Apr 25, 2018
Elimu Ya Fedha Katika Biashara Inatakiwa Kuwa Hivi.
Itakuwa ni bure kama unafanya biashara au unataka kufanya
biashara kama utakuwa huifahamu elimu ya fedha. Elimu ya fedha ndiyo
msingi mkubwa wa maisha yako na biashara yako kiujumla.
Elimu ya fedha katika biashara yako
inahusika na jinsi ya kupata fedha hizo na jinsi ya kufanya sizipotee.
Elimu ya fedha pia inahusisha masuala mazima kwa ajili ya
kujua kile ambacho kinapatikana na kutumika. Isipojua jinsi ya kupangalia
mapato na matumizi yako katika biashara ni sawa bure.
Hivyo ili kuwa mtunza kumbukumbu mzuri katika biashara
yako unatakiwa kuwa na daftari la kumbukumbu ambalo litahusiana na kuweka
kumbukumbu zako za kifedha na biashara yako.
Ijue vyema elimu ya fedha ikusaidie kufanikiwa katika biashara yako. |
Kwani kuweka kumbukumbu katika daftari kunasaidia kwa
kiwango kikubwa kujua kama unapata faida au unapata hasara. Pia kumbukumbu za
kibiashara husaidia kuweza kupata taarifa kwa kile kinachoingia na kutoka
katika biashara yako.
Lakini nitakuwa sijakutendea haki kama nitashindwa
kukueleza ukweli kwamba katika elimu ya fedha lazima ujue ya kwamba fedha
inahitaji nidhamu hasa katika upande wa uwekaji akiba.
Kama umeamua kuitenga fedha kwa ajili
ya kuindeshea biashara yako basi jitahidi ubaki katika reli hiyo.
Lakini kama hiyo haitoshi tunashauriwa kwa katika suala la
uwekaji akiba ni lazima uwe kila baada ya muda fulani. Hii ikiwa na maana
kama umeamua kutenga kila siku shilingi elfu kumi basi fanya hivyo kwani hii
itakusaidia kuweza kuboresha biashara yako pale ambapo itakuwa haifanyi vizuri.
Na wataalamu wa mambo wanasema asilimia 10 ndizo
zinatumika kutenga katika uwekaji akiba, hii inategemeana na kile
unachokipata.
Lakini pia pesa yeyote ambayo unapata ni lazima uigawe
katika mafungu matano ambayo ni:-
Akiba.
Uwezekaji.
Matumizi ya lazima.
Matumizi yasiyo yalazima.
Fungu la kumi.
Endelea kusoma ukurasa huu kila
wakati nitakuelezea kwa undani kuhusu ya ugawaji wa fedha ambazo
unazipata, ila kwa leo tu ni kwambie ya kwamba uhuru wa kifedha katika
biashara unahitaji mambo yafutayo:
1. Kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni siri ambayo ipo katika kupata
fedha ambazo unazihitaji.
2. Nidhamu.
Fedha inahitaji nidhamu katika kuipata na namna ambavyo
unaweza kuitumia, maana fedha ina makelele mengi, hivyo inahitaji kufanya mambo
ya msingi hasa pale inapopatikana.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba uyaweke yale
niliyokueleza katika matendo maana usipofanya hivyo itakuwa ni sawa na kupika
makande kwa mwanga wa mshumaa.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.