Dec 19, 2016
Je, Wajua! Kila Kitu Hutokea Kwa Sababu Maalumu?
Kijana mmoja baaada ya kuhitimu
masomo yake ya chuo alipanga kwenda kumtembelea mjomba wake ambaye kwa wakati
huo alikuwa anaishi kijijini. Kijana Aliamua kufanya hivyo kwani zilikuwa
zimepita siku nyingi bila kuonana kwa mjomba wake.
Hivyo siku uliyofuata kijana aliamka
asubuhi na mapema kabla jua halijaleta faraja kwa watu wake, alijiaanda
kwa kasi zaidi ya 4G kabla ya kuanza safari ya kuelekea kijijini
kwani muda haukuwa rafiki kwake.
Kwa kuwa safari ilikuwa ni ndefu sana
kijana huyo aliamua kubeba chakula ambacho kingemsaidia kupungunguza njaa
wakati wa safari, safari iliendelea huku kijana mawazo ya mjini akiyaacha na
wenye miji yao huku akili yake ikiwa ina shuaku na msukumo thabiti kuhusu
maisha ya kule kijinini.
Ilipofika mida ya muda wa mchana kwa
kuwa njaa ilikuwa inamuuma sana alichua chakula chake na kuanza kula.
Aliuamini ule usemi ambao unasema "usiudharau mkono kwa sababu ya
kijiko" hivyo chakula kile alikula kwa kutumia mkono ambao anaumini
zaidi, lakini kama ujuavyo wakati wa safari utaratibu wa kunawa mikono wakati
wa safari huwa si zingatio sana aliamua kula bila hata kunawa mikono yake.
Baada ya dakika chache kula chakula
kile, tumbo la ghafla lilimkamata huku akikaa kila aina ya mkao ujuao wewe
katika siti ile, alifanya vile ili kuyanusuru maumivu ambayo yalikuwa
yametawala katika tumbo. Hata hivyo kadri muda ulivyozidi kuyoyoma na tumbo
nalo lilikuwa linazidi kuuma zaidi.
Aliwaza ni kitu gani ambacho
kimesababisha tumbo lake kuuma, lakini kadri anavyozidi kuzama katika dibwi la
halmashauri ya fikra zake aligundua ya kwamba chakula alichokula kulikuwa ni
chanzo cha kuuma kwa tumbo lake.
Hivyo safari iliendelea mpaka
alipowasili katika kijiji ambacho alikuwa anaishi mjomba wake.
Mjomba alifurahi kumuona kijana yule,
lakini mjomba alishtuka kumuona kijana yule akiwa hana furaha, ndipo mjomba
akaamua kushirikisha mdomo katika kumuuliza swali kijana yule ni kipi ambacho
kimemtoa katika ulimwengu furaha, ndipo kijana akamueleza mjomba wake tumbo
lilikuwa linamsumbua kidogo.
Baada ya mjomba kusikia hayo
alimueleza ya kwamba asipate tabu kwani atakuwa sawa muda si mrefu, walipofika
nyumbani kwa mjomba, mjomba alimpa dawa za miti shamba, kijana yule baada
ya kula alikuwa sawa.
Baadae mjomba pamoja na kijana yule
walikaa katika mkeka kwa ajili ya kupata chakula. Chakula chenyewe ulikuwa ni
ugali wa mhogo pamoja nyama ya swala.
Chakula kile kilikuwa ni kitamu sana
kwani kilikuwa kimepikwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Wakati wanaendelea
kula huku hadithi mbalimbali zilikuwa zimetawala mahali pale kwani muda mrefu
ulikuwa umepita bila wao kuonana. Lakini katika ya maongezi yao mjomba
hakusahau kumpongeza kijana yule kwa kuhitimu masomo yake ya chuo.
Basi huku maongezi yao yakiendelea
walijikuta chakula kimeisha bila hata wao kujua. Hivyo kijana yule akaona asiwe
mchoyo wa fadhira hivyo akaamua kumshukuru mjomba kwa chakula kitamu, lakini
zaidi alisema ya kwamba alifurahishwa na nyama ile.
Lakini mjomba alimuahidi siku
iliyofuata kwamba wangeambatana pamoja kwenda kuwinda pamoja. Kijana yule
alifurahi maneno hayo kutoka kwa mjomba wake kwani alitamani kujua mbinu
amabazo zilitumika kuwinda. Kwani alimini ule usemi "usimpe mtu
samaki" bali mpe samaki siku ya kwana siku inayofuata mpe nyavu akavue
mwenye.
Ilipofika asabuhi na mapema kila
mmoja aliamka akiwa ni mzima wa afya tele, kijana alimuuliza mjomba wake ni
muda gani ambao wangeenda mawindoni? Mjomba akamwambia ya kwamba muda wa
kufanya mawindo ni muda wa usiku ambapo wanyama wengi huwa wamechoka sana.
Hivyo ingefaa waendee muda usiku.
Hivyo ilipofika usiku mjomba pamoja
na kijana yule walichukua dhana za uwindaji kwa ajili ya kuelekea mawindoni.
Harakati za mawindo zilikuwa zimepamba moto katikati ya msitu, lakini matarajio
yao yalikuwa hayapo sawa kwani hawakupata hata mnyama mmoja lakini hawakukata
tamaa waliendelea kufanya mawindo.
Muda ulizidi kwenda bila ya kupata
chochote. Kijana yule alikuwa amechoka sana, kwani aliamini ya kwamba kufanya
mawindo ni kitu rahisi sana. Kwa kuwa kijana yule alikuwa amechoka sana, licha ya
kuchoka alikuwa tayari ana usinginzi mzito, Hivyo mjomba aliamuru washushe hema
ili waweze kupumzika. Waliingia ndani ya hema na kulala ndani ya hema.
Baada ya dakika chache wote
walipitiwa na usingizi mzito ndani ya hema lile, baada ya masaa machache mjomba
alishtuka usingizini hivyo akaamua amuamshe kijana yule. Mjambo alimuasha
kijana yule, kijana aliamka, mjomba akamuuliza kijana "unaona nini
angani?" kijana akajibu naona nyota pamoja na mwezi unaoangaza kwa
mwanga mzuri.
Mjomba akauliza tena
"unachokiona kinamanisha nini? Kijana akajibu ya kwamba kile anachokiona
ni ishara ya kwamba Mungu yupo pamoja nao, pia mng'ao wa nyota
zinaonyesha ya kwamba siku uliyofuata ilikuwa ni njema . mjomba akasema umejibu
vyema, lakini tumeibiwa hema hivyo kikubwa zaidi nilitegemea utajibu ya kwamba
"tumeibiwa hema"
Mwisho umejifunza nini kupitia kisa
hiki?
Tafsiri ya kisa hicho ni;
Kisa cha hadithi hii ni kwamba wapo
baadhi ya watu wamekuwa na maisha magumu kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa
kupambanua vitu kwa mapana, hata hivyo naweza nikasema tumekuwa tukiishi
katika hali ya kimazoea. Wengi tumekuwa tukitazama mambo kwa kuanza na vitu
ambavyo vinaonekana mbali kuliko kuanza na vitu vilivyopo karibu.
Kwa mfano wahitimu wengi wa vyuo
huamini ya kwamba baada ya kuhitimu masomo yao ni ajira, wao hawaamini ya
kwamba wanaweza kujiri. Wapo baadhi ya watu ambao wanaishi mahali fulani
wanawaza kwenda sehemu nyingine huku wakiamini kufanya hivyo ni njia ya
mafanikio kwao, lakini ukweli ni kwamba kila mahali ambapo leo hii upo pana
fursa.
Hivyo chunguza kwa umakini na uweze
kujua fursa zile ambazo zinakuzunguka ndipo uje kuwaza fursa ambazo zipo
nje na hapo ulipo.
Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba
kiporo hakihitaji moto mwingi, maana yangu ni kwamba mafanikio yako hayahitaji
mambo makubwa sana ila yanahitaji kujiongeza zaidi kwa kila kitu ambacho
unakifanya.
Ndimi; Afisa mipango Benson Chonya,
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.