Nov 25, 2015
Mambo 5 Yatakayokusaidia Kutokuwa Na Mawazo Mengi Yaliyopitiliza.
Kati
ya tatizo ambalo huwa ni kubwa na linawakabili baadhi yetu bila kujua ni tatizo la kuwa na
mawazo mengi. Wapo watu ambao huwa wanafikiria sana matatizo yao, shida zao au changamoto
zao kiasi kwamba kwa wengine hupelekea kama kuchanganyikiwa. Natambua umeshawahi
kukutana na watu wa namna hii mara kwa mara tu.
Kuna
ambao ulipokutana nao walikuwa ni watu wa kuongea peke yao njiani. Pia kuna
wengine ambao uliwahi kukutana nao wakiwa ni watu wa kujiinamia tu muda wote.
Lakini watu hawa chanzo chao kikubwa ni nini kila ulipowafatilia, hakuna tatizo
lingine, zaidi ya hili la kuwa na mawazo mengi ambayo yapo akili mwao muda
mrefu.
Kitu
kibaya kuliko vyote kwa binadamu ni kwamba, tatizo hili kwa bahati mbaya
linapoanza kwa mtu kuisha kwake huwa sio rahisi sana. Tuchukulie kwa mfano
umekuwa una mawazo mengi ya mara kwa mara yaliyokupelekea ukaanza kuongea
mwenyewe. Tatizo kama hili likisha kuanza, kukuisha litachukua muda mwingi au linaweza lisiishe
kabisa na ukawa ndiyo umechanganyikiwa. kwa hiyo ni lazima kuepuka kutokujiweka katika hali ya kuwa na mawazo mengi hasa kutokana na ukubwa wa athari zake.
Sasa
unawezaje kutoka kwenye tatizo hili la kuwa na mawazo mengi?
1. Ishi sasa.
Wengi
wanapata tabu na kujikuta wakiwa na mawazo sana kutokana na wao kuamua kuishi
jana au kesho. Hapa ili uweze kuondokana na mawazo yanayokutesa unatakiwa
kusahau kila kitu kinachokusumbua kiwe kimetokea jana au kiwe kinakuja kesho.
Kama kuna deni unalotakiwa ulilipe kesho lisahau mara na ishi sasa kesho hiyo ikifika
itaeleweka hapo hapo.
Ruhusu
mawazo yako yafikirie pale ulipo. Acha kujibebesha mizigo mingi ambayo huwezi
kuibeba kwa pamoja. Acha kujibebesha matatizo ya jana na ya kesho halafu yote
ukawa nayo leo. Kwa hilo hutaweza zaidi utazidi kuwa na mawazo kama uliyonayo
sasa. Weka maisha yako yawe huru kwa kuamua kuishi sasa na sio kesho.
2. Jijengee mitazamo chanya.
Siri
nyingine itayokufanya uishi kwa kutokuwa na mawazo mengi sana ambapo wakati
mwingine unahisi hata kuchanganyikiwa ni kwa wewe kujijengea mtazamo chanya.
Fikiria yale mambo yanayokufurahisha na kukupa matumaini. Acha kuweka fikira
zako sana kwenye jambo linalokusumbua, hiyo itakuongezea mawazo zaidi.
Kwa
jinsi utakavyoendelea kufikiria yale mambo yanayokupa furaha, ndivyo ambavyo
utajikuta mawazo mengi ambayo ulikuwa nayo yanazidi kupungua kidogo kidogo.
Kumbuka, unapata kile unachikzingatia. Kama unazingatia furaha basi basi
utapata furaha. Kama unazingatia matatizo halikadhalika utapata hayo hayo
matatizo kwenye maisha yako.
3. Kuwa makini na mawazo yako.
Katika
kipindi ambacho unakuwa na mawazo mengi zaidi, jambo ambalo unatakiwa kuchunga
sana ni mawazo uliyonayo. Ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini na jinsi
unavyoruhusu mawazo yako yaingie akilini mwako. Wengi ukumbuke huwa tunapata
mawazo hasi pengine kutokana na maneno ya watu ambayo huwa tumeambiw. Sasa hayo ni moja ya mambo ambayo tunayotakiwa
kuwa makini nayo sana.
Hata
hivyo, kumbuka mara nyingi jamii tunayoishi ni hasi sana hivyo kuweza kuwa chanya
wakati wote inaweza ikawa ni jambo gumu zaidi. Hivyo kitu cha kufanya ni
kuhakikisha kila mara na kila wakati kama mtu akikuuzi achana naye na usipeleke
hayo mawazo kichwani mwako moja kwa moja. Hiyo itakuwa njia rahisi sana ya
kukufanya usiwe na mawazo mengi akili mwako.
4. Badilisha mazingira.
Inawezekana
ukawa unazidi kuwa na mawazo zaidi kutokana na mazingira uliyopo. Kitu pekee
cha kufanya kwako ni kuhakikisha unabadili mazingira hayo yanayokuplekea uwe na
mawazo hayo. Unaweza ukaenda katika eneo tulivu kama baharini au ziwani kupata
upepo mwanana. Kwa mazingira kama hayo ni lazima mawazo yako yabadilike.
Kwa
hiyo ni lazima uendelee kutokung’ng’ania mazingira ambayo kwako siyo rafiki
yanayokufya uendelee kuwaza mawazo yaleyale kila wakati. Kaa mbali na mazingira
hayo hiyo itakusaidia sana katika hali ya kuweza kuondokana na mawazo hasi
yanakusumbua. Ukitumia mbinu hii itakupa matokeao chanya na ya muda mfupi
kuliko unavyofikiri.
5. Fanya tahajudi(Sala).
Ni
jambo zuri sana pale unapokuwa na mawazo ikiwa utafanya tahajudi au sala. Hiyo
itakusaidia kuyaweka mawazo yako katika hali tulivu zaidi. Unaweza ukafanya hili
kwa kutafuta eneo ambalo ni tulivu na ukawa unafanya sala au tajudi angalau kwa
muda mchache sana kwa siku. Hiyo itakusaidia kujenga kupunguza mawazo mengi
uliyonayo.
Nakutakia
siku njema na endelea kujifunza kila siku ila usikose kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia
matandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.