Feb 17, 2016
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuitengeneza Tabia Yako Kabla Tabia Yako Haijakutengeneza Wewe.
Tabia ni mazoea yaliyopitiliza kiwango cha kawaida. Ni mazoea
yaliyozidi kawaida. Mazoea yakizidi katika kufanya jambo lolote ndio hujenga
tabia. Kwa maana hiyo basi tunapata ukweli kuwa tabia njema au mbaya tunatengeneza
wenyewe kutokana na mazoea. Kuwa na tabia njema au mbaya ni uamuzi wa mtu
binafsi katika kuamua kuacha au kuendelea kufanya kitu chenye kujenga au
kubomoa na kuharibu kabisa tabia yake.
Kwa mfano ukizoea kunywa kunywa mwisho utakuwa mlevi. Ukizoea
kuibaiba mwisho utakuwa mwizi. Ukizoea kusomasoma utakuwa msomaji mzuri. Ukizoea
kulimalima utakuwa mkulima. Mazoea yanajenga Tabia. Hivyo ukitaka
kufanikiwa ni maamuzi yako na ukitaka kutofanikiwa pia ni maamuzi yako.
Kila unachofanya katika maisha yako kitakupa matokea halisi ya
kile unachofanya haijalishi ni matokeo hasi au chanya. Ndio maana wataalamu wa
saikolojia tunasema ukitaka kujua tabia ya mtu mwambie akuonyeshe marafiki zake. Huu
ni ukweli wa asilimia mia moja. Huwezi kuwa na marafiki walevi wewe usinywe, utakuwa jiniazi kama mzee wa
nyundo. Huwezi kuwa na marafiki wahuni nawe usalimike ngumu utashawishika
tu.
TENGENEZA TABIA ZA MAFANIKIO. |
Ukikaa na ua waridi nawe utanukia, ukikaa na wasomi nawe
utaelimika, ukikaa na watu wenye ‘vision’ nawe utabalika. Hapo ndipo
tunaposema binadamu mafanikio yake ni jumla ya watu watano anao amka nao, kushinda
nao na kulala nao ‘that's all about
success’.
Maisha ya mafanikio ni rahisi leo nakuibia siri.
1.Tambua uwezo wako katika kufikiri na kutenda.
2.Tambua kipawa/kipaji chako.
3. Kuwa mkweli na muwazi.
4. Chagua marafiki wa kwenda nao sambamba wenye malengo na maono
yanayofanana na yako.
5. Jiamini kuwa unaweza kama mimi navyojiamini. Leo mtu
ukimwambia leo toa somo atakuambia siwezi, wewe nani alizaliwa anaongea na
kujua majina ya vitu?
6. Kuwa na ‘network’ ya watu wazuri unao link nao katika kutafuta
mafanikio.
7. Jenga tabia ya kutopoteza muda wako bure kwa vitu vya kipuuzi
ambavyo havina faida katika maisha yako.
8. Kuwa na ratiba katika kufanya vitu vyako.
9. Kuwa na bajeti na nidhamu katika matumizi yako ya pesa.
10. Ondoa Hofu katika mambo unayofanya .
11. Kuwa na vipaumbele katika maisha yako. Na vipaumbele viko vya aina 6
tutajifunza mbeleni katika masomo yajayo.
Kwa leo naomba tuishie hapa na ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Endelea kuwasharikisha wengine waweze kufaidi na makala
tunazotoa hapa.
Ni wako rafiki katika kuyasaka mafanikio ya kweli,
Shariff Kisuda aka Mzee wa Nyundo Kali,
Simu; 0715 079 993,
Email; kisudashariff@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.