Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, August 8, 2015

Kama Unataka Kufanikiwa Zingatia Sana Kitu Hiki.

No comments :
Funga macho, vuta picha ya magari mawili yanatembea. Dereva mmoja anajua kuwa anatoka kijiji A na kwenda kijiji B, halafu dereva wa pili wala hajui anakokwenda. Kati ya madereva hao wawili, yupi atafika anakokwenda?
Bila shaka jibu litakuwa ni dereva A. Kinachowatofautisha ni malengo, dereva wa gari la kwanza anajua kuwa lengo lake ni kufika kijiji B, hapo atatafuta hata njia ya mkato afike, hata kama hajui njia anaweza akauliza watu akaelekezwa. Dereva wa pili hata kama kuna barabara mbele yake anaweza akafika anakotakiwa kwenda, akapapita au akageuza maana hajui anakokwenda.
Hata kwenye maisha yetu hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya watu wenye malengo na wale wasiokuwa nayo. Wenye malengo huwa wanafanikiwa zaidi ya wale wasiokuwa nayo, yaani wanakwenda tu kama dereva wa pili!
Lengo?
Kuwa na malengo ni moja ya chachu kubwa ya mafanikio katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha. Malengo yanakupa dira kubwa ya mafanikio maishani mwako na kukuelekeza usiende mrama kwa kukosa mwelekeo na kama unataka kufanikiwa ni muhimu sana kuzingatia malengo yako.
Malengo yanaweza kuwa vitu vidogo tunavyotaka kubadili leo, pia yanaweza kuwa mambo makubwa tunayotaka kuyafanikisha siku zijazo, iwe baada ya mwezi, mwaka, au hata baada ya miaka mitano! Unaweza ukawa na malengo ya aina mbalimbali; ya kiafya, kikazi, kimasomo, kiuhusiano au kibiashara; muhimu ni kuwa na malengo.
Jiwekee malengo yako leo!
1. Fahamu unachokitaka.
Ninachomaanisha hapa ni kujua nini unakitaka, ukijua unachokitaka utakuwa na msimamo wa kutaka kufikia malengo yako. Mwanafalsafa Lawrence J. Peter aliwahi kusema, ‘’If you don’t know where you are going, you will probably end up somewhere else.’’ Akimaanisha ... “Kama hujui unakokwenda inawezekana ukaishia sehemu nyingine tofauti kabisa.” Bado hujajua unachokitaka? Chukua kalamu na karatasi, kaa mkao wa kuandika! Jiulize, unataka kufanikiwa katika kitu gani? Hapa ni muhimu kuwaza ki- chanya chanya, usianze kudhani kwamba utafeli kabla hata haujajaribu. Jiamini. Kwenye karatasi yako sasa, orodhesha mambo yote unayotaka kufanikiwa, iweke mahali ambako utaiona mara kwa mara, wengine hutundika ukutani. Sasa anza kupanga mipango kwa kujiwekea malengo na kutekeleza moja baada ya jingine. Si lazima uanze na uliloandika kwanza.
2. Tambua nini kinakupa hamasa ya kutaka kufanikiwa.
Motisha ni chachu ya ustahimilivu kwani hukufanya kuendelea kushikamana na mipango yako mpaka mwisho licha ya kuwa na vipingamizi vingi katika njia yako ya mafanikio. Malengo mengine ni ya muda mrefu hivyo yanakuhitaji uwe mvumilivu ili ufanikiwe, kama utakosa ustahimilivu unaweza kujikuta unakata tamaa mapema kabla ya kufi kia malengo. Motisha ni kitu pekee kinachokusaidia kukusukuma uendelee kutaka kufanikiwa hivyo ni heri kila malengo unayojiwekea yawe ni yenye kukupa kiu ya kutaka kufanikiwa kwa kuwa unapenda hayo unayoyahangaikia.
3. Jijengee nidhamu ya ufuatiliaji mpaka mwisho.
Ndiyo. Wapo wenye tabia ya kushika hiki na kuacha, kisha kuanza kingine na kingine vyote vinaishia njiani. Kuwa na nidhamu, fika mwisho.
4. Tathmini hatua utakazopitia.
Licha ya kutambua nini unataka, ni jambo la msingi kujua pia utasonga mbele. Wanasema safari ni hatua; Unaanzaje? Kuna vikwazo gani na utakabiliana navyo vipi? Inakufundisha nini? Pata picha halisi ya nini utafanya na wapi.
5. Amini inawezekana.
Safari ya mafanikio siyo rahisi kama watu wengi wanavyofi kiria, kila aliyefanikiwa ana hadithi yake ya kusimulia juu ya changamoto alizokumbana nazo katika jitihada za kutafuta mafanikio. Kama hutokuwa na imani thabiti ya kile unachofanya ni vigumu kuwa na matumaini ya kufi kia mafanikio. Hofu na shaka vinaweza kukurudisha nyuma, usikubali, lakini usidharau, jipange.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
No comments :

Post a Comment