Nov 23, 2015
Kama Utashindwa Kuyatawala Mambo Haya, Huwezi Kufanikiwa Tena.
Mafanikio siku zote hayaji kama ajali. Mafanikio ni safari ambayo huwa ipo hatua kwa hatua. Mafanikio kwa kawaida hayaji leo ghafla na kusema umefanikiwa, hapana. Mafanikio mara zote yanakuwa na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ili kufanikiwa.
Taratibu
hizo au sheria hizo zinaposhindwa kufuatwa hakuna tena mafanikio yanayoweza
kujitokeza zaidi ya kushindwa. Moja ya taratibu au sheria ambayo ni lazima
uifate na ikupe mafanikio ni ‘sheria ya
kutawala’. Ni lazima yawepo mambo ya kuyatawala kwenye maisha yako ili
ufanikiwe. Bila kuyatawala mambo hayo itakuwa ngumu sana kufikia mafanikio
makubwa.
Wengi
hujikuta wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutaka kujaribu kutawala kila
kitu au kushikiria kila jambo. Kwa maisha kama hayo inakuwa ni ngumu sana
kuweza kufanikiwa. Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa ni lazima umudu kutawala
mambo haya, ukishindwa kufanya hivyo sahau mafanikio.
1. Kutawala pesa.
Huwezi
kupata mafanikio kama matumizi yako ya pesa hayako sawa. Hili ni jambo linalowatesa
wengi na kuwasumbua. Lakini ili ufanikiwe ni lazima kutawala pesa na siyo pesa
ikutawala wewe. Unapokuwa una mudu kuitawala pesa inakusaidia katika mambo
mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza. Unataka maisha yako yote uishi kiumaskini, acha
pesa ikutawale.
TAWALA MUDA WAKO VIZURI. |
2. Kutawala hamasa.
Nguvu
kubwa ya mafanikio unaipata kutokana na wewe kuwa na hamasa kila siku. Hamasa
tunaweza tukasema kama ni mafuta ya kukusaidia kusonga mele. Mara nyingi hamasa
inapokosekana inakuwa siyo rahisi sana kuweza kufanikiwa. Kwani kazi kubwa ya
hamasa ni kukupa nguvu na kichocheo cha kuendelea mbele zaidi ya ulipo.
3. Kutawala kasi ya mafanikio.
Ni
uhimu kutawala kasi yako ya mafanikio yako. Unaweza ukajiuliza kivipi?sikiliza,
kasi ya mafanikio unaitawala kwa kuhakikisha unafanya jambo linalokusogeza
kwenye mafanikio kila siku. Kwa kufanya jambo hilo kila siku hata kama ni
kidogo hapo utakuwa unaendana sawa na kasi ya mafanikio unayoitaka. Ila kama
utashidwa kuitawala kasi hii na kushindwa kufanya jambo hata dogo ni lazima
uachwe.
4. Kutawala tabia njema.
Ili
uwe na mafanikio makubwa ni lazima uwe na tabia njema zinakusogeza kwenye
mafanikio kila siku. Ukiwa na uwezo wa kutawala tabia hizi za kimafanikio uwe
na uhakika ni lazima uweze kufanikiwa. Lakini kama utatawaliwa na mambo hayo
basi tegemea anguko kubwa sana kwenye maisha yako.
5. Kutawala muda.
Muda
ni kitu muhimu sana katika mafanikio yoyote. Pamoja na umuhimu wote huu wa muda,
kwa bahati mbaya sana wengi wanatumia muda vibaya. Kwa tatizo kama hili la kutumia
muda vibaya na kushindwa kutawala muda hupelekea maisha ya wengi kuharibika. Ukitaka
kujua hili vizuri, cheza na muda wako sasa, baada ya miaka kumi utaniambia nini
ambacho kitakutokea kwenye maisha yako.
Haya
ndiyo mambo unayotakiwa kuyatawala ili kufanikiwa kama ikatokea umeshindwa
kutawala jambo mojawapo kati ya hayo basi utakuwa umejiweka kwenye wakati mgumu
wa kuweza kufanikiwa.
Nikutakie
siku njema, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waendelee kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.