Dec 6, 2016
Sahau Kuhusu Elimu, Mafanikio Yako Yanahitaji Kitu Hiki Kwanza.
Moja
kati ya uongo mkubwa, ambao umekuwa ukijidanganya na kufanya ushindwe
kufanikiwa ni kule kuamini kwako kwamba, eti hujafanikiwa kwa sababu hujasoma
sana au huna shahada toka chuo chochote.
Ili
kupata matokeo unayoyahitaji katika maisha yako ikiwa pamoja na kufanikiwa haihitaji
uwe umesoma sana, bali mafanikio ni matokeo ya kuweka nguvu na juhudi kwa kile
unachokifanya kila siku.
Kama
unaendelea kuamini hujafanikiwa kwa sababu hukusoma hili ni kosa kubwa
sana unaloendelea kulifanya kwenye safari yako ya mafanikio na linakukwamisha
pia.
Je.
hivi unajua kwamba dunia imejaa watu wengi sana na waliofanya mambo makubwa bila
kuwa na elimu kubwa kama ya chuo kikuu kama unavyofikiri?
Inawezekana
hujui hili ndio maana unarudi nyuma kimafanikio kwa kuendelea kuamini uongo huo
ambao unajirisha pole pole. Lakini ngoja nikwambie hivi tena, maisha yana
washindi wengi sana ambao hawakusoma sana.
Biashara.
Richard
Branson ambaye ni mfanyabiashara mkubwa dunia na mmiliki wa kampuni ya ‘virgin’ ambapo chini yake zipo kampuni
ndogo ndogo 500, aliacha shule akiwa na umri wa miaka 15 na hakurudi tena.
Pamoja
na kuacha shule katika umri huo, aliamua kutafuta mafanikio yake bila sababu. Leo
hii mafanikio yake ni makubwa sana na inasemekana anao utajiri unaofikia kwa
sasa dola za kimarekani bilioni 5.
Viwanda.
Katika
eneo la viwanda tunaona Henry Ford hakuwa na elimu ya chuo kikuu. Elimu yake
ilikuwa ni ya kawaida tu. Hata hivyo huyu ndiye moja ya wagunduzi wa kwanza wa
gari na alifanikiwa kutengeneza kiwanda chake cha magari.
Wagunduzi.
Steve
Jobs anatajwa kama ni mtu ambaye alikaa chuo miezi sita tu. Hilo halikumuzuia
kutumia maarifa yake, matokeo yake aliibuka kuwa ni moja ya wagunduzi wakubwa
duniani, yeye aligundua kompyuta aina ya ‘apple.’
Waandishi.
William
Shakespeare aliacha shule pia na hakuweza kuendelea na masomo, lakini huyu ndiyo
mwandishi aliyapata kugundua maneno zaidi ya 2000 ya lugha ya kiingereza na pia
kuandika kazi zingine nyingi za kifasihi kwa lugha hiyo.
Sayansi.
Albert
Einstein alishindwa kabisa mtihani ambao ulitakiwa umwezeshe kuingia chuo
kikuu. Lakini Albert ni moja ya mtu ambaye alitokea kuwa na mchango mkubwa sana
katika mambo ya sayansi katika karne ya 20 mpaka leo.
Muziki.
Hapa
pia tunamwona mwanadada Aretha Franklin, hakuweza kuendelea na shule kwa sababu
ya kupewa ujauzito akiwa na umri wa miaka 14. Hata hivyo alitumia kipaji chake
cha uimbaji na kuibuka kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kuimba muziki aina ya ‘Rock’ .
Ukiangalia
orodha hii ya watu waliofanikiwa bila kuwa na elimu kubwa ni ndefu mno na inaendelea
tena na tena.
Watu
hawa na wengine wengi ukiwafatilia utagundua kilichowafanikisha ni matokeo ya
kuweka nguvu, juhudi na kuondoa hofu zote zinazowazuia kufanikiwa, hicho ndicho
kilichotokea na ndio siri ya mafanikio yao.
Kumbuka
wakati wote mafanikio sio elimu ya chuo kikuu peke yake, bali mafanikio ni
matokeo ya kuweka nguvu na juhudi kubwa kwa kile unachokifanya kila siku.
Bila
kuweka juhudi na nguvu kubwa, hata uwe na elimu kubwa vipi huwezi kufanikiwa na
hilo liko wazi. Ni vyema ukatambua nguvu na juhudi yako ndiyo itakayokupa mafanikio
haijalishi uwe umesoma au hujasoma.
Nikutakie
kila la kheri katia kuelekea mafanikio makubwa.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.