Sep 29, 2021
Sababu Nne (4) Kwa Nini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine.
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la watu linalalamika kwamba maisha yamekewa magumu. Kwa sababu hii pia watu wengi wamekuwa wakikata tamaa na kuona maisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradi siku ziende.
Malalamiko
ya maisha kuzidi kuwa magumu yamekuwa yakisikika sana karibu ulimwenguni kote.
Na kwa hili hiyo imekuwa ikipunguza raha
ya kuona ‘utamu’ wa maisha halisi. Si vijana wala wazee kila mtu amekuwa
akisema lake juu ya ugumu wa maisha.
Lakini
pamoja na malalamiko hayo, kitu ambacho tunatakiwa tujiulize nini kinachopelekea
kuwe na ugumu wa maisha kila kukicha? Makala haya ya leo inakwenda kukupa majibu
kwa nini maisha yanakuwa magumu kwa
wengi zaidi.
1. Kutegemea chanzo kimoja cha mapato.
Kutokana
na maisha kubadilika na gharama za maisha kupanda karibu kila siku, suala la kutegemea
kipato kimoja, ni moja ya chanzo cha maisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemea
kipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.
Kwa bahati
mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo
ya maisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tu ugumu wa maisha uonekane. Hata
siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kama bado una kipato kimoja.
2. Watu wengi wanafanya vitu
wasivyovipenda.
Maisha
ni magumu pia kwa watu wengi chini ya jua kwa sababu wamekuwa ni watu ambao
kila siku wanafanya kazi ambazo wasizozipenda. Kama unafanya kazi usiyoipenda,
unategemea nini, lazima maisha yatakuwa magumu tu.
Kufanya
kazi usiyoipenda, kwa kawaida kunakuwa kunakuchosha sana na unakuwa unaifanya
tu, kwa sababu eti upate pesa ya kula. Kama umechagua maisha hayo, ujue kabisa
maisha hayo yatazidi kukufanya wewe uyaone magumu kila kukicha.
3. Watu wengi wanaishi juu ya matumizi.
Ugumu
wa maisha pia kwa namna moja au nyingine unachangizwa na watu kuishi juu ya
matumizi au vipato vyao halali. Unatakiwa kuelewa watu wengi, wanaishi juu ya
matumizi kwa sababu ni watu ambao wanataka waonekane wamefanikiwa.
Watu
hawa wanakuwa wapo tayari wakope au wafanye lolote lile ili waonekane mambo yao
yako safi. Kwa msingi huo wanakuwa wanajitengenezea maisha magumu ambayo
wanashindwa kuyamudu kwa urahisi na matokeo yake kuongeza ugumu usio na sababu.
4. Hakuna anayejali sana maisha ya
wengine.
Maisha
ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa
hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa, ukilinganisha na zamani. Kwa sasa
ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae
nayo hadi utoke.
Kutokana
na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana
hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao
imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumu wa maisha.
Mwisho,
pengine ujiulize, je, maisha yanaendelea kuwa magumu kwako kila kukicha? Jibu
unalo wewe, nimekupa walau sababu chache zinazoonyesha kwa nini maisha yanazidi
kuwa magumu. Wewe unaamini nini, niwekee maoni hapo chini.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0687449428, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.