa yameishia
hapo.
Kwa
vyovyote vile unahitaji kujifunza mambo mengi yanayohusiana na fedha ili kuweza
kufanikiwa zaidi. Kwa kuanzia nimekupa mambo hayo machache ili kukujengea
misuli ya kusonga mbele.
Nakutakia ushindi katika safari ya mafanikio yako na endelea
kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Imekaa poa hii
ReplyDelete