Feb 11, 2016
Acha Kuupuza Kutumia Mlango Huu Kukufanikisha.
Kwa
muda mrefu imekuwa ikiaminika kwamba binadamu ana milango mitano ya fahamu.
Yaani kuona, kugusa, kuonja, kusikia na kunusa. Hata hivyo, ukweli umebainika
kuwa, binadamu ana zaidi ya hiyo milango mitano. Imebainika kuwa, sasa binadamu
ana milango sita ya fahamu.
Hii
ni moja ya tafiti muhimu kubwa ambazo zimedi kufanywa na wataalamu siku za hivi
karibuni. Watafiti hawa wanasema na ili binadamu huyu aweze kutimiza kusudio la
uhai wake hapa duniani, sharti autumie mlango huu wa sita wa fahamu ambao kwa
muda mwingi umesahaulika ama kupuuzwa na hivyo kushindwa kutumika ipasavyo.
Mlango
huu wa sita wa fahamu ni ule unaohusu nafsi ya binadamu. Kwa maana kwamba, huu
ni mlango unaohusiana na haja au tamaa ya asili ya binadamu katika mambo ya
kiroho. Mahitaji haya ya kiroho ambayo ni ya asili kwa binadamu huambatana na
nafsi yake na kujiimarisha zaidi kwenye moyo wake. Ninaposema ‘moyo’, nina maana ya akili na hisia.
Kama
ilivyo kwa milango ile mitano ya fahamu ambayo huwasiliana na kuongoza mwili,
ndiyo ilivyo pia kwa hisia hizi za kiroho ambazo kazi yake kuu ni kuilinda na
kuunganisha nafsi hiyo na muumba wake (Mungu), kuipa nafsi muongozo wa kiroho
wa kiroho na kuunganishwa na nguvu ambazo hutuongoza katika njia zetu na
makusudio yetu.
UBUNIFU NI MUHIMU |
Ile
milango mitano ya fahamu hutufanya tuweze kuendelea kuishi juu ya ardhi ya
dunia. Lakini mlango huu wa sita au mtikisiko wa ndani kabisa wa kihisia
hutupatia mabawa na kutufundisha namna ya kuruka. Hapa ni kwa maana kwamba,
hutuongezea uwezo na nguvu za kutimiza ndoto zetu. Ni watu wachache sana
wanaotambua ukweli huo na wanaojua kuutumia mlango huo.
Kutokana
na jinsi dunia yetu hii inavyozidi kusonga mbele, suala la kuutumia mlango huu
halitakuwa suala la hiari tena, bali litakuwa ni suala la lazima kwa mtu yeyote yule anayetaka
kuishi maisha yenye kusudi, salama na usawaziko. Hatupaswi kamwe kuukana uwezo
wetu ambao hutupatia hekima na maarifa ya hali ya juu na kuendelea kukumbatia
nadharia za kisayansi peke yake.
Ukweli
ni kwamba, tuna uwezo mkubwa usiothimilika ndani ya nafsi zetu kuliko vile
tunavyoelewa au kwa vile tulivyofundishwa kuamini. Ni jambo la msingi kujifunza
kuamini mitikisiko ya kihisia iliyomo ndani mwetu, mitikisiko yenye nishati
kubwa sana inayotokana na mlango huu wa sita wa fahamu. Nishati ambayo
inatikisika kupitia hali yetu ya kujitambua na kutuongoza kwenye safari ya
nafsi, katika maisha kwa ujumla.
Hivyo
basi mlango huu wa sita kwa binadamu unahusu umuhimu kwa binadamu kuzingatia
masuala ya kiroho ambayo ndiyo yanayoigusa moja kwa moja nafsi yake na kuipatia
nishati inayohitajika kwa ajili ya kuendelea kudumu hapa duniani na kutimiza
yale yote iliyopangiwa kuyatimiza.
Kupuuza
ukweli na umuhimu wa jambo hili ndiko kunakowafanya binadamu waendelee
kutesana, kuumizana na hata kuuana. Vilevile faida nyingine inayotokana na
kuutambua na kuutumia mlango huu, ni ile inayomfanya binadamu autambue kweli
kwamba, binadamu katika ujumla wao ni kitu kimoja na wanategemeana kwa kila
hali.
Hivyo,
basi lolote unalomfanyia mwingine ni sawa na kujifanyia mwenzako ni sawa na
kujifanyia wewe mwenyewe. Kwa hiyo tunapoamini kuhusu mtikisiko huu uliomo
ndani mwetu, ndipo tunaweza kusawazisha hali na kuwa na amani ndani mwetu.
Nikutakie
maisha mema na endelea kuwashirikisha wengine kuweza kujifunza kupitia mtandao
huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.