Sep 28, 2021
Mambo Ya kuzingatia Ukitaka Kufanikiwa Katika Masuala Ya Kifedha.
Somo la fedha ni la muhimu sana kwa kila mmoja wetu, hii ni kwa sababu tunashindwa kupata au kudumu katika mafanikio yetu kifedha hii ni kwasababu wengi wetu hutuna uelewa wa kutosha katika suala la kipesa.
Wengi hatuelewi namna ya kupata pesa na namna ya kuzifanya pesa
hizo ziendelee kuwa upande wetu, Ila ukweli unabaki palepale siku zote kwamba,
ukitaka kufanikiwa kifedha na kufika mbali, unalazimika kujua mambo haya
yafutayo;-
Katika maisha yako yote unatakiwa kuwa mtalawa wa fedha zako na
sio fedha zikutawale wewe. Wapo wengi wetu wanashindwa kufanikiwa
kimaisha hii ni kwa sababu fedha zimewatawala wao, yaani unaweza ukaona
mtu kapata fedha lakini atataka kila kitu nachoikiona akinunue, huku ndiko
kunakoitwa kutwaliwa na fedha.
Nini kifanyeke?
Jambo muhimu la kuzingatie ni kila mmoja wetu ahakikishe
hatawaliwi na pesa ila yeye ndio anayezitawala pesa hizo. Wewe ndiye unayekuwa
na maamuzi sahihi juu ya kuzitumia pesa hizo na si vinginevyo.
2. Jinsi ya kutoka kwenye
madeni.
Wakati mwingine madeni ni njia nambari moja imfanyayo mtu awe
maskini kama hatakuwa makini mtu huyo, japo wapo baadhi ya watu, wao huamini ya
kwamba mfanyabiashara wa kweli haogopi madeni, huko ni kujidanya. Kama una
mkopo au madeni ni bora ukawa nayo yale ya biashara zaidi lakini si kwa ajili
ya matumizi.
Nini kifanyike?
Hivyo ndugu yangu unatakiwa kuelewa ya kwamba madeni ni mabaya
sana hasa ukiwa na hulka ya kujiendekeza katika michezo hii, hivyo kila wakati
ili uweze kuwa na uhuru wako binafsi hususani katika uhuru wa kipesa unatakiwa
kuondokana na madeni hayo mara moja, kwani madeni ni mabaya sana.
3. Jinsi ya kuongeza
kipato.
Mara zote ukitegemea mfereji mmoja kama chanzo chako cha kipato
basi fahamu fika maisha yako yatakuwa ni yale yale kila wakati. Ni lazima uwe
na njia nyingi za wewe kuweza kukuingizia kipato ili njia hizo zikusaidie kuweza
kupiga hatua. Kama una njia moja tu ya kipato, sahau kuwa huru kifedha.
Nini kifanyike?
Jambo la muhimu unalotakiwa kulikumbuka hapa ni kwamba kila wakati
ni lazima uwaze kuongeza njia mbadala ya kuongeza kipato chako, na miongoni mwa
njia zitakazokusaidia kuwa hivyo ni kuongeza wigo wako wa kutafuta pesa.
4. Jinsi ya kuweka
akiba na jinsi ya kuwekeza kwa ajili ya baadae.
Wakati mwingine hatufahamu lile litakalojitokeza siku ya kesho
hii ni kwa sababu kesho si rafiki kwetu ila tunaamini siku hiyo ipo, kama tunaamini
hivyo basi tunatakiwa kujifunza kuweka akiba kwa ajili ya uwekezaji wa kesho.
Uwekaji wa akiba ni mzuri hii ni kwa sababu miongoni mwa faida
itokanayo na kuweka akiba ni kwamba inasadia kutatua changamoto husika kwa muda
muafaka hasa unapokuwa haupo vizuri katika suala la kifedha.
Unachotakiwa kufanya?
Ni kuhakikisha kwa kila kipato unachopata unatenga asilimia
kadhaa kwa ajili ya akiba hii ni kwa sababu hatujui likalotokea siku ya
kwesho na pia ni faida kuweka akiba kwa sababu itakusaidia kuwekeza.
Hayo ndiyo mambo ya msingi unayaopaswa kufahamu kuhusu fedha.
Ndimi Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.