google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 22, 2016

Kitu Kinachokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.

No comments :
Bila shaka umewahi kuwaona watu ambao katika maisha yao siku zote ni watu wasio na pesa na ni watu ambao wanaishi maisha ya kutotimiza  malengo yao siku hadi siku. Umeshawi kujiuliza watu hawa tatizo kubwa walilonalo nini linaowafanya waishi maisha hayo siku zote?Ni kitu ambacho pengine kimekuwa kikikushangaza.

Ukija kuangalia ama ukichunguza kwa makini utagundua kuwa watu hawa, ambao  inaweza ikawa ni wewe pia, wamekuwa wakiishi maisha ya kutokutimiza malengo yao  sio kwa sababu hawana pesa ama muda wa kutimiza malengo yao. Kitu kikubwa kinachowafanya wasitimize malengo ni kukosa nguvu ya uzingativu katika malengo yao.

Hiki ndicho kitu muhimu wamekiwa wakikikosa katika maisha yao na kimewafanya waishi maisha magumu yasiyo na pesa. Kwa kawaida, unapokosa nguvu ya uzingativu na kushindwa kutilia mkazo kwa kujikumbushia malengo yako mara kwa mara kinachotokea kwako ni lazima ushindwe kufikia malengo yako.


Watu wengi wenye mafanikio makubwa wanajua ukweli huu na wanaufanyia kazi kila siku kwa kujikumbushia malengo yao mpaka yanatimia. Kama unafikiri natania nenda kamuulize Thomas Edson na ugunduzi wake wa glopu/balbu alikosea mara 9999 bila kuchoka hadi akaja kugundua kitu ambacho kina manufaa kwetu mpaka leo.


Kama Thomas Edson angekata tamaa na kushindwa kuweka nguvu za kutosha za uzingativu kwenye malengo yake aliyojiwekea basi pengine leo hii dunia yote ingekuwa inalala giza. Kunapokuwa na nguvu ya uzingativu na kuielekeza akili yako yote kwa kile unachokifanya huwa kuna matokeo makubwa ya kimafanikio.

Nakumbuka nikiwa darasa la sita, katika somo la sayansi mwalimu wangu mmoja alikuwa akitufundisha namna ya kutumia kioo ambacho kilikuwa kipo katika mfumo wa lensi kuweza kuchoma vitu kama karatasi. Alikuwa akichukua kioo kile na kukielekeza kwenye karatasi ambapo baada ya muda kwa kukiweka kioo sehemu moja kilikuwa kinakusanya mwanga wa jua na kuweza kuchoma karatasi.

Mwalimu Yule aliweza kutufafanulia  kuwa mwanga wa jua una nguvu sana lakini kama umesambaa hauwezi kuleta madhara yoyote, mpaka ukusanywe pamoja na kitu kama lensi ya kioo ndio unaweza ukaleta madhara na kuchoma vitu kama karatasi. Kwa kupitia mfano huo hivyo ndivyo tulivyo katika maisha yetu.


Mara nyingi binadamu tunazonguvu nyingi sana na kubwa ambazo tunauwezo wa kuzitumia na kutuletea mabadiliko makubwa katika maisha yetu kama tutaziwekea nguvu ya uzingativu. Yale mambo ambayo umekuwa ukishindwa mara kwa mara ukijakuangalia unashindwa sio kwa sababu huwezi ila ni kwa sababu unakosa nguvu hii muhimu kwako.

Kama unataka kufanikisha malengo yako na kuona ndoto zako zikiwa zinatimia ni jukumu lako wewe kuweza kujifunza kutumia nguvu hii vizuri ya uzingativu ili ikuletee matokea chanya unayohitaji. Hata kama umeshindwa mara ngapi kwa kile unachokifanya acha kupoteza mwelekeo kwa kukosa nguvu hii muhimu kwako na mafanikio yako.

Kitu pekee kinachowafanya watu wengi wawe waoga, wawe watu wa kuahirisha mambo, wakose uvumilivu na nidhamu binafsi  ni kutokana na kukosa nguvu hii ambayo wakiwa nayo itawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea. Unapokosa uzingativu wa kulenga kile unachokitaka kiwe katika maisha yako, inakuwa ni ngumu sana kufikia malengo yako.

Ili uweze kutimiza malengo yako unahitaji kuwa na nguvu ya uzingativu hasa kwenye malengo yako iliyojiwekea kila wakati. Kuwa na mafanikio siyo suala la bahati kama wengi wanavyofikiri ni kitu cha kupanga na kuamua kisha kuweka nguvu zako zote huko, uwe na uhakika malengo yako hapo yatatimia.

Nakutakia mafanikio mema, endelea kutemblea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza na kuhamasika, mpaka maisha yako yaimarike.

IMANI NGWANGWALU,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.