Nov 24, 2017
Mambo Ambayo Unatakiwa Kuyakumbuka Kila Wakati.
U
hali gani mpenzi msomaji wa DIRA YA
MAFANIKIO naamini siku yako imekwenda poa na unaendelea kuweka juhudi za
kweli katika kubadilisha maisha yako. Kwa harakati hizo tu nakupa hongera na
endelea kupambana mpaka kieleweke.
Naomba
pia nitumie wasaha huu kuweza kukaribisha katika makala yetu ya leo ili tuweze
kujifunza juu ya mafanikio. Naamini unajua kujifunza hakuna mwisho, hivyo
unatakiwa kila siku kuweka maarifa ya kukusaidia, ukishindwa kufanya hivyo
utakwama.
Katika
makala yetu ya leo nitaomba tu nikukumbushe mambo ambayo unatakiwa uyakumbuke
kila wakati kwenye maisha yako . Ni
mambo ya msingi kwani yatakusaidia kuweza kuwa na mtazamo chanya na kubadili
mambo mengi sana kwako.
1. Mambo yaliyopita hayawezi
kubadilishwa tena.
Unatakiwa
kuelewa kama kuna mambo ambayo yameshapita huwezi kuyabadilisha tena hata kama
yalikuumiza au ulifanya makosa kiasi gani. Kwa sasa unatakiwa kuganga yajayo,
habari ya mambo yaliyopita yatumie kama fundisho tu kwako, lakini ndio
yameshapita, usiumize kichwa na kujilaumu sana.
2. Maoni ya watu hayaamui hatima ya
maisha yako.
Hata
siku moja usije ukakaa ukafikiri kwamba maoni ya watu wengine wanayosema juu ya
wewe ndiyo yanaamua maisha yako yawe vipi. Maisha yako yanabaki hivyo yalivyo
kwa sababu wewe umeamua yawe hivyo. Lakini usikubali hata siku moja maoni ya watu
yakurudishe nyuma na usiyatumie kama kisingizio.
3. Maisha yako yatakuwa mazuri tu
ukijipa muda.
Ukiamua
siku zote kubadilisha maisha yako unaweza. Kikubwa jipe muda wa kutosha
kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadalika. Haijalishi
unaona maisha yako ni magumu kiasi gani, lakini muda ndio kila kitu. Muda
unaweza kusawazisha mambo mabaya na yakawa mazuri kabisa. Tumia muda wako vizuri.
4. Utashindwa tu, kama utakata tamaa.
Ndoto
yoyote ile uliyonayo au ambayo unatamani kuifikia una uwezo mkubwa wa kuifikia.
Ila hautaweza kuifikia ndoto yako hiyo ikiwa utafika mahali wewe mwenyewe
utaamua kukata tamaa. Moja ya sumu kubwa ya kimafanikio ni kukata tamaa, ukikata
tamaa ujue kila kitu kwako kimeishia hapo na hutaweza kusogea tena.
5. Furaha ya kweli inapatikana ndani
mwako.
Ukweli
huu hautakaa ubadilike kamwe kwamba furaha ya kweli inapatikana ndani mwako na
wala si nje yako. Unaweza ukakazana sana kutafuta furaha nje kwa kufanya vitu
ambavyo unaamini vitakupa furaha, lakini ukivipata vitu hivyo unashangaa ile
furaha tena bado huna. Hivyo jifunze kutafuta furaha ya kweli ndani mwako.
6. Mawazo chanya, ni njia ya mabadiliko
chanya pia.
Mbinu
mojawapo ya kuwa na maisha bora. Ni kwa wewe kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa
na mawazo chanya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kuleta mabadiliko chanya pia.
Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kuwa na mlundikano wa mawazo mengi ambayo
kwao ni hasi. Kuwa na mawazo chanya ubadili maisha yako.
Yapo
mambo mengi ya kukumbuka kila unapoelekea kwenye mafanikio yako. Kwa leo hii
nimekukumbusha mambo haya machache. Kwa kuyafanyia kazi itakuwa sehemu kubwa ya
mabadiliko kwenye maisha yako.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.