Feb 12, 2016
Kushindwa Kupanga, Ni Kupanga Kushindwa.
Katika maisha hakuna kitu chenye thamani kama
kuwa na mipango imara yenye kutekelezeka kila siku. Ili ufanikiwe katika maisha
ni lazima uwe na mipango, bila ya mipango hakuna mafanikio katika maisha yako kabisa.
Mipango ya maisha ndiyo dira na mwongozo wa mtu katika kuyafikia mafanikio na
maisha mazuri.
Mtu mwenye mipango huwa na malengo katika
maisha yake. Mtu mwenye malengo huishi maisha ya ndoto yake. Mtu mwenye
malengo hapangiwi maisha yake hujituma yeye mwenyewe. Mtu asiye na mipango ni
mtumwa wa maisha yake.
Kukosea kupanga ni kupoteza ndoto zako na
kutimiza ndoto za wenzio waliopanga mipango ya maisha yao. Kwa nini watu
wanashindwa kupanga maisha yao? Na kwa nini wengine wameweza kupanga mipango
yao katika maisha na kutimiza ndoto zao?
Sababu kuu ya kuweza au kushindwa kupanga
mipango katika maisha iko katika KUFANYA MAAMUZI. Maamuzi yako ndio huamua
kupanga kwako au kushindwa kupanga ktk Mipango yako ya maisha. Leo naomba
nikupe njia 10 nzuri za kufanya kabla ya kufanya maamuzi na mipango yako ktk
maisha:-
JIWEKEE MALENGO. |
1. Usifanye haraka katika kutoa maamuzi.
2. Jipe muda wa kutosha kufikiri kabla ya kutoa
maamuzi.
3. Lipime na kulitazama jambo kwa marefu na
mapana kabla ya kutoa maamuzi.
4. Tafuta ushauri kwa wataalamu.
5. Tumia makosa yako ya nyuma kama njia ya
kujifunza.
6. Sikiliza Hisia zako yaani sauti yako ya
ndani.
7. Usitoe maamuzi ukiwa na hasira.
8. Angalia ni nini makusudio ya maamuzi yako.
9. Chunguza ni nini athari za maamuzi yako.
10. Jielewe udhaifu wako na mapungufu yako katika
kufanya maamuzi yako.
Asante kwa kutembelea na kufuatilia blog yetu waalike
na wengine ili wafaidike na makala tunazotoa hapa.
Makala hii imeandaliwa na Shariff H. Kisuda a.k.a Mzee wa Nyundo Kali.
Simu; 0715-079993
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.