Dec 1, 2018
Kitu Kimoja Ambacho Unatakiwa Kukijua Kuhusu Mafanikio.
Kila mtu anataka kufanikiwa. Kila mtu ana kiu, hamasa na nia kubwa ya kuona anafanikiwa kwenye maisha yake. Japokuwa, pamoja na kiu hiyo kipo kitu kimoja ambacho unalazimika ukijue ili uweze kufikia mafanikio hayo.
Kama
hutaweza kukijua kitu hicho na huku ukitafuta mafanikio yako, kitakachotokea
kwako ni kwamba utakuwa unapata tabu sana kwenye safari ya mafanikio. Kwa lugha
rahisi kuna wakati utakuwa huelewi elewi jinsi mambo yanavyokwenda.
Najua
safari ya mafanikio ina anza na watu wengi sana, lakini kwa bahati mbaya wengi
wanakuwa ni watu wa kuishia njiani. Unajua ni kwa nini, ni kwa sababu ya wengi kushindwa
kukujia kitu hicho muhimu katika mafanikio.
Kitu
hicho ambacho wewe unalazimika sana kukijua kwenye safari yako ya mafanikio ni
kwamba mafanikio yanatumia muda mrefu sana kuyafikia. Hiki ndicho kitu unatakiwa
ukiweke kwenye akili yako na kutambua mafanikio hayafikiwi siku moja,
yanahitaji muda ili uweze kuyafikia.
Kuna
kipindi, wakati naanza kuandika kwenye blog hii nilikuwa nashangaa sana kwa
nini inachukua muda mrefu kwa blog hii kuwa na wasomaji wengi. Kwa sababu hii
niliamua kujifunza muda halisi wa mafanikio kwa watu waliofanikiwa hasa ni upi.
Nilichokuja
kugundua ni kwamba mafanikio yanatumia muda mrefu na si mfupi kama unavyofikiri
ili kuweza kuyafikia. Kwa chochote kile unachokifanya, inatakiwa utenge muda wa
kutosha ili mpaka kuanza kuona matunda yake.
Kwa
mfano, ilichukua muda wa miaka 11 hadi program ya ‘Microsoft’ ya bilionea mkubwa duniani kuanza kufanya kazi na kuleta
mafanikio makubwa. Mafanikio yake hayakutokea tu ghafla kuna miaka ilikataika
hapa katikati.
Pia
ilimchukua miaka 29 kwa Abraham Lincoln hadi kuweza kuwa Rais wa marekani. Ipo
mifano mingi inayoonyesha kwamba mafanikio si kitu cha mara moja tu, unatakiwa
kuwekeza muda ili uweze kufanikiwa kwenye mafanikio hayo uyatakayo.
Kama
utakuwa ni mtu wa kutaka mafanikio na halafu ukategemea mafanikio hayo
yakatokea ghafla ghafla kwa muda mchache ni rahisi sana kwako kuweza kukata tamaa
na kuona ni kitu ambacho hakiwezekani au mafanikio ni ya watu wa aina fulani tu
lakini si wewe.
Kwenye
akili yako sasa weka wazi, mafanikio ni safari ya muda mrefu. Unatakiwa kabisa
utenge miaka angalau kuanzia 5 hadi 15 ya kutafafuta mafanikio yako ya kweli na ya kudumu. Ukikurupuka na kutaka
mafanikio ya chapu chapu utakwama.
Watu
wengi wanakata tamaa kwenye safari ya mafanikio kwa sababu ya kutokujua kwamba
mafanikioo yanataka muda mrefu. Katika kipindi cha kutafuta mafanikio yako
unatakiwa ujitoe hasa, kuvumilia na kutoa kila ulichonacho hadi ufanikiwe.
Nimekundikia
makala haya si kukatisha tamaa bali kukupa ukweli na uhalisia ulivyo. Kama una
bisha chunguza mwenyewe kwa watu waliofanikiwa, utagundua wametumia muda mrefu
ili kuweza kufanikiwa kwao kwa uhakika.
Kwa
kifupi, hakuna mafanikio ya ghafla, hakuna mafanikio ya chapu chapu, unatakiwa
kutumia muda na nguvu kujenga mafanikio yako pasipo kukata tamaa, kila siku
unatakiwa ujitume kwa kutenga miaka 5 hadi 15 ya mafanikio yako.
Unatakiwa
kujua hakuna ambaye atashindwa kama ataamua kufanya kazi kwa bidiii na pasipo
kukata tamaa. Kwa mtu wa namna hii ushindi upo mbele yake na unamsubiri kwa
hamu kubwa na wewe unaweza kuamua ikawa hivyo kwako.
Kitu
cha msingi hapa ambacho unatakiwa kuelewa kwenye makala haya ni kwamba,
mafanikio yanatumia muda mrefu kuweza kuyafikia. Hiki ndicho kitu unatakiwa
ukiweke akilini mwako wakati unatafuta mafanikio. Ukijua hili mapema hutakata
tamaa na kikubwa kwako endelea kupambana
na utafanikiwa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.