Apr 24, 2018
Mambo Kumi Ya Kujikumbusha Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.
Safari ya mafanikio ina mambo mengi ambayo unatakiwa uyajue na kuyafanyia kazi kila siku. Na unapoyafata mambo hayo ndio unazidi kujitengenezea msingi mkubwa wa kufanikiwa kwako kwa kile unachokifanya.
Leo
katika makala haya nakukumbusha baadhi ya mambo ya msingi ya wewe kuyakumbuka
kwenye safari yako ya mafanikio. Haya ni mambo ya msingi kwa sababu, ukiyatumia
yatakutoa kutoka kwenye hatua moja na kukupeleka hatua nyingine.
Yafuatayo Ni Mambo Kumi Ya Kujikumbusha
Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.
1. Unapowasaidia
watu, ujue hiyo ni sawa na kujisaidia
wewe mwenyewe. Itafika wakati ule msaada unaoutoa kwa ajili ya watu wengine nao
msaada huo utakurudia wewe kwa namna ya tofauti ambayo hujaijua bado.
2.
Hakuna matokeo ya papo kwa papo ambayo unaweza kuyapata kwa chochote kile
unachokifanya kwenye maisha yako. Unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi na
kusubiri. Mafanikio ni matokeo ya kuwekeza juhudi na kuweza kusubiri. Kama
hutaki kusubiri sahau kupata mafanikio yoyote makubwa maishani.
3. Ni
muhimu kuboresha afya, ni muhimu kuboresha kipato, ni muhimu kuboresha
mahusiano sahihi na wengine na muhimu pia kuwa na maarifa bora na sahihi.
Unapokuwa unaboresha mambo hayo kila siku unajitengenezea uhakika mkubwa wa
kuyafanya maisha yako kuwa bora sana karibu kila siku.
4.
Kama kuna kitu unakihitaji kweli na kwa moyo wote, ni kweli lazima kitu hicho
hata iweje ni lazima utaweza kukipata, Hautaweza kuweka sababu wala hutaweza
kutoa visingizio kivile. Utakachokifanya ni kufanya kila linalowezekana mpaka
kitu hicho uweze kukipata. Ni kipi ambacho unakitaka, usiweke sababu, kitu
hicho utakipata.
5.
Moja ya kitu ambacho unatakiwa kukisahau kabisa
ni juu ya umri wako na kuendelea kuishi. Umri wako usikuzuie kufanya kitu
chochote, bali wewe kama ni kuwekeza endelea kuwekeza sahau habari ya kwamba
sasa hivi umri wako ni mkubwa. Kama unababaishwa na umri utapotea na maisha
yanaendelea kusonga mbele.
6.
Maisha ya kufanya makosa ni bora zaidi kuliko kuishi maisha ambayo hufanyi
makosa kabisa. Ni bora uishi kwa kufanya makosa kabisa na hiyo itakusaidia
kufika mbali kuliko ukae tu hufanyi kitu kisa eti unaogopa kukosea.
7.
Mara nyingi kwenye maisha hatuoni vitu kama vilivyo kwa uhalisia wake, bali
tunaona vitu kama tunavyoviona sisi kwa mitazamo yetu na sio kinyume cha hapo.
8. Hamna
kitu cha maana kuwa nacho kama amani moyoni mwako. Unapokuwa na amani moyoni
hiyo ndiyo inayokupa nguvu ya kufanya mambo makubwa kwa jinsi unavyotaka wewe.
Anza leo kutengeneza amani moyoni ili ikupe faida kubwa kwako.
9. Unaweza
kufurahia maisha yako popote na wakati wowote pasipo kujali mtu, kitu au hali
ya aina fulani. Ni kitendo cha kuamua kuyafurahia maisha yako tu, na ukishaamua
kuyafurahia maisha yako na kweli utayafurahia hayo maisha.
10. Kama
unaweka nguvu za uzingativu, juhudi na mabadiliko chanya kwenye kila hatua unayofanya,
hata kama huoni mabadiliko ya wazi, tambua kabisa, wakati utafika maisha yako
yatabadilika kabisa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.