Dec 2, 2018
Aina Ya Watu Wanaoendelea Haraka Kwenye Maisha Yao.
Kwenye maisha wapo watu ambao ukiwaangalia kwa haraka wanaonekana ni kama hawaendelei upesi yaani zile hatua za mafanikio kwao zinaonekana zinachelewa kabisa, na wapo watu ambao wanaonekana wanafanikiwa upesi sana.
Hili
nafikiri umeshawahi kuliona, na kuna wakati labda ulijiuliza hawa wanaoendelea
sana ni watu wa namna gani. Pia ukaendelea kujiuliza kwa nini wao waendelee
upesi na wengine wasiendelee upesi? Je, kuna bahati au nini sababu?
Katika
makala haya leo tutajifunza aina ya watu ambao wanaendelea sana. Watu hawa ni
wa aina gani, karibu tujifunze.
1. Watu wenye mapenzi na kile
wanachokifanya.
Watu
hawa wenye mapenzi na kile wanachokifanya, ama ‘passionate people’ huwa ni watu wanaofanikiwa. Kwa nini kwao
kufanikiwa kunakuwa nje nje ni kwa sababu watu hawa watafanya kila linawezekana
hadi kuona wanafanikiwa.
Itafika
mahali watu hawa watakosea, lakini kwa sababu wana mapenzi na kitu hicho
watakifanya na hadi kuona wanafanikiwa tena kwa kiasi kikubwa kwenye maisha
yao. Jaribu kuwatafuta watu wa namna
hii, utagundua wanaendelea kwa haraka sana.
2. Watu wenye nidhamu ya hali ya juu.
Pia
kundi lingine la watu ambao wanaendelea kwa haraka ni hili la watu wenye nidhamu
kubwa. Nidhamu inawafanya watu hawa wajitume kufanya kile wanachotakiwa
kukifanya hata bila kujali kama wana hamasa au hawana hamasa.
Wakati
watu wengine wana subiri wapate hamasa ndio wafanye kitu, watu hawa wanajituma
tu, pasipo kujali hamasa hiyo. Kwa kifupi ni watu wanaofanya pasipo kujali
wanajisikia au hawajisikii ila wao wanafanya, kwa sababu hiyo wanaendelea sana
upesi.
3. Watu wanaojitoa mhanga.
Inasemekana
pia watu wanaojitoa mhanga juu ya maisha yao,
‘risk taker’ pia ni watu wanaoendelea sana. Watu hawa kwanza hawaogopi
kuchukua hatua yoyote, pia hata wakishindwa wanarudi upya tena upesi sana.
Mafanikio
yoyote yanawafata watu wa namna hii bila kipingamizi. Mafanikio hayawezi
kukwepeka ikiwa unajitoa kweli hata kwenye mazingira ambayo yanaonekana ni
hatarishi kwa wengi. Kujitoa huko ndiko kunakowafanikisha sana watu hawa.
4. Watu wanaozingatia jambo moja.
Wale
watu ambao mawazo yao wanaweka kwenye jambo moja na kulifanya kwa usahihi, watu
hao wanafanikiwa moja kwa moja. Watu hawa mara nyingi hawataki kuzigawanya
nguvu zao zikawa katika maeneo makubwa mawili.
Kwa
sababu hiyo ya kuweka nguvu zao katika eneo moja hujikuta wakifanikisha mambo
yao na kuendelea kwa upesi. Hawa ni watu ambao nasema wanazingatia sana PLAN A
ya maisha yao kuliko ile PLAN B. Wanaamini mafanikio yao yapo kwenye ule mpango
wa kwanza, hivyo kwa hili hufanikwa.
5. Watu wanaojua kuishi na watu vizuri.
Uzuri
wa watu hawa, kwa sababu wanajua kuishi na watu vizuri, hilo linawasaidia
kufanya biashara kwa ushirikiano mkubwa, hiyo haitoshi inawasaidia pia kuweza
kuwajua wateja kwa wengi kila siku zinavyokwenda.
Unatakiwa
kuelewa hivi kwenye maisha hatufanikiwi tukiwa sisi kama sisi, ni lazima tuwe
na ushirikino na watu. Kwa kuwa na ushirikiano huo inasaidia sana kuweza kukuza
mahusiano yetu kibiashara na hatimaye na sisi kuweza kufanikiwa kwa haraka.
Hizi
ndizo aina za watu ambao kwenye maisha huwa ni watu wa mafanikio au kuendelea
sana. Kama unataka kuwa miongoni mwao unaweza ukavuta tabia mojawapo hapo na wewe
ukawa ni miongoni mwa watu wenye mafanikio ya kasi katika sayari hii.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.