Nov 16, 2015
Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
Kwa
kila safari yoyote ya mafanikio duniani ni lazima iwe na changamoto zake.
Hakuna mafanikio ambayo yanakuwa yanakuja moja kwa moja bila kukutana na
changamoto. Mara nyingi changamoto hizi zinapotokea kwa wengine hupelekea
kushindwa kufanikiwa kwa kile kitu ambacho wanakifanya.
Inapotokea
ukashindwa kufanikiwa kwa kile unachokifanya kutokana na changamoto yoyote, ni
nini ambacho huwa unafanya? Hapa ndipo ule umuhimu wa kujifunza kutokana na
makosa huwa unakuja. Najua umewahi kusikia sana juu ya kujifunza kutokana na
makosa pale unapokosea. Lakini je, umeshawahi kujiuliza ni mambo gani
unayotakiwa kujifunza?
Yafuatayo Ni Mambo 4 Ya Kujifunza Pale Unaposhindwa
Kufanikiwa Kwa Kile Unachokifanya.
1.
Mafanikio hayaji mara moja.
Kwa
lugha rahisi naweza nikasema kwamba mafanikio yote yanakuja hatua kwa hatua.
Hakuna mafanikio yanayokuja mara moja. Kwa hiyo kushindwa kwa lile jambo
unalolifanya ni ishara inayo onyesha kwamba ili kufanikiwa ni lazima kujaribu tena
na tena mpaka kufanikiwa, ikiwa lakini umefanya kwa mara ya kwanza na
kushindwa.
Itakuwa
haina maana kwako na utakuwa hupo makini na mafanikio ikiwa utaka tamaa mara
moja baada ya kushindwa. Ukishindwa jambo tambua huo siyo mwisho wako, bali
ndio mwanzo wa mafanikio kwa sababu mafanikio hayaji mara moja. Ukijua hivyo
mafanikio hayaji mara moja hutakaa ukisikitika pale unaposhindwa, zaidi
utaongeza juhudi na uzoefu.
JIFUNZE KITU KUTOKANA NA MAKOSA YAKO. |
2. Kujenga mafanikio inahitaji muda.
Pia
unaposhindwa kufanikiwa katika jambo unalolifanya kwa mara ya kwanza, hiyo
inatuonyesha kwamba mafanikio yanahitaji muda kuyajenga. Mafanikio sio kitu cha
kutokea tu mara moja kama wengi wanavyofikiri. Unatakiwa ujipe muda wa kujaribu
tena na tena mpaka matokeo chanya yatokee.
Watu
wote wenye mafanikio, walitumia muda mwingi kuwekeza kwenye mafanikio yao.
Hakuna mkato juu ya hilo, inabidi ujitume na kuwekeza muda wako vya kutosha ili
ufanikiwe. Kama kuna jambo unalifanya usihisi kama vile unapoteza muda kama
hupati matokeo ya haraka. Kumbuka siku zote kujenga mafanikio inahitaji muda.
3. Siyo rahisi kufanikiwa kama jambo
unalolifanya hulipendi.
Kama
kuna jambo unalifanya halafu ukawa hulipendi sana, elewa ukishindwa huo ndio
utakuwa mwisho wako. Kanuni au sheria za mafanikio zinatufundisha kwamba ili
uweze kufanikiwa ni lazima ulipende lile jambo unalolifanya kwa moyo wote.
Unapofanya
jambo unalolipenda hata unapokosea inakupa nguvu ya kusonga mbele kwa kuweza
kujaribu tena na tena. Hili ni jambo ambalo unatakiwa kulielewa kuwa utajifunza
kutokana na makosa yako kama jambo hilo unalipenda kweli kutoka moyoni. Kinyume
cha hapo haitawezekana kwako.
4. Kushindwa kwako ni ishara ya
kwamba umechukua hatua.
Ni
sawa umeshindwa kwa kile unachokifanya, lakini yote hiyo inakuonyesha kwamba
umechukua hatua. Kama usingechukua hatua ya kufikia mafanikio yako, basi ni
wazi ungebaki kama ulivyo. Kwa kuwa umelijua hilo endelea kuchukua hatua kwa
kusonga mbele. Usihofie kukosea kwako, huo pia ni msingi wa mafanikio yako.
Ansante
kwa kusoma makala hii, kumbuka kushindwa kwa kile unachokifanya ni njia
mojawapo ya kukupeleka kwenye mafanikio ikiwa utajifunza. Usifanye kushindwa
kwako kukakurudisha nyuma.
Ni
kipi unachojifunza wewe pale unaposhindwa kwa mara ya kwanza kwa jambo
unalolifanya? Unaweza ukanishirikisha machache hapo chini kwenye maoni,
tukajifunza kwa pamoja.
Nikutakie
ushindi katika safari yako ya mafanikio, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine
waweze kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika.
Tupo
pamoja katika safari ya kuyafikia mafanikio makubwa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.