Apr 6, 2018
Ifanye Hii… Iwe Sababu Ya Kufanikiwa Kwako.
Pale unapokuwa na kazi nyingi za kufanya na unaona kama hutaweza kukamilisha kazi hizo, hiyo sio sababu pekee ya kukufanya wewe ukate tamaa.
Pale
unapoona njia ya kufikia mafanikio yako ni ndefu sana, na unaiona mafanikio
yako kama yanachelewa vile, hiyo pia si sababu ya wewe kuweza kukata tamaa.
Kwa
vyovyote vile unapoona ugumu wa kufanikiwa na kukatishwa tamaa na vitu kama
hivyo, fanya sasa hiyo ndio iwe sababu ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Usitishwe
na njia ya mafanikio yako ni ndefu au usitishwe kwa kuona kwamba una majukumu
mengi, hapo ndipo unapotakiwa wewe kukaza mwendo kuelekea mafanikio yako.
Unapokuwa
na vitu vingi zaid vya kufanya na vinakutaka wewe, hapo ndipo ipo fursa pia ya
kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Unapoona
njia ya mafanikio ni ndefu, hapo ndipo huo wakati wa wewe kuweza kutafuta njia
nyingine za kuweza kukusaidia kukufanikisha.
Unapaswa
kujua mafanikio makubwa yanakuja katikati ya changamoto nyingi zaidi, na
changamoto hizo ndizo unazotakiwa kukabiliana nazo na kuzishinda.
Matajiri
unaowaona, walifanikiwa katika njia hizi hizi ambazo hata wewe kuna wakati
unaona kwa njia hii kufanikiwa ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa tena.
Unapokutana
na magumu, unapokutana na hali ya kuona kama njia yako ya mafanikio ni ndefu
sana na haiwezi kufika hiyo isiwe sababu ya kufanya ukashindwa.
Kila
wakati jaribu kutafuta sababu ya kufanikiwa pale unapokutana na ugumu au kuna
njia ya mafanikio ni ndefu kwako.
Unapaswa
kujua hakuna maisha pasipo changamoto na changamoto zipo ili tuweze kuzishinda
na kutupa sisi mafanikio.
Ndio
maana kuanzia leo unatakiwa kujua kwa uwazi kabisa, fanya sababu yoyote ile
inayokupa ugumu wa kuweza kufanikiwa kiwe ndio chanzo cha mafanikio yako.
Kikubwa
unatakiwa uwe mvumilivu na usiwe mtu wa kuweza kukata tamaa mapema kwani
hautaweza kufika mbali kama utakuwa ni mkata tamaa mapema.
Unapokutana na magumu na unapoona njia ya mafanikio ni ndefu kwako huo ndiio wakati wa
kutafuta kwako kung’aa kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.