May 5, 2018
Unaharibu Au Kutengeneza Maisha Yako Kwa Sababu Ya Kuruhusu Mambo Haya.
Kwa chochote unachokiruhusu kikurudishe nyuma kwenye maisha yako kitu hicho kitakurudisha nyuma na kwa chochote unachokiruhusu kikupeleke mbele kwenye maisha yako basi kitakupeleka mbele hadi kwenye mafanikio yako.
Kwa mfano,
kama umeruhusu changamoto unazopitia ndizo ziwe chanzo cha kukurudisha nyuma
basi uwe na uhakika utarudi nyuma, na kama pia umeruhusu changamoto zako ziwe
ndio chanzo cha kuweza kukufanikisha basi ujue utafanikiwa.
Kufanikiwa
kwako kunategemea sana, ni nini ambacho unakiruhusu kikutokee. Wewe ndie chanzo
kikubwa cha mafanikio yako. Unatakiwa uwe makini na ujue hasa ni kitu kipi au
mambo gani ambayo unaruhusu kwenye maisha yako yawe chanzo cha kufanikiwa kwako au kushindwa.
Yapo
mambo ambayo ukiyaruhusu kwenye maisha yako yanakupa mafanikio na yapo mambo ambayo
ukiyaruhusu kwenye maisha yako yanakufungulia njia ya kuweza kushindwa, hapa
ndipo unatakiwa ujue jinsi ya kutambua.
Unapaswa
kujua zipo sababu na hali tofauti zinazofanya maisha yako yawe kama hivyo
yalivyo, lakini hiyo yote inatokana na jinsi
wewe unavyoruhusu baadhi ya mambo kwenye maisha yako. Inategemea unaruhusu nini
kikusogeze mbele au nini kikurudishe nyuma?
Ni wazi
hakuna anayependa kurudi nyuma kwenye maisha yake, lakini ni ukweli kwamba yapo
mambo ambayo ukiyaruhusu ni lazima yatakurudisha nyuma sana kwenye mafanikio
yako hata kama hupendi na yapo mambo ukiyaruhusu yatakupeleka mbele tu.
Huwezi ukafanikiwa kama unaruhusu uzembe, hujitumi au unakosa nidhamu binafsi. Kwa
kuruhusu mambo hayo utakwama lazima na kinyume chake kama unaruhusu kujituma,
kujifunza kukazana kwa kile unachokifanya pia utafanikiwa.
Maisha
yako hayo uliyonayo hujayapata kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya yale mambo
ambayo umeyaruhusu kwenye maisha yako na ndio ambayo yameumba maisha yako yawe
hivyo yalivyo leo hii.
Huwezi
hata kidogo kukwepa kwamba wewe ndio chanzo pekee cha maisha yako na wewe ndie
chanzo cha uliyefanya maisha yako yawe hivyo yalivyo, ni lazima ujue
unawajibika kwa namna yoyote ile kutengeneza maisha yako.
Kaa chini
na tafakari kwa kujiuliza ni mambo gani ambayo uliyaruhusu na unaruhusu sasa ambayo
yamekuwa chanzo cha kuharibu au kutengeneza maisha yako, ukishayajua mambo hayo
kuwa makini nayo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.