Apr 25, 2018
Elimu Ya Fedha Katika Biashara Inatakiwa Kuwa Hivi.
Itakuwa ni bure kama unafanya biashara au unataka kufanya
biashara kama utakuwa huifahamu elimu ya fedha. Elimu ya fedha ndiyo
msingi mkubwa wa maisha yako na biashara yako kiujumla.
Elimu ya fedha katika biashara yako
inahusika na jinsi ya kupata fedha hizo na jinsi ya kufanya sizipotee.
Elimu ya fedha pia inahusisha masuala mazima kwa ajili ya
kujua kile ambacho kinapatikana na kutumika. Isipojua jinsi ya kupangalia
mapato na matumizi yako katika biashara ni sawa bure.
Hivyo ili kuwa mtunza kumbukumbu mzuri katika biashara
yako unatakiwa kuwa na daftari la kumbukumbu ambalo litahusiana na kuweka
kumbukumbu zako za kifedha na biashara yako.
Ijue vyema elimu ya fedha ikusaidie kufanikiwa katika biashara yako. |
Kwani kuweka kumbukumbu katika daftari kunasaidia kwa
kiwango kikubwa kujua kama unapata faida au unapata hasara. Pia kumbukumbu za
kibiashara husaidia kuweza kupata taarifa kwa kile kinachoingia na kutoka
katika biashara yako.
Lakini nitakuwa sijakutendea haki kama nitashindwa
kukueleza ukweli kwamba katika elimu ya fedha lazima ujue ya kwamba fedha
inahitaji nidhamu hasa katika upande wa uwekaji akiba.
Kama umeamua kuitenga fedha kwa ajili
ya kuindeshea biashara yako basi jitahidi ubaki katika reli hiyo.
Lakini kama hiyo haitoshi tunashauriwa kwa katika suala la
uwekaji akiba ni lazima uwe kila baada ya muda fulani. Hii ikiwa na maana
kama umeamua kutenga kila siku shilingi elfu kumi basi fanya hivyo kwani hii
itakusaidia kuweza kuboresha biashara yako pale ambapo itakuwa haifanyi vizuri.
Na wataalamu wa mambo wanasema asilimia 10 ndizo
zinatumika kutenga katika uwekaji akiba, hii inategemeana na kile
unachokipata.
Lakini pia pesa yeyote ambayo unapata ni lazima uigawe
katika mafungu matano ambayo ni:-
Akiba.
Uwezekaji.
Matumizi ya lazima.
Matumizi yasiyo yalazima.
Fungu la kumi.
Endelea kusoma ukurasa huu kila
wakati nitakuelezea kwa undani kuhusu ya ugawaji wa fedha ambazo
unazipata, ila kwa leo tu ni kwambie ya kwamba uhuru wa kifedha katika
biashara unahitaji mambo yafutayo:
1. Kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni siri ambayo ipo katika kupata
fedha ambazo unazihitaji.
2. Nidhamu.
Fedha inahitaji nidhamu katika kuipata na namna ambavyo
unaweza kuitumia, maana fedha ina makelele mengi, hivyo inahitaji kufanya mambo
ya msingi hasa pale inapopatikana.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba uyaweke yale
niliyokueleza katika matendo maana usipofanya hivyo itakuwa ni sawa na kupika
makande kwa mwanga wa mshumaa.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya,
Apr 24, 2018
Mambo Kumi Ya Kujikumbusha Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.
Safari ya mafanikio ina mambo mengi ambayo unatakiwa uyajue na kuyafanyia kazi kila siku. Na unapoyafata mambo hayo ndio unazidi kujitengenezea msingi mkubwa wa kufanikiwa kwako kwa kile unachokifanya.
Leo
katika makala haya nakukumbusha baadhi ya mambo ya msingi ya wewe kuyakumbuka
kwenye safari yako ya mafanikio. Haya ni mambo ya msingi kwa sababu, ukiyatumia
yatakutoa kutoka kwenye hatua moja na kukupeleka hatua nyingine.
Yafuatayo Ni Mambo Kumi Ya Kujikumbusha
Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.
1. Unapowasaidia
watu, ujue hiyo ni sawa na kujisaidia
wewe mwenyewe. Itafika wakati ule msaada unaoutoa kwa ajili ya watu wengine nao
msaada huo utakurudia wewe kwa namna ya tofauti ambayo hujaijua bado.
2.
Hakuna matokeo ya papo kwa papo ambayo unaweza kuyapata kwa chochote kile
unachokifanya kwenye maisha yako. Unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi na
kusubiri. Mafanikio ni matokeo ya kuwekeza juhudi na kuweza kusubiri. Kama
hutaki kusubiri sahau kupata mafanikio yoyote makubwa maishani.
3. Ni
muhimu kuboresha afya, ni muhimu kuboresha kipato, ni muhimu kuboresha
mahusiano sahihi na wengine na muhimu pia kuwa na maarifa bora na sahihi.
Unapokuwa unaboresha mambo hayo kila siku unajitengenezea uhakika mkubwa wa
kuyafanya maisha yako kuwa bora sana karibu kila siku.
4.
Kama kuna kitu unakihitaji kweli na kwa moyo wote, ni kweli lazima kitu hicho
hata iweje ni lazima utaweza kukipata, Hautaweza kuweka sababu wala hutaweza
kutoa visingizio kivile. Utakachokifanya ni kufanya kila linalowezekana mpaka
kitu hicho uweze kukipata. Ni kipi ambacho unakitaka, usiweke sababu, kitu
hicho utakipata.
5.
Moja ya kitu ambacho unatakiwa kukisahau kabisa
ni juu ya umri wako na kuendelea kuishi. Umri wako usikuzuie kufanya kitu
chochote, bali wewe kama ni kuwekeza endelea kuwekeza sahau habari ya kwamba
sasa hivi umri wako ni mkubwa. Kama unababaishwa na umri utapotea na maisha
yanaendelea kusonga mbele.
6.
Maisha ya kufanya makosa ni bora zaidi kuliko kuishi maisha ambayo hufanyi
makosa kabisa. Ni bora uishi kwa kufanya makosa kabisa na hiyo itakusaidia
kufika mbali kuliko ukae tu hufanyi kitu kisa eti unaogopa kukosea.
7.
Mara nyingi kwenye maisha hatuoni vitu kama vilivyo kwa uhalisia wake, bali
tunaona vitu kama tunavyoviona sisi kwa mitazamo yetu na sio kinyume cha hapo.
8. Hamna
kitu cha maana kuwa nacho kama amani moyoni mwako. Unapokuwa na amani moyoni
hiyo ndiyo inayokupa nguvu ya kufanya mambo makubwa kwa jinsi unavyotaka wewe.
Anza leo kutengeneza amani moyoni ili ikupe faida kubwa kwako.
9. Unaweza
kufurahia maisha yako popote na wakati wowote pasipo kujali mtu, kitu au hali
ya aina fulani. Ni kitendo cha kuamua kuyafurahia maisha yako tu, na ukishaamua
kuyafurahia maisha yako na kweli utayafurahia hayo maisha.
10. Kama
unaweka nguvu za uzingativu, juhudi na mabadiliko chanya kwenye kila hatua unayofanya,
hata kama huoni mabadiliko ya wazi, tambua kabisa, wakati utafika maisha yako
yatabadilika kabisa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Apr 23, 2018
Ukijifunza Kanuni Hizi Na Kuzifanyia Kazi, Utafanikiwa.
Kila mtu anaweza akawa na mafanikio akiamua. Mafanikio si uchawi ni sayansi tu ya kujifunza kanuni za mafanikio na kuzifanyia kazi kila siku. Watu wenye mafanikio wanajua kucheza na kuzitumia kanuni za mafanikio na kuweza kuwafanikisha.
Leo katika makala haya
nataka tuzungumzie moja ya kanuni muhimu za mafanikio, ambazo ukizifanyia kazi
na utafanikiwa. Nimesema kama utazifanyia kazi zitakusadidia kufanikiwa lakini
kama usipozifanyia kazi utaendelea kubaki hapo ulipo kama ulivyo.
1. Picha unazoziweka kichwani mwako.
Kati ya kitu ambacho
unatakiwa kukichunga sana ni picha ambazo unaweka kichwani mwako. Yapo matokeo
makubwa sana kwa yale mambo ambayo unayoyaweka kichwani mwako kila wakati.
Jaribu kuangalia ni vitu
gani ambavyo unaviweka akili mwako kila mara. Mambo hayo unayoyaweka akili
mwako kila wakati, basi ujue mambo hayo ni rahisi kuweza kukutokea. Hii ni kanuni
ambayo unatakiwa kuichunga na kuitumia.
2. Vitendo vyako.
Unaweza ukawa una ndoto zako
nzuri sana, lakini kama huchukui hatua hiyo ni sawa na kazi bure. Unatakiwa kujua
jinsi ya kuchukua hatua kwa yale mawazo ambayo unayo. Hatua ndizo zitakazo
kusaidia kukufikisha kwenye ndoto ulizonazo.
Watu wengi wanaokwama kwenye
maisha, ni watu ambao wanakwama kwa sababu
ya kushindwa kuchukua hatua zinazostahili kwenye maisha yao. Chukua hatua leo
mapema kwa chochote kile unachotaka kukifanya na utaweza kufanikiwa.
3. Nidhamu.
Hutaweza kufanikiwa kwa
chochote kwenye maisha yako kama huna nidhamu. Kila wakati nidhamu inahitajika
kwenye ndoto zako, kwenye kazi na kila eneo ili uweze kufanikiwa. Ukikosa nidhamu
upo kwenye wakati mgumu wa kushindwa.
Jenga nidhamu kwa chochote
kile ambacho unakifanya na nidhamu hiyo itakuongoza kuweza kufanikiwa. Wanaoshindwa
ni watu ambao kwa dhahiri naweza nikasema ni watu ambao hawana nidhamu kabisa
maishani mwao.
4. Kujitoa.
Picha unazoziweka, vitendo
vyako na nidhamu ni moja ya kanuni muhimu za kukusaidia kufanikiwa, lakini hivi
haviwezi kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hautaweza kujitoa. Ni muhimu sana
kujitioa kwenye ndoto zako.
Toa kila kinachowezekana ikiwa
ni pamoja na muda wako, nguvu zakio na kila kitu cha muhimu ili ikusaidie kufanikiwa.
Usipojitoa kwenye ndoto zako ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwa sababu kuna
changamoito na mambo mengi yanayotakiwa kukabiliana nayo.
Ukiweza kufanyia kazi kanuni
hizi, zitakusaidia sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Apr 20, 2018
Hii Ndio Athari Ya Hatua Chanya Na Thamani Unayoitengeneza.
Hatua chanya unazozichukua, haziishii kwako tu, bali hatua hizo huzidi kwenda zaidi na zaidi na kuweza kuwafikia watu wengine ambao hata hukuweza kufikiri kama hatua hizo chanya zinaweza kuwafikia.
Thamani
unayotengeneza, pia thamani hiyo haiwezi kuishia kwako, thamani hiyo huweza
kuenea na kusambaa na kuweza kuwasaidia watu ambao hata pia hukifikiri kwamba
inaweza ikawasaidia watu hao ambao hata huwajui kwa sura.
Leo
hii kuna sehemu, maisha ya watu ya watu yanakuwa bora kwa sababu ya hatua
ambazo ulizichukua kipindi cha nyuma na hatua hizo zinawasaidia kuboresha
maisha yao na kuonekana ni bora zaidi, lakini chanzo kikubwa ukiangalia ni
wewe.
Huwezi
kutawala na huwezi kujua hatua zako chanya zitafika wapi, kikubwa unachotakiwa
kufanya ni kuzidi kuchukua hatua chanya na kutengeneza thamani iliyobora ambapo
thamani hiyo itawasaidia wengine hata kama wewe hupo.
Kwa jinsi
unavyowekeza nguvu zako katika hatua chanya na kutengeneza thamani, unatakiwa
ujue kuna maisha ya mtu ambayo unayobadili hata kama maisha hayo huyaoni leo,
lakini kuna mtu atasaidiwa na wewe pasipo kujua.
Kwa hiyo
unachotakiwa kuelewa usiangaliae matokeo ya sasa kwa kile unachokipata na
kukifanya, angalia nguvu zako jinsi ambavyo zitakavyosambaa na kuwasaidia watu
wengine kuweza kupiga hatua za maisha yao pia.
Fanya
kilichobora leo, tengeneza thamani iliyobora zaidi kwako kila siku na thamani
hiyo itaenea karibu kila eneo kwa jinsi siku zinavyokwenda. Hakuna nguvu yako
ambayo itapotea kama unaweka thamani na kutoa yale yaliyo mazuri kwako.
Angalia
hata ulipo kuna mambo mazuri unayatumia ni kwa sababu ya hatua chanya na
thamani kubwa ambazo kuna watu walizichukua na hiyo inakusaidia hata wewe
kuweza kufaidi matunda yao.
Hilo
ni fundisho kwako usiwe sehemu ya kutoa mambo hasi na hayo pia yanaweza
yakasambaa na kuwaathiri watu wengine. Tengeneza thamani na kutoa mambo chanya
ili uwe sehemu ya kuitengeneza dunia ikawa ni sehemu salama.
Ishi
maisha yako kwa kutoa yaliyochanya na kutengeneza thamani inayotakiwa kila
siku. Ukiwa utafanya hivyo utakuwa ni sehemu kubwa ya mabadiliko makubwa ya
dunia. Hii ndio athari ya hatua chanya na thamani unayoitengeneza.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha
ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
`
Apr 13, 2018
Nyuma Ya Pazia La Mafanikio.
Mafanikio yoyote unayoyaona kwa nje mara nyingi yanatengenezwa sana na hatua au vitu visivyoonekana, kile unachoona ni matokeo yake tu.
Kazi
fulani inapokamilika na mafanikio yake kuonekana kwa nje, ni wazi dunia nzima inakuwa
makini kushangaa kwa kuyaona mafanikio yale yaliyotokea.
Lakini
kuna kuwa hakuna mtu ambaye anakuwa yupo tayari kufatilia mchakato wa nyuma ya
pazia ni nini kilifanyika hadi kuibua mafanikio hayo.
Na
kwa sababu hiyo ya kuangalia mafaniko au matokeo ya nje, yote hiyo hupelekea
kuwaona watu wenye mafanikio ni kama watu wenye bahati sana.
Ikiwa
utang’ang’ania kuangalia mafanikio ya nje ya watu na kuchanganyikiwa nayo na
kusahau kwamba kuna nyuma ya pazia la mafanikio, umepotea.
Mchezaji
wa mpira anaonekana anafanya vizuri uwanjani, ujue nyuma yake kuna mazoezi
mengi sana ameyafanya tayari.
Mpiganaji
bora wa ngumi duniani unayemwona anang’ara na kuchukua ushindi wa kila aina ujue
kabisa huyo kafanya mazoezi mengi ya kutosha yaliyompa ushindi huo.
Biashara
yoyote inayoonekana ina mafanikio makubwa haikuanzia pale, nyuma ya pazia la
mafanikio, ilianzia mbali sana na pengine na mtaji mdogo na wa kawaida sana.
Hiyo
yote inaonesha mafanikio yanajengwa na vitu vidogo sana, vitu ambavyo kuna
wakati kama havionekani, lakini baadae huleta matokeo makubwa.
Utakata
tamaa na kujiona mshindwaji kama utakuwa unaangalia mafaniko kwa kuona tu
matokeo yaliyopo sasa na kusahau, kuna vitu vinatengenezwa nyuma ya pazia.
Ushindi
na mafanikio hauendi kwa watu wenye bahati kama unavyofikiri wakati mwingine
kwamba ndivyo ulivyo.
Ushindi
na mafanikio unakwenda kwa kila mtu ambae ameamua kujenga nidhamu, kujituma, kuwa
king’ang’anizi na kuwa chanya wakati wote.
Angalia nyuma ya pazia la
watu wenye mafanikio, utajua na wewe ufanye nini, ujitume vipi na uweke juhudi
gani zinazotakiwa.
Lakini ukiwa utakuwa
unaangalia matokeo yao na kushindwa kuangalia nyuma ya pazia hutaweza kujifunza
kitu cha kukusaidia.
Mafanikio yote makubwa
yanatengenezwa nyuma ya pazia la mafanikio, huko ndiko mafanikio yanakopikwa na
kuandaliwa haswaa, mengine unayoyaona ni matokeo.
Usiendelee kusubiri,
tengeneza mafanikio yako nyuma ya pazia na hayo matokeo yatakuja kuonekana huko
mbeleni, kama huoni matokeo kwa sasa usijali.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Apr 12, 2018
Inawezekana Kubadili Maisha Yako Sana…Ukiamua Kufanya Hivi.
Kila wakati unapofikiria na kikiwaza kile kitu unachokita ili kikutokee, uwe na uhakika na ujue kabisa kitu hicho kitawezekana na kutokea.
Kila
wakati unapojenga mategemeo chanya kwa kile ukifanyacho, tambua pia mategemeao
hayo yatawezekana na kuwa kweli katika uhalisia.
Kila
wakati unapoweka juhudi na kujitoa kikamilifu kwa kile ukifanyacho, uwe na
uhakika inawezekana kufikia lile lengo lako ambalo umejiwekea.
Kila
wakati unapokuwa upo tayari kuendelea kuchukua hatua na hata kama mbele yako
kuna changamoto kubwa sana za kimaisha, tambua inawezekana kufanikiwa.
Kila
wakati unapoamua kuwa king’ang’anizi na hadi kuhakikisha ndoto zako zinatimia,
pia unatakiwa kujua kwamba hilo linawezeka na ndoto zako zitatimia.
Kila
wakati unapojifunza kutokana na makosa unayofanya na ukachukua hatua za
kujirekebisha kwenye makosa yako utafika wakati itawezekana kufanikiwa kwako.
Kila
wakati unapoamua kuendelea mbele hata kama umekatishwa tamaa, itafika wakati
pia ujue kufanikiwa kwako ni lazima utafanikiwa kwa sababu umeamua.
Kila
wakati unapoamua kupambana na hali hatarishi, hali za kuogopesha zinakufanya
uone ndoto zako hazitimii, ujue muda utafika itawezekana kufanikiwa kwako.
Unapaswa
ujue kila hali unayotegemea, kila juhudi na kila kujitoa ambako unafanya kila
siku, huko ndiko kutakapokupa mafanikio makubwa maishani mwako.
Hakuna
ambaye anategemea kile kilichobora na halafu mwisho wa siku akabaki kama jinsi
alivyokuwa mwanzoni.
Kitu
cha kuzingatia ni kuwa mvumilivu na kujua kwamba mabadiliko katika maisha
hayaji mara moja tu au ghafla, mabadiliko yanakuja wakati mwingine kidogo
kidogo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Apr 6, 2018
Ifanye Hii… Iwe Sababu Ya Kufanikiwa Kwako.
Pale unapokuwa na kazi nyingi za kufanya na unaona kama hutaweza kukamilisha kazi hizo, hiyo sio sababu pekee ya kukufanya wewe ukate tamaa.
Pale
unapoona njia ya kufikia mafanikio yako ni ndefu sana, na unaiona mafanikio
yako kama yanachelewa vile, hiyo pia si sababu ya wewe kuweza kukata tamaa.
Kwa
vyovyote vile unapoona ugumu wa kufanikiwa na kukatishwa tamaa na vitu kama
hivyo, fanya sasa hiyo ndio iwe sababu ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Usitishwe
na njia ya mafanikio yako ni ndefu au usitishwe kwa kuona kwamba una majukumu
mengi, hapo ndipo unapotakiwa wewe kukaza mwendo kuelekea mafanikio yako.
Unapokuwa
na vitu vingi zaid vya kufanya na vinakutaka wewe, hapo ndipo ipo fursa pia ya
kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Unapoona
njia ya mafanikio ni ndefu, hapo ndipo huo wakati wa wewe kuweza kutafuta njia
nyingine za kuweza kukusaidia kukufanikisha.
Unapaswa
kujua mafanikio makubwa yanakuja katikati ya changamoto nyingi zaidi, na
changamoto hizo ndizo unazotakiwa kukabiliana nazo na kuzishinda.
Matajiri
unaowaona, walifanikiwa katika njia hizi hizi ambazo hata wewe kuna wakati
unaona kwa njia hii kufanikiwa ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa tena.
Unapokutana
na magumu, unapokutana na hali ya kuona kama njia yako ya mafanikio ni ndefu
sana na haiwezi kufika hiyo isiwe sababu ya kufanya ukashindwa.
Kila
wakati jaribu kutafuta sababu ya kufanikiwa pale unapokutana na ugumu au kuna
njia ya mafanikio ni ndefu kwako.
Unapaswa
kujua hakuna maisha pasipo changamoto na changamoto zipo ili tuweze kuzishinda
na kutupa sisi mafanikio.
Ndio
maana kuanzia leo unatakiwa kujua kwa uwazi kabisa, fanya sababu yoyote ile
inayokupa ugumu wa kuweza kufanikiwa kiwe ndio chanzo cha mafanikio yako.
Kikubwa
unatakiwa uwe mvumilivu na usiwe mtu wa kuweza kukata tamaa mapema kwani
hautaweza kufika mbali kama utakuwa ni mkata tamaa mapema.
Unapokutana na magumu na unapoona njia ya mafanikio ni ndefu kwako huo ndiio wakati wa
kutafuta kwako kung’aa kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Apr 2, 2018
Andika Mawazo Yako na Ukae Kimya.
Watu wengi wana mawazo mazuri, wana ndoto
kubwa, lakini mojawapo ya sababu ya kwanini hakuna kinachofanyika ni kwamba
wengi tunaongea sana. Utakuta mtu ndo kwanza amepata wazo la kufanya kitu
fulani, lakini saa hiyo hiyo anaanza kuwashirikisha anaowaita marafiki zake. Na
kuanzia hapo inakuwa kila siku ni...
kuongea ongea juu ya wazo hilo jipya.
Baada ya siku si nyingi, anapata wazo jingine na hapo lile la mwanzo linasahaulika na anaanza kuongelea wazo jipya. Mwisho wake ni kwamba unaendelea kujenga mazoea ya kufikiri wazo na kulitoa kwa marafiki na ndugu basi! Matokeo yake miaka inavyozidi kwenda unajikuta huna mradi wowote wa biashara ambao umeweza kuufanikisha.
Tabia hii ya kupenda kuwashirikisha wazo lako changa watu wengine, inakuingiza kwenye hatari kubwa sana. Kwasababu hao unaojaribu kuwashirikisha wazo lako, yawezekana ni watu ambao hawajawahi kuwazia wazo lako kwa kiwango ambacho wewe unafikiri juu ya wazo hilo. Lakini pia, hao wanaoitwa marafiki, unaweza ukakuta kuwa ni wale watu ambao hawana hamasa yoyote ya kufanikiwa, ni wavivu, wabinafsi na inawezekana hapo walipo wamefika mwisho, wamebakia kusubiri muujiza utokee ndipo watajirike—jaribu kuwa mwangalifu!
Baada ya siku si nyingi, anapata wazo jingine na hapo lile la mwanzo linasahaulika na anaanza kuongelea wazo jipya. Mwisho wake ni kwamba unaendelea kujenga mazoea ya kufikiri wazo na kulitoa kwa marafiki na ndugu basi! Matokeo yake miaka inavyozidi kwenda unajikuta huna mradi wowote wa biashara ambao umeweza kuufanikisha.
Tabia hii ya kupenda kuwashirikisha wazo lako changa watu wengine, inakuingiza kwenye hatari kubwa sana. Kwasababu hao unaojaribu kuwashirikisha wazo lako, yawezekana ni watu ambao hawajawahi kuwazia wazo lako kwa kiwango ambacho wewe unafikiri juu ya wazo hilo. Lakini pia, hao wanaoitwa marafiki, unaweza ukakuta kuwa ni wale watu ambao hawana hamasa yoyote ya kufanikiwa, ni wavivu, wabinafsi na inawezekana hapo walipo wamefika mwisho, wamebakia kusubiri muujiza utokee ndipo watajirike—jaribu kuwa mwangalifu!
Katika hali ya kawaida haiwezekani wewe upate kuwa na wazo zuri mwezi mzima
halafu umshirikishe rafiki yako na yeye siku na saa hiyo hiyo akwambie “haiwezekani”.
Ukiamua kumsikiliza kama wengi tunavyofanya nakuhakikishia kuwa itaendelea kuwa
vigumu sana kwako kuweza kufanikisha mradi wowote wa maana. Ebu! Fikiria rafiki
yako, anakwambia, hicho kitu unachotaka kufanya hakijawahi kufanywa na mtu
yeyote na kwamba wewe utawezaje? Eti! unaambiwa husifanye jambo fulani
kwasababu hakuna aliyewahi kufanya hivyo—ushauri wa namna hii utaendelea
kuupata sana, kama utaendelea kuwa mtu wa kuongeaongea tu!
Unapoamua kumwaga mawazo yako kwa wengine, ujue kuwa kwa namna moja au nyingine yatapokelewa kwa hisia na mtazamo tofauti kulingana na uelewa wa watu unaowambia. Mara nyingi watu wakiambiwa jambo ambalo liko nje ya fikra zao au uelewa wao, moja kwa moja upata hofu na baadae woga, kutegemea na ukubwa na upya wa wazo lako. Wakishapata hofu juu ya wazo lako, kinachofuata ni kutaka kujaribu kuhamishia hofu yao kwako. Hapo wataanza kukupa mifano ya watu waliowahi kujaribu na wakashindwa, watakueleza hatari zote zinazoweza kujitokeza endapo utendelea na mpango wa kutekeleza wazo lako hilo. Kwahiyo, wewe bila kujua, unashitukia umeambukizwa woga na hofu ambayo kimsingi hukuwanayo hapo awali.
Baadhi ya maneno yanayodhihirisha hofu ya marafiki zako juu ya wazo lako ni kama maneno ya “huwezi”, “haiwezekani”, “ni ngumu sana kufanikiwa” n.k. Ndiyo maana ukiendelea kuhubiliwa maneno hayo mara kwa mara, utajikuta taratibu taratibu unaanza kuyaamini. Hali hii ndiyo mwisho wake ukusababishia kukosa ujasiri wa kuthubutu pindi zinapotokea fursa mbalimbali.
Kwa taarifa yako ni kwamba pale rafiki au ndugu yako akikwambia“huwezi” maana yake ni kwamba yeye ndiye “hawezi”. Mara zote usilichukulie jibu la “huwezi” kama ndiyo jibu lako. Pia, usijaribu kulitumia jibu la “huwezi” kama kisingizio au kikwazo cha kukuzuia wewe kutekeleza wazo lako kama ulivyolifikiria hapo awali.
Achana na kuongea ongea sana! Maneno ya nita……anza biashara, shule, kutafuta pesa, kufanya mazoezi mwaka huu hayasadii sana. Nataka nikwambie kwamba maneno yote ya “nita….nita…!” ni kuongea tu! Na ni sawa na “mvuke”—hakuna vitendo hapo.
Nitawezaje kuendeleza wazo langu bila kuongea?
Sasa, ili kuepuka mawazo yako kuwa kama “mvuke”, inabidi kuanzia sasa kila ukipata wazo zuri, cha kwanza kufanya ni kuliandika na kisha kulifanyia kazi huku ukiwa kimya.
Unapoandika wazo lako, unapata fursa ya
kutathimini kile ulichotakiwa kufanya kwa kulinganisha na kile ulichokifanya. Mfano; kama
umeanza siku yako usiongee kwamba mimi leo nitafanya hili na lile; wewe
unachotakiwa ni kuandika orodha ya mambo ambayo unatakiwa kuyafanya kwa siku
hiyo basi! Kama yale uliyoyaandika kwenye orodha umekamilisha asilimia 40% basi
ujue kuwa bado wewe ni walewale waongeaji tu! Lakini kama utakamilisha kuanzia
asilimia 70-100%, basi ujue kuwa sasa umeanza kuwa mtu wa vitendo zaidi na siyo
maneno.
Hapa nizidi kukusihi kuwa, kila wakati ujitahidi kuruhusu vitendo vikuongoze na siyo kuongozwa na maneno. Tumia muda wako mwingi kutenda na kila wakati “yape nafasi matendo yako yaongee kwa sauti”kuliko maneno.
Kila ukipata wazo zuri kumbuka kauli mbiu hii “andika mawazo yako na ukae kimya”.
Hapa nizidi kukusihi kuwa, kila wakati ujitahidi kuruhusu vitendo vikuongoze na siyo kuongozwa na maneno. Tumia muda wako mwingi kutenda na kila wakati “yape nafasi matendo yako yaongee kwa sauti”kuliko maneno.
Kila ukipata wazo zuri kumbuka kauli mbiu hii “andika mawazo yako na ukae kimya”.
Makala
hii imeandikwa na cypridion mushongi wa maarifashop.blogspot.com, unaweza
kujifunza zaidi juu ya mafanikio kwa kutembelea blog yake.
Apr 1, 2018
UJUMBE WA PASAKA; Tenda Wema Kwa Faida Hizi Kwako.
Habari za muda mpenzi
mzomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio bila shaka u mzima na unaendelea
vyema na majukumu yako ya kila siku.
Ikiwa leo ni tarehe 1/4/2018
ambapo wakristo wote duniani wanasherekea siku za kufufuka kwa bwana wetu Yesu
Kristo yaani ni sikukuu ya pasaka.
Siku hii huenda sambamba
na kipindi chenye tafakari kubwa yenye kuwataka wakristo wote duniani kote
waweze kutafakari uwepo na uweza wa matendo makuu ya mwenyezi Mungu.
Kwa Misingi hiyo Uongozi
mzima wa Mtandao huu wa DIRA YA
MAFANIKIO inapenda kukutakia sikukuu njema ya Pasaka, huku ujumbe wetu
mkubwa kwako ikiwa ni kwamba hakikisha unaitumia siku hii katika
kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kuhakikisha unakuwa ni mtu Mwema na si kutenda
dhambi.
Tunasiitiza juu ya hilo
kwa sababu watu wengi hutumia siku hii katika kufanya maovu ambayo ni chukizo
mbele ya Mungu wetu, yamkini yawezekana vipo vishawishi mbalimbali ambavyo
vitajitokeza katika siku ya leo, unachopaswa kukifanya ni kujitenga mbali na
vitu hivyo. Hata maandiko yanasema ya kwamba jicho lako likikukosea ling'oe.
Hivyo katika siku hii epuka sana marafiki ambao watakusababisha uingie katika kutenda maovu, kwani maovu ni dhambi na pia ni chukizo mbele za mwenyezi Mungu.
Hivyo katika siku hii epuka sana marafiki ambao watakusababisha uingie katika kutenda maovu, kwani maovu ni dhambi na pia ni chukizo mbele za mwenyezi Mungu.
Tukutakie sikukuu njema
ya Pasaka.
Imeandaliwa na uongozi
mzima wa Blog hii ya dira ya mafanikio na kuletwa kwako nami Afisa
Mipango Benson Chonya.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)