Oct 6, 2021
Njia mbili ziletazo mafanikio maishani.
Katika kufikia mafanikio yoyote yale, huwa zipo njia za kuweza kufikia mafanikio hayo. Hakuna mafanikio ambayo yanapatikana nje ya njia husika za mafanikio.
Na kwa kawaida, zipo njia mbili bora za kuufikia mafanikio. Hizi ni njia halali ambazo zinatumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kweli na halali duniani.
Njia ya kwanza; Njia ya kawaida.
Hii ni njia ambayo mtu anafikia mafanikio makubwa kutokana na malengo anayoyafatilia kila siku. Hapa lazima uwe na malengo ya kuyafatilia kila siku.
Katika njia hii unakuwa na malengo yako, lakini wakati huo huo unakuwa unaenda nayo mdogo mdogo hadi kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Hii ni njia bora, inayoaminika, kwa sababu kuna kujifunza mengi ndani yake, ingawa inataka muda na uvumilivu, lakini mwisho wa siku utafika.
Njia ya pili; Njia isiyo ya kawaida.
Hii ni njia isiyo ya kawaida kwa sababu ndani yake kuna kuwa na hali hatarishi nyingi. Kwa mfano, kuna kuweka mtaji mkubwa ndani yake au kuchukua hatua kubwa kabisa.
Katika kutekeleza njia hii iko hivi, unakuwa unafata njia ile ya kawaida kama kawaida, isipokuwa katika njia hii kuna vitu ambavyo vinaongezeka.
Katika njia hii lazima utenge kiasi fulani cha pesa, ili kuingiza katika 'dili' ambazo zinajitokeza kati kati lakini wakati huo ukiendelea na njia ya kwanza.
Kufata njia ya pili hatumaanishi njia ya kwanza umeiacha, hapana unakuwa nayo, isipokuwa hii unaitumia kama ziada kutengenezea pesa ndefu.
Hizi ndio njia kubwa mbili, ambazo zinatumiwa na watu wengi
wenye mafanikio kuweza kufanikiwa. Ni muhimu kutumia njia zote mbili ili
kujihakikishia mafanikio.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Oct 5, 2021
Zingatia Jambo Hili Sana, Litakusaidia Kufanikiwa.
Inapotokea kuna kitu hukijui, kuwa mtu wa shukrani, kwa sababu umepata fursa nzuri ya kujifunza juu ya kitu hicho.
Inapotokea unapitia magumu katika maisha yako, shukuru pia, kwani magumu hayo yanakufanya uwe bora na imara.
Ikiwa pia unapitia changamoto sana, huo sio wakati wa kukimbia, bali ni wakati wako wa kujiboresha kimaisha.
Unapokuwa umechoka kwa sababu ya kazi, basi pia huo ni muda wa kushukuru, kwa sababu kuna mabadiliko umefanya.
Kama umefanya makosa, pia shukuru, kwa sababu hiyo inakukumbusha ni kipi ambacho hutakiwi tena kukifanya.
Ni rahisi sana kuwa na shukrani na mambo mazuri, lakini pia jifunze kuwa na shukrani hata kwenye changamoto.
Watu wengi si wepesi sana wa kushukuru pale wanapokutana na magumu. Ni watu ambao wanakuwa hawaoni zuri lolote.
Kipo kitu chanya au kizuri unaweza kukiona pia kwenye changamoto. Usilalamike, jifunze kupitia changamoto yako.
Yapo mafanikio na baraka ambazo zimejificha kwenye changamoto. Unatakiwa uyaone mafanikio hayo.
Changamoto unazopitia zina uwezo wa kukufanya, ujifunze, ukue na kuwa jasiri wa kufikia mafanikio yako.
Zingatia, mafanikio yako utaendelea kuyapata kama utakuwa mtu wa shukrani katika kila eneo la maisha yako.
Kuwa na shukrani ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yako. Anza
leo kuwa mtu wa shukrani, utafanikiwa.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Oct 4, 2021
Mawazo Kumi (10) Yatakayokupa Nguvu Kubwa Yakufikia Mafanikio Yako.
Mafanikio siku zote yanaanza na mawazo. Kama hakuna wazo sahihi ieleweke pia hakuna mafanikio sahihi ambayo yataweza kuchipua kwa nje, sana sana utakuwa ni mtu wa kushindwa kila wakati. Kupitia makala haya utajifunza mawazo muhimu yatakusaidia kuweza kufikia mafanikio yako. Karibu na twende tujifunze;-Oct 3, 2021
Weka Umakini Wako Wote Kwenye Vitu Hivi Na Utafanikiwa.
Kila wakati zingatia kile kinacholeta mabadiliko sana kwenye maisha na unatakiwa kuachana na kile ambacho hakileti mabadiliko kwenye maisha yako. Kama unaendelea kufanya vitu ambavyo havileti matokeo chanya kwako huko ni kujipoteza.Oct 2, 2021
Jinsi Ya Kupika Tambi Za Mayai.
Oct 1, 2021
Hiki Ndicho Kitu Kinachokuzuia Kufanya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.
Wakati ulipokuwa shule ulisoma sana na kuhakikisha unafaulu ili kukwepa maumivu ya kufeli. Pia kuna wakati umeweka juhudi nyingi sana ili kukwepa maumivu ya aina fulani na kutafuta mahala sahihi kwako.
Tunaambiwa kitu chenye nguvu ya kubadili tabia yako na mafanikio ni maumivu. Waulize wote ambao wamefanikiwa na ambao wanafikiri chanya kuhusu mafanikio, watakwambia maumivu yamewasaidia sana kubadilika na kuweza kufika hapo walipo mpaka leo.
Sep 30, 2021
Njia Pekee Itakayokufanya Ukawa Hodari Ni Hii…
Jiulize unataka kuwa hodari katika jambo lipi? Ukishapata jambo hili ambalo unataka kuwa hodari, anza utekelezaji wa kulifanya jambo hilo kila siku na kwa juhudi zote. Usijaribu kufanya na halafu ukaacha, hautaweza kuujenga uhodari kwa namna hiyo.
Sep 29, 2021
Sababu Nne (4) Kwa Nini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine.
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la watu linalalamika kwamba maisha yamekewa magumu. Kwa sababu hii pia watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kuona maisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradi siku ziende.Sep 28, 2021
Mambo Ya kuzingatia Ukitaka Kufanikiwa Katika Masuala Ya Kifedha.
Somo la fedha ni la muhimu sana kwa kila mmoja wetu, hii ni kwa sababu tunashindwa kupata au kudumu katika mafanikio yetu kifedha hii ni kwasababu wengi wetu hutuna uelewa wa kutosha katika suala la kipesa.Sep 27, 2021
Silaha Kubwa Ya kufikia Mafanikio Yako Ni Hii.
Kati ya kitu muhimu sana cha kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Kati ya silaha kubwa ya kukusaidia kufanikiwa, ni akili ya utulivu. Unapokuwa na akili ya utulivu inakusaidia kuona mambo mengi, na kufanikisha mambo mengi pia.
Si rahisi sana kuweza kufanikiwa sana kama akili yako haijatulia. Unatakiwa ujue, silaha yako kubwa ya mafanikio ni matumizi ya akili yako na wala si bahati au muujiza kama uwazavyo.
Akili yako ina uwezo wa kukupa matokeo makubwa sana kama imetulia, hapa inaweza ikakupa majibu mazuri na ikaleta matokeo ya kushangaza ambayo huwezi kuyaamini.
Hivyo, unatakiwa kila wakati kuchagua mazingira tulivu yatakayoifanya akili yako ifanye kazi kwa utulivu. Unatakiwa kuishi na watu sahihi, wasio na makelele kwako.
Lakini si hivyo tu, unatakiwa kuishi na mke au mume sahihi kwako asiye na makelele. Unatakiwa kuishi na mwenzi wako ambae anaifanya akili yako itulie na isiwe ya vurugu.
Amani ya akili, utulivu wa akili, ndio chanzo cha mafanikio makubwa yote na yakutisha. Hakuna ambae aliyefanikiwa huku akili yake ikiwa haijatulia, mtu huyo hayupo.
Waangalie vizuri watu waliofanikiwa, utajifunza kitu kimoja kwao ni watu ambao akili zao zimetulia. Unasema nimejuaje, angalia jinsi wanavyoongea, wanaongea kwa utulivu mkubwa sana, hiyo ni ishara akili zao zimetulia.
Ili kufukia mafanikio yako makubwa, haina haja na maana kuishi na watu au katika eneo ambalo linakunyima utulivu wa akili. Jiulize, ya nini kuishi na mpenzi ambaye anaifanya akili yako isitulie na kuanza kumwaza yeye. Tafuta utulivu wa akili utaona matokeo yake makubwa jinsi utakavyo yapata.
Unapokuwa na utulivu wa akili inakusaidia sana wewe kupangilia mambo na mikakati yako kwa ukamilifu, tofauti na ambavyo ukikosa utulivu akili yako haiwezi kuwaza kitu cha maana na kukupa matokeo makubwa.
Zingatia sana, utulivu wa akili, ni silaha ya kwanza katika kufikia mafanikio yako. Kila siku, jitahidi, utafute eneo lilotulia na tafakari maisha yako, na utaona matokeo mazuri yakija kwa upande wako.
Unatakiwa ujue, silaha kubwa katika kufikia mafanikio yako ni
utulivu wa akili. Ukituliza akili zako, utafanya mambo makubwa sana na ya
kushangaza wengi na pia wengi hawataamini je, kweli ni wewe. Kumbe siri, ipo
kwenye kutuliza akili, basi.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 26, 2021
Chagua Mwendo Upi Unakusaidia Kufanikiwa.
Kuna wakati unaweza ukakamilisha mambo mengi sana, kama utaamua kwenda kwa taratibu. Unatakiwa usikimbize mambo yako, ila unatakiwa kwenda taratibu na kufanya kwa uhakika na ufanisi mkubwa wenye faida.
Kwa mfano, kama kuna majukumu ambayo unayafanya kila siku, basi, majukumu hayo yafanye kwa utaratibu, kwa utulivu mkubwa na utajikuta unakamilisha mambo mengi ambayo hukutegemea.
Kuna watu wanafikiri ili kukamilisha mambo mengi unatakiwa kwenda kwa haraka zaidi, kitu ambacho si kweli. Unaweza kwenda taratibu na ukakamilisha mambo mengi, unaweza kwenda haraka halafu ukaharibu.
Ni wajibu wako unatakiwa ujue ni wakati upi unatakiwa uende taratibu na wakati upi unatakiwa uende haraka. Si kila wakati wa kwenda kwa haraka ikiwa utafanya hivyo huwezi kukamilisha mambo mengi zaidi unajiharibia wewe.
Kama nilivyosema, kwenda haraka hakuwezi kukusaidia kukamilisha mambo mengi kwa sababu, akili yako inakuwa haijatulia yaani inayumba yumba. Kama akili yako inayumba hivyo, kufanikisha mambo mengi ni ndoto.
Unatakiwa kila wakati kujiuliza, hapo ulipo ni wakati wa kwenda haraka au wakati wa kwenda kwa kasi. Kisha ukishapata majibu, fanya uamuzi sahihi. Maisha sio mashindano na wengine, angalia mwendo wako.
Hapa ndio upo ule umuhimu wa kuchagua mwendo upi unakusaidia kukamilisha mambo mengi. Je, mwendo wa kasi au mwendo wa taratibu, lakini kaa ukijua kila mwendo una sehemu yake.
Suala hili, lipo kama vile unavyoendesha gari. Si kila wakati unatakiwa kukimbiza gari, yapo mazingira yake. Na kwenye maisha iko hivyo hivyo, kuna wakati wa kwenda kwa haraka na wakati wa kwenda taratibu.
Kufanikiwa kwako kunategemea sana uchaguzi wako wa mwendo upi
uutumie na katika eneo lipi. Fanyia kazi hili, na utaona matokeo makubwa kwa
upande wako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.
Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.
Sep 25, 2021
Mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kufanya uwekezaji.
Ipo hivi unapofanya uwekezaji katika jambo lolote unatakiwa
kuelewa kwamba hakuna faida utakayoipata papo hapo. Bali uwekezaji huchukua
muda fulani mpaka uje uone uwekezaji wa jambo hilo.
Wengi
wanapoambia wawekeze katika jambo fulani hukurupuka katika kuwekeza mwisho wa
siku hujikuta wanapata hasara au kutokuona faida ya uwekezaji waliofanya.
Kitu
pekee ninachopaswa kukumbusha ni kwamba unapotaka kuwekeza katika jambo fulani,
unatakiwa kuzingatia mambo haya machache;
·
Uwekezaji unakutaka uweze kulielewa jambo unalotaka kuliwekeza kwa
undani zaidi.
·
Faida ya uwekezaji huchelewa sana kuonekana.
·
Uwekezaji huitaji uvumilivu mkubwa ndani yake.
·
Uwekezaji unahitaji umakini wa hali ya juu ili kuepukana kupata
hasara ya jambo husika.
Hivyo ni
vyema ukayazingatia hayo machache kati ya mengi kabla hujaamua kuwekeza katika
jambo lolote lile ulitakalo.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942