Dec 9, 2016
Watoto Wenye Uzito Mdogo Hawaji Kuoa.
Kwa
mujibu wa tafiti, imethibitika kwamba watoto wa kiume wanaozaliwa wakiwa na
maumbo madogo na uzito mdogo, uwezo wao wa kuoa hupungua ukilinganisha na
wenzao wenye maumbo makubwa na uzito mkubwa.
Kulingana
na moja ya ripoti iliyotolewa na watafiti wa kiingereza kupitia kwenye jarida
la la British Medical, imegundulika
kuwa wanaume ambao waliozaliwa wakiwa na maumbo na uzito mdogo, ukubwani
huchelewa sana kuoa au hushindwa kabisa kuoa.
Hata
hivyo, kulingana na matokeo ya uchunguzi huo, imebainika kwamba kuna mambo
mengi yanayosababishwa wanaume waoe ikiwa ni pamoja na yale ya kibaiolojia na
kijamii.
Na
pia imefahamika kwamba, kasoro zinazojitokeza wakati wa kuzaliwa hasa kwa
upande wa watoto wa kiume, zinaweza zikapelekea mtu kuwa matatizo makubwa
ukubwani.
Matatizo
hayo ni pamoja na ugumu wa kujumuika na watu wengine, kupungua kwa uwezo wa
kujamiiana, matatizo ya kitabia na hasa kihisia na mengineyo.
Tatizo
kubwa liko kwa watoto wakiume wachanga wanaozaliwa wakiwa na uzito unaopungua
kilo tatu na nusu. Ukweli ni kwamba watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito pungufu
na huo, wako katika uwezekano mkubwa wa kushindwa kuoa wanapokuwa watu wazima.
Watafiti
hao wamethibitisha kwamba, kati ya watoto 100 wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa
uzito huo, 80 huja kuoa na 20 wanaobaki hushindwa kabisa kuoa. Hii si idadi
ndogo hata kidogo. Kwa ujumla katika kila watoto watano wa aina hii, mtoto
mmoja hatooa anapofikia umri wa utu uzima.
Watafiti
hao wanaongezea kusema kwamba, hali hii haichagui iwapo watoto hao ni njiti,
umri wa mama zao, kipato chao wanapokuwa watu wazima na hata daraja lao katika
jamii.
Kwa
ujumla matokeo na utafiti huo yanaonesha kwamba, wanaume ambao wameshindwa kuoa
ni wafupi kwa robo tatu ya inchi, wana uzito pungufu kwa takribani kilo 2.5, na
kwa ujumla ni wembamba sana ukilinganisha na wenzao.
Hata
hivo, tunachokisema hapa ni kuwa,umbo na uzito wakati wa kuzaliwa, vina mchango
mkubwa katika kuwafanya wanaume wasioe wanapokuwa watu wazima. Lakini hio sio
sababu peke yake inayopelekea baadhi ya wanaume washindwe kuoa.
Endelea
kujifunza kupitia diraamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.