Apr 13, 2018
Nyuma Ya Pazia La Mafanikio.
Mafanikio yoyote unayoyaona kwa nje mara nyingi yanatengenezwa sana na hatua au vitu visivyoonekana, kile unachoona ni matokeo yake tu.
Kazi
fulani inapokamilika na mafanikio yake kuonekana kwa nje, ni wazi dunia nzima inakuwa
makini kushangaa kwa kuyaona mafanikio yale yaliyotokea.
Lakini
kuna kuwa hakuna mtu ambaye anakuwa yupo tayari kufatilia mchakato wa nyuma ya
pazia ni nini kilifanyika hadi kuibua mafanikio hayo.
Na
kwa sababu hiyo ya kuangalia mafaniko au matokeo ya nje, yote hiyo hupelekea
kuwaona watu wenye mafanikio ni kama watu wenye bahati sana.
Ikiwa
utang’ang’ania kuangalia mafanikio ya nje ya watu na kuchanganyikiwa nayo na
kusahau kwamba kuna nyuma ya pazia la mafanikio, umepotea.
Mchezaji
wa mpira anaonekana anafanya vizuri uwanjani, ujue nyuma yake kuna mazoezi
mengi sana ameyafanya tayari.
Mpiganaji
bora wa ngumi duniani unayemwona anang’ara na kuchukua ushindi wa kila aina ujue
kabisa huyo kafanya mazoezi mengi ya kutosha yaliyompa ushindi huo.
Biashara
yoyote inayoonekana ina mafanikio makubwa haikuanzia pale, nyuma ya pazia la
mafanikio, ilianzia mbali sana na pengine na mtaji mdogo na wa kawaida sana.
Hiyo
yote inaonesha mafanikio yanajengwa na vitu vidogo sana, vitu ambavyo kuna
wakati kama havionekani, lakini baadae huleta matokeo makubwa.
Utakata
tamaa na kujiona mshindwaji kama utakuwa unaangalia mafaniko kwa kuona tu
matokeo yaliyopo sasa na kusahau, kuna vitu vinatengenezwa nyuma ya pazia.
Ushindi
na mafanikio hauendi kwa watu wenye bahati kama unavyofikiri wakati mwingine
kwamba ndivyo ulivyo.
Ushindi
na mafanikio unakwenda kwa kila mtu ambae ameamua kujenga nidhamu, kujituma, kuwa
king’ang’anizi na kuwa chanya wakati wote.
Angalia nyuma ya pazia la
watu wenye mafanikio, utajua na wewe ufanye nini, ujitume vipi na uweke juhudi
gani zinazotakiwa.
Lakini ukiwa utakuwa
unaangalia matokeo yao na kushindwa kuangalia nyuma ya pazia hutaweza kujifunza
kitu cha kukusaidia.
Mafanikio yote makubwa
yanatengenezwa nyuma ya pazia la mafanikio, huko ndiko mafanikio yanakopikwa na
kuandaliwa haswaa, mengine unayoyaona ni matokeo.
Usiendelee kusubiri,
tengeneza mafanikio yako nyuma ya pazia na hayo matokeo yatakuja kuonekana huko
mbeleni, kama huoni matokeo kwa sasa usijali.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.