Dec 16, 2016
UTAFITI; Mwanamke Huota Tofauti Na Mwanaume.
Wanasema
mwanamke na mwanaume ni tofauti kwenye baadhi ya mambo, kimaumbile. Lakini, sio
yale mambo yenye kuonekana peke yake, kwani imebainika sasa ni kwamba, tofauti
huenda hadi kwenye usingizi. Ni kwamba mwanamke na mwanaume huota tofauti.
Kwa
hiyo, hata wakiwa usingizini, mwanamke na mwanaume wanaendelea na tofauti zao.
Dk.
Mark Blagrove, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia, anasema kwamba, yeye pamoja na
mwenzake wamefanya utafiti kwa watu zaidi ya 100,000 na kubaini kwamba, kuna
tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hasa linapokuja suala la kuota ndoto.
Utafiti
uliofanywa na Blagrove na wenzake umehusisha watu wa dunia nzima, sio ulaya na
marekani peke yake.
Hivyo,
ni utafiti ambao unazungumzia jambo linalohusu dunia nzima, siyo upande fulani
tu wa dunia.
Ipo tofauti kubwa kati ya ndoto ya mwanaume na mwanamke. |
Katika
utafiti huo, wamegundua kwamba, wanandoa ambao wamelala kitanda kimoja, ubavu
kwa ubavu, wanakuwa na ndoto tofauti kabisa, ingawa wanaweza wakawa wanaota
wakati mmoja.
Ndoto
za wanawake zinaonekana wazi zinahusu kazi, zimejaa hisia sana ndani yake na
huchukua muda mrefu zaidi.
Mwanamke
anaweza kusimulia kuhusu ndoto yake, ukadhani imechukua saa kadhaa kuota kwa
jinsi ilivyo ndefu. Huwa wanaota ndoto moja kwa muda mrefu zaidi.
Ndoto
za wanawake zimejengwa kwenye msingi wa nyumbani na kuhusisha watu wengi na
hasa wa familia zaidi, kuliko watu wa nje ya familia.
Kwa
upande wa ndoto za wanaume, kuota wageni ni jambo la kawaida sana kwao. Wageni,
ina maana watu ambao hawawafahamu. Ndoto za wanaume zimejengwa kwenye msingi wa
maeneo ya barabara, magari na vurugu.
Hauwezi
kupita muda mrefu kabla mwanaume hajaota kuhusu gari, barabara au vurugu za
aina fulani.
Huhusisha
pia tendo la ndoa na wanawake wasiowajua, mara nyingi.
Ndoto
za wanaume pia zimejengwa pia kwenye mazingira ya kazi, na kuhusiana na hofu za
kipato na hofu za kupoteza kazi au kufilisika. Zimejaa masuala ya kazi au
shughuli.
Mwanasaikolojia
aliyeandika pia vitabu kadhaa kuhusu ndoto, Veronica Tonay, anasema, utafiti
huu unathibitisha tafiti za siku nyingi ambazo zilikuwa zinadai kwamba,
wanawake huota tofauti na wanaume.
Hivi
sasa, inaweza kusemwa kwamba, suala hilo halina utata tena. Inaonyesha pia
kwamba, zaidi ya nusu ya watu wote wanapata ndoto mbaya angalau mara moja kwa
wiki.
Kuna
wengine ambao ndoto mbaya ni sehemu ya maisha yao ya kindoto,yaani karibu kila
siku zinawatokea.
Inaelezwa
kwamba, kazi anayofanya mtu inaweza kuchangia kwenye kuwa kwake na ndoto za
jinamizi au ndoto mbaya.
Kwa
mfano, wauguzi wahasibu na watumishi kwenye vyombo vinavyohusiana na
mawasiliano, ndiyo ambao hukumbwa sana na ndoto hizi mbaya.
Kukimbizwa,
meno kudondoka, kuanguka, kutegewa au kuwekewa kizuizi, ni miongoni mwa mada
zinazootwa sana, hasa na wale wanaoota majinamizi.
Wanasaikolojia
wanasema, ndoto zinahusiana na shughuli ambazo hatujazimaliza kwenye mpangilio
wetu wa kazi wa siku au kujaribu kufanya kile ambacho tulishindwa kukifanya
tukiwa macho.
Kwa
mfano, kuota kupata fedha, jambo ambalo katika hali ya kawaida, limekuwa gumu
kwetu.
Watafiti
hapo wanazidi kuchambua ndoto kwa kusema kwamba, ndoto zinazohusu mambo mabaya
ndizo ambazo zinaotwa zaidi kuliko zile zinazohusu mambo mazuri.
Hata
wale watu wenye furaha maishani, wanaonekana kuota ndoto zenye mada
zisizopendeza kuliko mada zenye kupendeza.
Ingawa
wataalamu wa ndoto wanasema, kila ndoto ina maana kutegemea na mtu aliyeota,
utafiti huu unaonyesha kwamba, pamoja na kuwa hilo ni kweli, kuna mambo ambayo
mtu mmoja akiyaota , maana yake ni ile ile kwa mtu mwingine yeyote.
Kwa
mfano, kuanguka, kwenye ndoto ina maana ya mtu kukosa uhakika wa usalama.
Kukimbizwa
au kufukuzwa, bila kujali ni nani anaota, inaweza kuwa na maana ya kukimbia
matatizo.
Ndoto
ya kupoteza au kung’oka meno inahusiana na mtu kujali namna anavoonekana au
sura.
Ndoto
ya mtu kukimbia, lakini lakini akajikuta bado yupo pale pale, yaani hasogei,
ina maana au inahusiana na mtu kuwa na kazi nyingi kumzidi uwezo.
Ndoto
ya mtu kuwa uchi, ina maana kwamba, mhusika ana matamanio ya kuwasiliana na
mwingine au wengine.
Kile
ktiendo cha kuvua nguo ndotoni kina maana ya mtu kuondoa vikwazo vinavomkabili
kwenye maisha ake.
Pamoja
na kwamba, lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuona kama mwanamke na mwanaume
wanaota tofauti, bado umezaa masuala mengine muhimu ynayohusiana na ndoto. Moja
ya hili lilozaliwa ni maana ya ndoto, ambazo hazibadiliki, bila kujali ni nani
ameziota.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja
tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.