google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 20, 2018

Hii Ndio Athari Ya Hatua Chanya Na Thamani Unayoitengeneza.

No comments :
Hatua chanya unazozichukua, haziishii kwako tu, bali hatua hizo huzidi kwenda zaidi na zaidi na kuweza kuwafikia watu wengine ambao hata hukuweza kufikiri kama hatua hizo chanya zinaweza kuwafikia.
Thamani unayotengeneza, pia thamani hiyo haiwezi kuishia kwako, thamani hiyo huweza kuenea na kusambaa na kuweza kuwasaidia watu ambao hata pia hukifikiri kwamba inaweza ikawasaidia watu hao ambao hata huwajui kwa sura.
Leo hii kuna sehemu, maisha ya watu ya watu yanakuwa bora kwa sababu ya hatua ambazo ulizichukua kipindi cha nyuma na hatua hizo zinawasaidia kuboresha maisha yao na kuonekana ni bora zaidi, lakini chanzo kikubwa ukiangalia ni wewe.
Huwezi kutawala na huwezi kujua hatua zako chanya zitafika wapi, kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuzidi kuchukua hatua chanya na kutengeneza thamani iliyobora ambapo thamani hiyo itawasaidia wengine hata kama wewe hupo.

Kwa jinsi unavyowekeza nguvu zako katika hatua chanya na kutengeneza thamani, unatakiwa ujue kuna maisha ya mtu ambayo unayobadili hata kama maisha hayo huyaoni leo, lakini kuna mtu atasaidiwa na wewe pasipo kujua.
Kwa hiyo unachotakiwa kuelewa usiangaliae matokeo ya sasa kwa kile unachokipata na kukifanya, angalia nguvu zako jinsi ambavyo zitakavyosambaa na kuwasaidia watu wengine kuweza kupiga hatua za maisha yao pia.
Fanya kilichobora leo, tengeneza thamani iliyobora zaidi kwako kila siku na thamani hiyo itaenea karibu kila eneo kwa jinsi siku zinavyokwenda. Hakuna nguvu yako ambayo itapotea kama unaweka thamani na kutoa yale yaliyo mazuri kwako.
Angalia hata ulipo kuna mambo mazuri unayatumia ni kwa sababu ya hatua chanya na thamani kubwa ambazo kuna watu walizichukua na hiyo inakusaidia hata wewe kuweza kufaidi matunda yao.
Hilo ni fundisho kwako usiwe sehemu ya kutoa mambo hasi na hayo pia yanaweza yakasambaa na kuwaathiri watu wengine. Tengeneza thamani na kutoa mambo chanya ili uwe sehemu ya kuitengeneza dunia ikawa ni sehemu salama.
Ishi maisha yako kwa kutoa yaliyochanya na kutengeneza thamani inayotakiwa kila siku. Ukiwa utafanya hivyo utakuwa ni sehemu kubwa ya mabadiliko makubwa ya dunia. Hii ndio athari ya hatua chanya na thamani unayoitengeneza.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





`


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.