Apr 20, 2016
Huu Ndio Mchango Sahihi Wa Marafiki Katika Maisha Yako.
Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu
ya kila siku. Aina ya kwanza ni marafiki
ambao ni wema na marafiki wabaya. Tukianza na kuangalia aina hiyo ya kwanza hao ni marafiki ambao ni watu ambao
wana mawazo chanya katika kushauri hata kutenda mambo mbalimbali. Pia katika
kundi hili la marafiki wapo marafiki wa aina hii wachache sana.
Aina ya pili ya marafiki hawa ni marafiki ambao ni watu ambao
hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa
tu.
Watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi
mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu
ambazo hatusatili kuishi na watu hao . Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba
ushauri kwa watu ambao sio sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona
marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao.
Tumekuwa tukushuhudia baadhi
ya wanafunzi ambao pindi waendapo
masomoni baada ya kufikia huko wamekuwa na tabia za ajabu hii ni
kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi. Tumeona baadhi ya vijana hao
wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,
utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana
watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.
Chagua marafiki sahihi kwenye maisha yako. |
Mpenzi msomaji wa makala haya naendelea tena juu ya somo hii la
marafiki. Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya
marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo
mazuri na kuwashirikisha marafiki zao, na marafiki hao wamekuwa wanazidi kuwakatisha
tamaa tu.
Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako na kumwambia nataka
kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki uliyenaye utamsikia
akisema biashara hiyo hatatoka kwa sabubu fulani anaifanya au fulani kaliteka
soko la biashara hiyo, hivyo hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya.
Ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya
jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye.
Wapo baadhi ya marafiki ambo wao ukiwashirikisha jambo lako na wao
huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata
kidogo.
Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua
marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki
sahihi ambao unahisi wewe wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke
wanasema ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua
marafiki wema. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya
maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.
Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika
jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia "always forward, backward
never" ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko. Marafiki sahihi
wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi kwa kile
ulichowashirikisha na sababu za msingi.
Swali dogo la kujiuliza marafiki ulio nao ni wema au wabaya? kama
ni wabaya unachukua jukumu gani baada ya kukupa somo hili? ni muda wako mzuri wa kufikiri juu ya jambo
hili na kuchukua uamuzi sahihi.
Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele
yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung'unike kutokana na magumu
unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie
nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa
bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana
mbele ya jamii.
Mwandishi: Afisa mipango na Maendeleo Benson
Chonya
Mawasiliano
simu; 0757-909942
Barua pepe; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.