Dec 1, 2016
Matumizi Sahihi Ya Muda Yanavyoweza Kukupa Mafanikio.
Mwandishi mmoja wa kitabu cha
"Mikasa ya Maisha" alieleza mengi sana kuhusu maisha ambayo
ameyapitia mpaka kufikia ndoto zake, lakini katika kitabu chake hicho
nilijifinza mengi sana. Ngoja nichukue japo dakika chache kuweza kukushirikisha
kwa kile ambacho nilijifinza katika kitabu hicho.
Mwanzano mwa kurasa za awali katika
kitabu hicho alianza kwa kusema:
Kitendawili..............
Unaweze ukaitikia (Tega.......!)
Ni kitu gani kirefu kuliko vyote? Na pia
wakati huohuo ni kifupi kuliko vyote?
Na kitu hicho hicho, wakati mwingine
kikitumiwa vizuri huleta faraja, na endapo kitatumiwa vibaya huleta majuto.
Mwandishi akauliza je, ni kitu gani hicho?
Je wewe mwenzangu unafikiri ndio
ungekuwa katika chumba cha mtihani umeulizwa swali hilo ungejibu nini? Maana
hata mimi wakati najiuliza juu ya kitendawili hicho nilikosa majibu, wakati
nafikiria majibu, nikaona niendelee kwenda sambamba na mwandishi ili kujua
kusudio la swali lake. Basi mwandishi akasema ya kwamba kitu hicho ni
"MUDA"
Mwandishi akaendelea kusema ya kwamba
muda ni kitu cha dhania tu, ambacho mtu huhisi, pia muda hauwezi kuishika kwa
kutumia mikono. Akaendelea kusema ya kwamba muda umegawanyika katika sekunde,
dakika, masaa, siku, wiki, mwezi, mwaka.
Lakini pia muda kama huna jambo la
kufanya huonekana ni mrefu sana, hapa ndipo tunapokutana na wale ambao husema
ya kwamba siku ya leo ilikuwa ndefu sana.
Pia muda ukiutumia vizuri katika
uzalishaji mali huonekana ni mfupi, hii ni kutoka na vile ambavyo umejipanga
katika kuuthamini muda, katika suala zima la kuweza kufanya vitu vya
msingi. Swali la kujiuliza hapa muda ulionao ni mrefu au mfupi, kama ni mrefu
unafikiri ni kwanini usinipe majibu?
Lakini vile vile muda kama ukitumia
vizuri wakati huu, huleta faraja kubwa sana maishani. Watu wengi hushindwa
kuutumia muda vizuri wakati bado wana nguvu na mwisho wa siku huja kulalamika
mbeleni ya kwamba maisha ni magumu, yote hayo hutokea hasa pale mtu
anaposhindwa kuitumie leo yake vizuri.
Hivyo ni vyema ukaitumia leo yako
vizuri ili uweze kuitengeneza kesho yenye furaha na faraja kwako.
Nimesema hayo kwa sababu watu wengi
hufa na ndoto zao kwa sababu ya kutokutambua umuhimu wa muda, jambo hilo
hutokea kwa sababu wao waliamini ya kwamba mafanikio yao yataanza kesho, lakini
ukweli ni kwamba mafanikio huanza leo haijalishi utaanza kwa hatua ndogo kiasi
gani.
Hivyo nikwambie ya kwamba mafanikio
ni vile ambavyo utaamua kuutumia muda ambao uanao, hata uwe ni muda kidogo
kiasi gani bali utumie kwa manufaa.
Ndimi; Mkeleketwa Wa Mafanikio Afisa
mipango Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.