google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 10, 2016

Je, Upo Tayari Kutoa Kitu Gani Ili Uweze Kutimiza Ndoto Zako?

No comments :
Katika maisha yake,  siku zote na wakati wote, alitamani sana kuona ndoto zake zikitimia. Hakuna kitu ambacho kilimkera sana kama kuona siku zinakwenda bila kuona mafanikio, zaidi ya umaskini uliomgubika.
Ili kutimiza ndoto yake na kuikomboa familia yake kwenye umaskini ilikuwa ni lazima atumie kipaji chake cha kuigiza. Hicho ndicho kilikuwa kitu pekee aliamini ni lazima kitamtoa kwenye umaskini.
Hata hivyo kwa bahati mbaya sana haikuwa rahisi sana kama kijana huyu alivyofikiri. Alikutana na upinzani mwingi sana, ambao ulitosha kumkatisha tamaa kabisa.
Katika jaribio lake la kwanza la kujaribu kucheza filamu, wakala aliyekuwa akisimamia zoezi hilo alimkataa kwa sababu ya lafudhi yake mbovu na pia kupooza kwa upande mmoja wa shavu lake, hali iliyopelekea shingo yake ikae upande.
Hivyo kwa madai ya wakala huyo, isingekuwa rahisi kufanya kazi na mtu wa namna hiyo, ilikuwa hiyo ni sawa na kuipa kampuni hasara, kwa sababu filamu itatoka bila mvuto wowote.


Hilo halikumkatisha tamaa kijana huyu, alichokuwa akitaka ni lazima afanikiwe. Alijaribu tena na tena lakini kote alikataliwa na ilifika wakati akawa amekataliwa mara elfu moja.
Pamoja na juhudi zote hizo, mambo yalizidi kumwendea hovyo, ilifika mahali hata zile pesa ndogo alizo kuwanazo zilikwisha, akajikuta akiuza mikufu ya dhahabu ya mkewe ili kulipia baadhi ya mahitaji, lakini nayo haikusaidia kitu mambo yalizidi kwenda hovyo upande wake.
Kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni lazima acheze filamu yake ya kwanza na atimize ndoto zake, hicho kilikuwa ni kitu ambacho hakikwepi. Ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwa gharama yoyote ile.
Aliwaza cha kufanya ni nini? Hapo ndipo alipopata wazo kla kuuza mbwa wake mpendwa aliyekuwa akimpenda. Alimuuza mbwa yule ili walau apate pesa kidogo itakayoweza kumsaidia kulipia baadhi ya gharama zitakazosaidia kutimiza ndoto yake.
Hatimaye alimuuza mbwa yule kwa maumivu makubwa, lakini alipata pesa iliyomsaidia kuta filamu ya kwanza na ambayo ilianza kumuingizia pesa hata kama ni kidogo.
Huko ndiko alikoanzia maisha yake mcheza filamu maarufu duniani yaani Sylvester Stallone. Ilikuwa sio rahisi kufika hapo ila ni kwa sababu ya kujituma kwake na kuvumilia kila hali ndivyo vilivyomtoa.
Sylvester Stallone anatajwa kwamba ni moja ya wacheza filamu maarufu duniani na wenye mafanikio makubwa, waliodumu zaidi ya miongo mitatu na kujiingizia kipato kikubwa sana.
Hayo yote hayakuja bure, ila yalitokana na kujituma sana na kuvumilia sana. Ilifika mahali wakati anatayarisha kazi yake alifanya kazi zaidi ya saa 20 kuandaa ‘script’ amabaye angeitumia kwenye filamu yake.
Kupitia maisha ya Sylvester Stallone kule alikoanzia na kuwa mcheza sinema maarufu, yapo mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa ujifunze na kuyaelewa ili kufikia mafanikio yako.
1. Unatakiwa kulipa gharama yoyote il hadi ndoto zako zitumie. Kama una unakitu chochote cha kutoa, toa hadi mafanikio yako yatimie. Tunaona Sylvester Stallone ilifika mahali aliuza mbwa wake kwa ajili ya mafanikio.
2. Acha kukatishwa tamaa na kitu chochote. Katika maisha kupo kukataliwa kwa aina nyingi. Kupo kukataliwa na watu, ambao watakwambia huwezi hicho unachokitaka, kukifanya. Lakini pia kupo kukataliwa na matokeo. Yote hayo unatakiwa uyajue na kuwa nayo makini zaidi.
3. Fanya kazi kwa bidii sana. Ikiwezekana fanya kazi kwa masaa mengi sana ili upambane na hali ya umaskini na hatimaye kuwa mshindi.
Ikiwa utazingatia mambo hayo matatu, uwe na uhakika katika eneo lako ulipo ni lazima uweze kuibuka kuwa mshindi wa mafanikio.
Kabla sijamalizia makala haya, naomba nikuache kwa kukuuliza swali, katika maisha yako upo tayari kutoa nini ili kuhakikisha ndoto zako zinatumia? Upo tayari kutoa muda, pesa au upo tayari kutoa nini?
Tumejifunza hapa Sylvester Stalloe ilifika mahali alitoa mbwa wake kwa kumuuza ili afanikiwe. Je, wewe binafsi upo tayari kutoa kitu gani kuhakikisha tu ni kwamba unafanikiwa?
Nakutakia siku njema na mafanikio mema yawe kwako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
O713048035,
dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.