Dec 8, 2018
Jambo Hili Lisiwe Kizuizi Cha Mafanikio Yako...Kila Mtu Anapitia.
Haijalishi
unafanya kitu gani na una uhakika gani wa kukamilisha kitu hicho, lakini huwezi
kukipata kitu hicho moja kwa moja kwa jinsi unavyotaka wewe iwe. Yapo mambo
ambayo ni lazima yataingilia malengo yako hayo kwa namna moja au nyingine.
Unapojiwekea
malengo, utafika wakati malengo yako yataingiliwa tu. Itafika wakati pesa
ambayo ulikuwa umeitenga kwa ajili ya malengo fulani, unaweza ukashangaa
umeitumia kwa dharura na kujikuta tena unaanza upya.
Lakini
pia unaweza ukawa umeamua kufanya kazi fulani inayohitaji utulivu, lakini
ukashangaa simu ikaita, au ukapokea dharura ya kuitwa pengine na bosi wako na
miingiliano mingi kama hiyo ambayo naweza kusema haikwepiki kirahisi.
Yanapotokea
mambo kama haya ambayo yanaingilia ndoto na malengo yako isifike mahali
ukajikuta unakata tamaa. Unachotakiwa kuelewa ni kwamba, mwingiliano wa vitu
katika malengo, ni kitu ambacho kinamtokea kila mtu na kwa wakati wake.
Mwingiliano wa mambo ukizidi, ni sumu ya mafanikio yako. |
Kama
ikitokea umepoteza mwelekeo na huoni tena dalili ya kufanikiwa kutokana na
mambo mengi kuingilia ndoto zako, usikate tamaa, unatakiwa kurudi haraka sana na
kuendelea kuifatilia ndoto yako.
Usipoteze
muda wako kulalamika au kulaumu hali ambayo imekupata, badala yake tumia muda
huo, kutafuta njia ambayo itakufanya uirudie ndoto yako haraka sana na sio
kuipotezea kama ambavyo unataka kufanya.
Ni kawaida
sana kwa mambo ambayo yanaonekana kwa macho ya kawaida hayawezekani, kuingiliwa
na vitu ambavyo hukutarajia. Lakini ukikata tamaa na kusema ndio basi, uwe na
uhakika utaipoteza ndoto yako.
Weka
mkazo katika akili yako wa kusahau karibu kila kitu nakuamini, unaweza kuirudia
ndoto yako hadi kuifanikisha, hata kama hapa kumetokea mwingiliano mkubwa sana
ambao kwa uwazi umeonekana kukuvuruga na kukuchanganya kabisa.
Kuingiliana
mambo ambayo hukutegemea kunapokuja kama huelewi vizuri, unaweza ukaacha kila
kitu, lakini nikwambie hivi tu, kitu hiki kidogo kisiwe kizuizi kwako cha
kukuzuia kufanikiwa hata kidogo.
Maisha
ya mafanikio makubwa bado yanakuja kwenye maisha yako, changamoto ndogo kama
hizi kwako kutokea, anza kuzichukulia kama fundisho la kukukomaza na kukupeleka
kwenye mafanikio makubwa. Jipe moyo na
inawezekana.
Tunakutakia
kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa.
Daima
tupo pamoja mpaka maisha yako yaimarike na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku maisha na mafanikio.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.