Feb 10, 2016
Kama Unatafuta Mafanikio Makubwa, Huwezi Kukwepa Maumivu.
Mabadiliko makubwa ambayo unayahitaji katika maisha yako kuna wakati huwa hayaji kirahisi tu kama tulivyozea, ila huja na kuambatana na maumivu. Maumivu haya ambayo unakuwa unayapata wakati mwingine hupelekea hata kujiona kama umekosea ndoto zako na usipokuwa makini unaweza kuachana na kile unachokifanya katika maisha yako.
Jaribu
kuangalia kile kipindi ambacho ulikuwa umejiwekea malengo yako makubwa na
ambapo ulitakiwa kujizuia na baadhi ya mambo ili malengo yako yatimie, ni nini
ambacho kilitokea? Bila shaka uliumia sana kwa kuona unajikosesha raha ya kuishi
au umekosa uhuru fulani hivi.
Lakini
si hivyo tu hata wale rafiki zako uliokuwa nao na ambao mlikuwa mna malengo
yanafanana wengine waliachana na wewe na kuamua kuishi maisha yao ya kawaida na
kusahau kwamba siku zote mafanikio makubwa yanapatikana kwa maumivu.
Jiulize
umeacha malengo mangapi mazuri kwa sababu ya maumivu ambayo umekuwa ukiyaona
yatakulemea kwa sababu ya mabadiliko unayotaka kufanya? Bila shaka ni mengi.
Hapo ndipo ulipokuwa ukikosea zaidi ulishindwa kutambua kwamba siku zote
mafanikio yanakuja kwa maumivu.
MAUMIVU NI SEHEMU YA KUKUSAIDIA KUFIKIA LENGO |
Ili
uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa unayoyataka, hii ni kanuni ambayo
hutakiwi kuikwepa, lazima uitekeleze. Kipo kipindi katika maisha ambacho
unatakiwa kuacha karibu kila kitu ikiwa pamoja na familia, usingizi, kuachana
na marafiki kwa muda na kuacha mambo mengi matamu kwako kwa sababu ya
mafanikio.
Bila
kufanya hivyo au kuachana na mambo hayo kwa muda inakuwa ni ngumu kufikiwa
mafanikio makubwa, zaidi unaweza ukawa ni mtu wa mafanikio madogo na ya kawaida
sana. Naamini hata ukifatilia watu wengi waliofanikiwa walifanya hivi na
kuachana karibu na kila kitu ili kutimiza malengo yao.
Hivyo
kitu cha kutambua hapa ni kwamba maumivu ni muhimu wakati mwingine ili kufikia
mafanikio yetu makubwa. Tatizo kubwa linalowakabili binadamu wengi ni ule
uasili wa kukataa mabaliko. Mara nyingi unapotaka kufanya kitu fulani nje ya
kile ulichokizoea mwili huwa unapiga kwelele sana.
Kama
unafikiri natania jaribu kuamka asubuhi na mapema kuliko kawaida yako uone nini
kitatokea. Mwili utakataa sana. Hali hiyo huja kwetu, nakuona kama maumivu fulani
ambayo hatujayazoea ambayo hutupelekea kuweza kukata tamaa au kuacha kabisa
kile tunachokifanya kwa mawazo ya kuona kama tunajitesa.
Lakini
kwa kuwa siku ya leo umeujua ukweli huu, tambua wakati mwingine mafanikio
yanakuja kwa maumivu. Inatakiwa ulitambue hilo na kuacha kukubaliana sana na
kile ambacho mwili wako unakwambia sana. kwa kufanya hivi utakuwa
unajitengenezea mazingira mazuri ya mafanikio yako.
Kama
kuna jambo unalifanya lifanye tu. Hata kama kuna wakati unajihisi umechoka,
unajihisi mwili unapiga kelele kama unaumia, jipe muda wa kuvumilia. Hayo kwako
ni mapito tu. Na mafanikio makubwa yoyote duniani mara nyingi huwa yanapatikana
kwa namna hiyo. Endelea kusonga mbele utafanikiwa.
Nikutakie
siku njema na endelea kutembelea mtandao wetu wa DIRA YA MAFANIKIO kuweza
kujifunza na kuhamsika. Waalike na wengine ili waweze kufaidika na mafundisho
mazuri yanayoendelea hapa.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.