Apr 24, 2015
Hatua Muhimu Zitakazokuongoza Kufanya Maamuzi Yatakayokupa Mafanikio Makubwa.
Ni kitu ambacho kinawezekana
kabisa katika maisha yako kuwa unaouwezo mkubwa wa kuwa na maisha yenye
mafanikio kama unavyotaka iwe kwako. Ili uweze kufikia mafanikio hayo
unayoyataka kwako ni lazima ujifunze kutumia uwezo mkubwa ulionao kuchunguza
maamuzi unayoyafanya kila siku juu ya maisha yako. Maamuzi unayofanya, ndio
msingi mkuu wa mabadiliko ya maisha yako.
Mara nyingi maamuzi
unayofanya kila siku juu ya maisha yako ndiyo yanayotabiri au kukupa picha kamili
ya maisha yako yanaekea wapi. Kama unafanya maamuzi mabovu kila wakati na kila
mara uwe na uhakika maisha yako ni lazima yatakuwa sio mazuri. Kwa kulijua hilo
ni muhimu sana kwako kuwa makini na maamuzi unayofanya kila siku ili uweze
kuboresha maisha yako zaidi.
Ni kweli kwamba kuna wakati
inaweza ikawa ni ngumu kwako kufanya maamuzi yatakayokupa mafanikio makubwa
katika maisha yako, yote hiyo ni kwa sababu pengine ya kutaka kuona matokeo ya
haraka zaidi. Kama umeamua kuwekeza ni muhimu sana kwako ukawa mvumilivu na
kujipa muda ili kuweza kupata matokeo ya kile unachokitaka. Ukifanya hivyo, ule
ugumu wa maamuzi unaouona hautakuwa shida kwako.
Kwa haraka haraka mpaka hapo
unaona kuwa maamuzi ni kitu cha msingi sana katika maisha yako kuliko
unavyofikiri. Unapokesea kufanya maamuzi
hata kama ni madogo vipi, ndivyo unavyozidi kubomoa maisha yako hata kama
hujui. Hivyo basi, ni muhimu kwako kuwa na maamuzi mazuri na sahihi kila siku
yatakayoweza kubadili maisha yako na kuwa ya mafanikio makubwa.
Unapokuwa na maamuzi haya
sahihi, hii itakusaidia wewe kukuwezesha kustawisha uwezo wako wa kuchagua maisha yanayofaa kila siku.
Katika makala hii ya leo utaweza kujifunza hatua muhimu unazotakiwa kuzichukua
katika maamuzi yako ili kuweza kuishi maisha ya mafanikio. Je, unajua ni hatua
zipi zitakazokuongoza kuchagua kuishi maisha ya mafanikio?
Hizi
Ndizo Hatua Muhimu Zitakazokuongoza Kufanya Maamuzi Yatakayokupa Mafanikio
Makubwa.
1.
Fikiria matokeo ya maamuzi
yako.
Kabla ya kufanya uamuzi wowote
ule katika maisha yako, fikiria kwa makini matokeo ya uamuzi wako huo.
Ukichunguza matokeo ya uamuzi wa unaotaka kuuchukua hiyo itakusaidia kuwa
makini sana na uamuzi wowote unaouchukua kwenye maisha yako. Kwani utakuwa
umejua uamuzi huu unaweza kuboresha ama kubomoa maisha yangu kwa kiasi gani.
Pia kabla hujafanya uamuzi
wowote ule jiulize hivi, uamuzi wangu huu utakuwa na matokeo gani katika maisha
yangu baada ya mwaka mmoja, miaka miwili au hata miaka kumi ijayo. Kama uamuzi
huo unaouchukua utaona unaharibu maisha yako kwa sehemu kubwa, ni bora
ukaachana nao na ukafanya uamuzi tofauti utakao boresha maisha yako.
2.
Chunguza kwa makini maamuzi unayohitaji kufanya.
Ni muhimu sana kuchunguza
maamuzi unayotaka kufanya na sio tu kujifanyia maamuzi ambayo wakati mwingine
hayawezi kukusaidia zaidi ya kukugharimu. Wengi wetu huwa ni watu wa kuiga
maamuzi ya wengine kitu ambacho huweza kuathiri maisha yako moja kwa moja. Ni
muhimu kujichunguza maamuzi unayotaka kuyafanya mara kwa mara.
Kwa mfano kama unataka kuwa
na maisha mazuri ni lazima kwako kujiliza na kujichunguza ni kipi ukifanye ambacho kitaweza kukupa hayo maisha
unayoyatamani. Haitawezekana kwako kufikia maisha hayo kama tu utakuwa bado mtu
wa kuishi maisha yaleyale ya kuendekeza marafiki wa uzembe ama kuendekeza
matumizi ya hovyo. Ukiweza kujichunguza kwanza maamuzi unayoyafanya
yatakusaidia kusonga mbele.
Kwa kumalizia makala hii, tambua
kuwa hizo ndizo hatua muhimu ambazo zinaweza kukuongoza kufanya maamuzi ambayo
yatakupa maisha ya mafanikio kwako na sio tu kujifanyia maamuzi ambayo hayawezi
kukusaidia. Kumbuka kabla hujafanya maamuzi yoyote ni muhimu kufikiria matokeo
ya maamuzi yako na kujichunguza kwa makini maamuzi unayoyataka kufanya
yatakusaidia vipi kuboresha maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri
katika safari yako ya mafanikio na endelea kuwashirikisha wengine kujifunza kupitia
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO ili kuboresha maisha yetu.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE.
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.