Dec 3, 2018
Marafiki Ambao Hutakiwi Kuwa Nao Kama Unataka Kufika Mbali Kimafanikio.
Upo mchango mkubwa sana wa marafiki katika kutufikisha kwenye mafanikio. Lakini hata hivyo ieleweke hivi si kila rafiki ni rafiki mwema katika kutusaidia kutufikisha kwenye mafanikio yetu. Wapo marafiki ambao hawafai kuambatana nasi hata kidogo kama tunataka kufanikiwa na kuweza kufika mbali kabisa kimafanikio.
Hapa
kati makala haya nataka nikuonyeshe rafiki
ambao hutakiwi kuambatana nao katika safari yako ya kimafanikio. Kama utaamua
kuambatana na marafiki hawa ujue kabisa utakuwa unafanya kazi ya ‘makitaimu’ yaani utakuwa huendi mbali
sana kimafanikio. Twende sasa pamoja kujifunza aina hii ya marafiki unaotakiwa
kuwaepuka.
1. Marafiki wakosoaji.
Aina
hii ya marafiki watakakukosoa kila kitu unachokifanya au kile ulichonacho. Watakosoa
kwamba ukifanyacho hakifai. Watakosoa utendaji wako wa kazi na hata pia wanaweza
kukosoa aina ya maisha unayoishi.
Kuwa
na marafiki wa namna hii ambao ni wakosoaji ni sawa na kujitafutia majanga. Hawa
ni marafiki ambao unatakiwa uwakwepe sana. Kuendelea kukaa na marafiki hawa
huko ni kujipotezea muda wako wewe, kwani hawatakusaidia kufanikiwa.
2. Marafiki wasio na malengo ya
kimaisha.
Hawa
pia ni aina ya marafiki wabaya sana kwenye maisha yako. Unapokuwa na marafiki
wa aina hii unatakiwa kuelewa kwamba upo uwezekano mkubwa hata wewe ukaanza
kuishi mfumo wa maisha yao yaani ukaishi bila malengo yoyote.
Marafiki
hawa kwa sababu hawana malengo, basi hata muda wao wanautumia hovyo sana. Muda ambao
ungetumika kufanya vitu vya msingi wao wanaoupoteza, ukifatilia sababu hasa,
utagundua hawana malengo maishani mwao.
3. Marafiki watumiaji.
Hii ni
aina ya marafiki ambao muda wao mwingi sana wanawaza juu ya kutumia. Marafiki hawa
hawako tayari kuweka pesa kwa ajili ya kuwekeza bali ni kuzitumia. Kila ikifika
ijumaa wao ni sherehe kwa kujirusha huku na kule.
Epuka
sana marafiki hawa kwani watakufanya wewe ushindwe kuwekeza pesa zako kwa ajili
ya kesho. Pia marafiki hawa watakufanya utumie sana pesa zako hovyo bila
mpangilio. Kama ukiweza kuwaepuka marafiki hawa basi utajenga mwelekeo wa
kufanikiwa.
4. Marafiki wanaopenda ushindani usio na
maana.
Hawa
ni marafiki ambao kila kitu ukifanya wanataka kushindana na wewe. Kwa mfano, ukinunua
kitu hiki na wao wanataka kununua. Ukiwekeza kwenye mradi huu na wao wanataka
kuwekeza. Kama unataka kufika mbali kimafanikio, hawa ni marafiki ambao pia
hawakufai kabisa
Kuendelea
kuwa na marafiki hawa, inabidi utambue wanakupotezea sana nguvu zako nyingi
ambazo ungezitumia kuweza kufanikiwa. Kwa kifupi hawa ni marafiki wasumbufu
kwako na hawakufai katika kukufikisha kwenye ndoto zako.
Kwa kuhitimisha
makala haya, hizi ndizo aina za marafiki unaotakiwa kuwaepuka sana katika
maisha yako. Ni jukumu lako sasa kuchagua marafiki waliobora kwako na kuachana
na marafiki watakaokurudisha nyuma kimafanikio.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.