google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 23, 2018

Ukijifunza Kanuni Hizi Na Kuzifanyia Kazi, Utafanikiwa.

No comments :
Kila mtu anaweza akawa na mafanikio akiamua. Mafanikio si uchawi ni sayansi tu ya kujifunza kanuni za mafanikio na kuzifanyia kazi kila siku. Watu wenye mafanikio  wanajua kucheza na kuzitumia kanuni za mafanikio na kuweza kuwafanikisha.
Leo katika makala haya nataka tuzungumzie moja ya kanuni muhimu za mafanikio, ambazo ukizifanyia kazi na utafanikiwa. Nimesema kama utazifanyia kazi zitakusadidia kufanikiwa lakini kama usipozifanyia kazi utaendelea kubaki hapo ulipo kama ulivyo.

1. Picha unazoziweka kichwani mwako.
Kati ya kitu ambacho unatakiwa kukichunga sana ni picha ambazo unaweka kichwani mwako. Yapo matokeo makubwa sana kwa yale mambo ambayo unayoyaweka kichwani mwako kila wakati.
Jaribu kuangalia ni vitu gani ambavyo unaviweka akili mwako kila mara. Mambo hayo unayoyaweka akili mwako kila wakati, basi ujue mambo hayo ni rahisi kuweza kukutokea. Hii ni kanuni ambayo unatakiwa kuichunga na kuitumia.
2. Vitendo vyako.
Unaweza ukawa una ndoto zako nzuri sana, lakini kama huchukui hatua hiyo ni sawa na kazi bure. Unatakiwa kujua jinsi ya kuchukua hatua kwa yale mawazo ambayo unayo. Hatua ndizo zitakazo kusaidia kukufikisha kwenye ndoto ulizonazo.
Watu wengi wanaokwama kwenye maisha, ni watu  ambao wanakwama kwa sababu ya kushindwa kuchukua hatua zinazostahili kwenye maisha yao. Chukua hatua leo mapema kwa chochote kile unachotaka kukifanya na utaweza kufanikiwa.
3. Nidhamu.
Hutaweza kufanikiwa kwa chochote kwenye maisha yako kama huna nidhamu. Kila wakati nidhamu inahitajika kwenye ndoto zako, kwenye kazi na kila eneo ili uweze kufanikiwa. Ukikosa nidhamu upo kwenye wakati mgumu wa kushindwa.
Jenga nidhamu kwa chochote kile ambacho unakifanya na nidhamu hiyo itakuongoza kuweza kufanikiwa. Wanaoshindwa ni watu ambao kwa dhahiri naweza nikasema ni watu ambao hawana nidhamu kabisa maishani mwao.
4. Kujitoa.
Picha unazoziweka, vitendo vyako na nidhamu ni moja ya kanuni muhimu za kukusaidia kufanikiwa, lakini hivi haviwezi kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hautaweza kujitoa. Ni muhimu sana kujitioa kwenye ndoto zako.
Toa kila kinachowezekana ikiwa ni pamoja na muda wako, nguvu zakio na kila kitu cha muhimu ili ikusaidie kufanikiwa. Usipojitoa kwenye ndoto zako ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwa sababu kuna changamoito na mambo mengi yanayotakiwa kukabiliana nayo.
Ukiweza kufanyia kazi kanuni hizi, zitakusaidia sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.