Sep 8, 2015
Jinsi Ya kuweka Vipaumbele Katika Malengo Hadi Kuyafikia.
Kila
mtu ili kuweza kufikia mafanikio ni muhimu kwake kujiwekea malengo. Malengo
haya anayojiwekea huwa ni lazima kuyatimiza. Inapofika mahali ukawa ni mtu wa kushindwa
kutimiza malengo yako mara kwa mara, hiyo inakuwa ni hatari na shida kwako kuelekea kwenye
safari ya mafanikio. Jaribu kujiuliza pale unapokuwa hutimizi malengo yako huwa
unajisikiaje? Bila shaka ni vibaya.
Lakini
hata hivyo pamoja na kujiwekea malengo hayo kuna wakati huwa tunajikuta
tunakuwa tunamalengo mengi ambayo huanza kutuchanganya na kushindwa kujua
tufanye lipi kwanza na tuache lipi. Kwa mfano, katika hali ya kawaida unaweza
ukajikuta una malengo mengi zaidi ambayo umepanga na unatakiwa kuyatekeleza,
hapo unafanyaje?
Kwa
kawaida malengo yanapokuwa mengi unakuwa huna uwezo wa kuyatekeleza yote kwa
pamoja hata ungefanyaje? Hii yote huwa inatokea hivyo kwa sababu, kila lengo
linakuwa linachukua muda na nguvu kulitekeleza hadi kufanikiwa. Hivyo malengo
yanapokuwa mengi inakuwa siyo rahisi kufanikiwa kutokana na sababu hiyo.
Na
hata kama ikatokea umejaribu kufanya malengo mengi kwa wakati mmoja basi
utafanya kwa uhafifu badala ungefanya malengo machache na kwa ubora wa hali juu
kabisa. Utafanya vizuri kwenye malengo ikiwa utajitoa kwenye malengo machache(
Pengine moja) yaliyofafanuliwa na kupangwa vyema kabisa.
Kwa
mfano, unaweza ukajikuta una malengo ya kutimiza kumi katika kipindi cha muda
fulani. Hapo kwanza, katika hali ya kawaida huwezi kutimiza malengo yote kumi
kwa wakati mmoja, ila unachotakiwa kufanya ili malengo yako hayo yatimie ni
kuweka kipaumbele tena kwa haraka sana.
Pengine
unajiuliza, nitawekaje kipaumbele? Nitakueleza unachotakiwa kufanya. Unachotakiwa kufanya ni kujiuliza swali hili
‘ Kama nitaacha kila kitu isipokuwa kimoja
katika malengo yangu niliyonayo, ni kitu gani kimoja ambacho ningeanza kukitekeleza?’
Utakapojibu swali hilo hicho ndicho kipaumbele mbele chako cha kwanza
unachotakiwa kukitekeleza bila kuacha.
Kwa
lugha nyingine hapo katika uwekaji wa vipaumbele chagua kile kilicho cha muhimu
kuliko vingine vyote anza kukitekeleza. Kitu hicho kikishakamilika nenda
kingine tena. Kwa kufanya hivyo utajikuta malengo yako yanatimia moja baada ya
jingine na mwisho wa siku utajikuta malengo yote yametimia. Acha kubabaika na
uzuri wa malengo mengine, ukishaweka kipaumbele, fata lengo moja tu, mpaka
litimie.
Acha
kujifanya kutekeleza malengo yote kwa wakati mmoja hutaweza na itafika mahali
lazima utakwama tu. Nguvu yako kubwa ya kukufanikisha hasa pale unapokuwa na
malengo mengi ni kufanya lengo moja moja kwanza. Hiyo ndiyo siri ya ushindi
ilioyopo katika uwekaji wa vipaumbele.
Hivyo,
watu ambao wataweza kuyapa vipaumbele malengo yao. Katika maana halisi na
mtiririko mzuri ni wazi kuwa lazima watafanikiwa. Chukua hatua hii ya kuweka
vipaumbele katika malengo yako ili ufanikishe, kufaulu na kusonga mbele kwa
ujasiri. Tegemea mafanikio makubwa kama utatekeleza hili.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari ya mafanikio, endelea kuwashirikisha wengine
kutembelea mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku kwa kujifunza na
kuhamasika zaidi.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Mawazo mazuri sana tukizingatia tufafikia ndoto au shabaha zetu. ipo poa sana
ReplyDelete