Dec 10, 2017
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Ukipanda Nyasi, Usitegemee Kuvuna Mchele.
Karibu
rafiki na mpenzi msomaji wa matandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO katika siku ya leo, kuweza kujifunza hekima za maisha
na mafanikio. Inawezekana unajiuliza kwa nini tunajifunza hekima za maisha na mafanikio
na hekima hizi ni zipi?
Kupitia
makala hizi za hekima za maisha na mafanikio utakuwa ukijufunza, misemo au
mithali ambazo zilitolewa na wahenga zamani, lakini lengo lake likiwa ni
kufunza juu ya maisha na mafanikio kwa ujumla.
Yapo
mambo mengi ya kujifunza sana kupitia hekima za maisha na mafanikio. Ni jukumu
lako wewe kufanyia kazi hekima hizi ili ziweze kukubadilisha na kukutoa ulipo
na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha.
Karibu
rafiki yangu tuweze kujifunza pamoja, juu ya hekima hizi za mafanikio ambazo
nimekuandalia kwa siku ya leo.
1. Kujua njia sahihi ya unakotaka
kwenda, waulize wanaorudi na njia hiyo.
Hekima
hii ina maana kwamba, ukitaka kujua
wapi unaokoelekea kwenye maisha na hata mafanikio yako, ni vyema ukawauliza
wale ambao wanafanya kitu hicho ambacho unakifanya kuliko kukaa kimya tu ambako
hakuwezi kukusaidia.
Kwa mfano,
kama unafanya biashara ya viatu, ni
vizuri ukawauliza watu pia wanaofanya biashara ya viatu ili wakupe mwangaza wa
kipi ambacho unatakiwa kufanya kuliko kwenda kuwauliza watu wengine wanaofanya
biashara tofauti, hapo utakwama.
2. Usiogope kama unakua kidogo kidogo,
ogopa sana kama hukui kabisa.
Katika
hekima hii iko wazi inaonyesha kwamba kama kuna mabadiliko unayafanya hata kama
ni kidogo, wewe upo sahihi sana kuliko yule mtu ambaye hafanyi mabadiliko
yoyote yupo yupo tu na ameganda, mtu huyo
ndio hatari sana.
Kwa hiyo
kama kuna hatua unapiga hata kama ni kidogo sana, endelea kupiga hatua hizo
maana zitakusaidia kwenda mbele kuliko kama utakuwa hupigi hatua. Ukumbuke hatua
ni hatua hata kama ni kidogo vipi.
3. Ukipanda nyasi, usitegemee kuvuna
mchele.
Msingi
wa hekima hii imejikita kwamba kwa chochote kile unachokipanda kwenye maisha
yako uwe na uhakika utakivuna tu. Pasipo kujalisha unapanda nini, jiandae
kuvuna kile unachokipanda na usitegemee kuvuna kinyume cha hapo.
Kama
unapanda wema, jiandae kuvuna wema. Kama unapanda ubaya pia jiandae kuvuna ubaya
huo. Hakuna ambacho utaweza kukivuna kinyume na kile unachokipanda kwenye
maisha yako. Kuwa mwangalifu unapanda kitu gani, kwani utakivuna.
4. Fanya mambo mengi kwa busara, lakini
si kwa kutumia nguvu peke yake.
Hekima
hii pia inatuonyesha umuhimu wa kufanya mambo yetu mengi kwa kutumia busara
zaidi kuliko nguvu yaani kwa kulazimisha. Unapofanya mambo yako kwa kutumia
busara ni wazi mambo yako yataweza kufanikiwa.
Tambua
wapo watu ambao kazi yao badala ya kutumia akili, bali wao ni kulazimisha mambo
yaende kwa nguvu hata ndani yake busara haipo. Sasa hapa tunaonywa kutumia pia
busara lakini si nguvu peke yake.
Kwa leo
kutokana na hekima hizo za maisha na mafanikio tulizojifunza tunaishia hapa,
naamini kuna kitu umejifunza na utakitendea kazi mara moja.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.