Sep 3, 2021
Vigezo Wanavyotumia Wanawake Kupenda Hushangaza.
Watu
wengu hujisikia vizuri wanapowavutia wenzao wa jinsia nyingine. Je, unafikiri
ni kitu gani kinachomfanya mwanamke aonekane wa kuvutia?
Kuna
vitu vingi vinavyojulikana vizuri zaidi kwa upande wa mwanamke kama vile; mwili
mzuri, sauti yenye mvuto, nywele, mikono mizuri na mengineyo mengi. Lakini,
kuna vingine ambavyo siyo vya kawaida vinavyohusu mwanaume kumvutia mwanamke.
Je,
ni vitu au mambo gani ya kipekee ambayo, humfanya mwanamke aguswe na mwanaume
fulani na huku mwanamke mwingine akishangaa ni kwa nini mwanamke mwenzake
ameguswa sana na huyo jamaa?
Inawezekana
yapo mengi ambayo, huyajui. Kwa mfano, mwanamke anaweza akavutiwa na jina la
kwanza au la ukoo la mwananume fulani. Hapa mwanamke hufikiri kwamba, huyo
mwenye hilo jina hawezi kuwa mtu wa kawaida, na kila kitu anachofanya ni lazima
kiwe cha ajabu.
Labda
ni kutokana na jina hilo kuwa ni la kigeni au anatoka kwenye ukoo ambao ni bora
au wa kipekee au anafikiri labda huyo mwanaume atamwezesha kile ambacho, mara
nyingi amekuwa hakipati.
Lakini,
inawezekana kabisa kwamba, mwanamume huyo si mzuri sana wa kuvutia au ni mbaya
sana kuliko wengine. Hakuna anayejua, labda anachotaka mwanamke huyo ni
kujaribu bahati yake ili aone kitakachotokea kwa uhakika ziadi.
Inawezekana
pia kuwa, mwanamke anaweza kuchanganyikiwa zaidi baada ya kuona umbo la mwanamume
huyo au gari lake. Pengine mambo hayo ndiyo ambayo, amekuwa akiyapenda zaidi. Inawezekana
ikawa ni dalili ya bahati kwake kwamba, ametokea katika maisha yake mtu ambae,
kwa muda mrefu amekuwa akitamani kumpata.
Upo uwezekano
pia kwamba, mwanamke akavutiwa na mwandiko au sahihi ya mwanamume fulani. Wakati
mwingine mwanamke hutokea kuwa na uhakika zaidi na kuamini yale anayoambiwa
kuhusu tabia ya mwanaume huyo, bila hata kufanya uchunguzi wa kina. Hata hivyo,
ukweli ni kwamba, upo uwezekano wa kuisoma tabia ya mwanaume huyo kwenye sahihi
au mwandiko wake.
Mwanamke
pia huvutiwa na lafudhi ya mwanamume, fani yake, hobi, na kitu kingine kisicho
cha kawaida ambacho mwanamume huyo anakipenda na kukifanya. Hata hivyo, mwanamke
anatakiwa awe mwangalifu mno na upande wa pili wa mtu huyo ambao, yeye haujui. Hapa
ikiwa na maana kuwa , pamoja na sifa zote hizo alizozibaini kutoka kwake,
anapaswa kujua kwamba, mwanamume huyo kama binadamu asiyekamilika pia ana
mapungufu na udhaifu mwingi.
Kuufahamu
ukweli huu, kutamsaidia katika kuimarisha zaidi na kumfanya awe makini
anapotafuta mwanaume wa kuishi naye. Na akumbuke kuwa, wapo wanaume ambao huficha
makucha yao au kasoro zao kwa wapenzi wao.
Kuna
mwanamke mwingine hupenda mwanaume mwenye vituko, kilema au mwenye kasoro
nyingine za kimwili. Yote hayo hutokana na asili ya mwanamke. Na ni mambo
yanayoongea ndani mwake kwamba, anataka kumjali na kumhurumia mwanaume huyo.
Kwa kawaida,
mwanamke huvutiwa zaidi na kwa urahisi, pale mwanaume anapoonyesha tabia ya
usikivu na utulivu. Hata hivyo, mtazamo huu kwa upande wa mwanamke, huhesabika
kuwa ni ushindi kwake.
Hali
kadhalika, mwanamke huvutiwa na tabia fulani ya kipekee ambayo, mwanaume anayo. Kwa
mfano, jinsi mwanaume huo anavyoutumia mkono wake wa kushoto, kwani watu wengi
wanatumia mkono wa kulia. Ukweli ni kwamba, labda huyo ndiye mwanaume ambae
mwanamke huyo anamtaka, kwani pia wanawake wengine hawawezi kujizuia kuwapenda
wanaume wenye macho ya bluu. Hilo pia ni jambo la kawaida.
Mwanamke
anaweza kumpenda mwanaume kutokana na jinsi anavyofanya kazi za nguvu au
kutokana na mwili wake kuwa na misuli. Ni jambo la kawaida kwa wanawake
kufurahia wanaume waliojazia, na inavyoonekana wanawake huwaona wanaume ambao
ni lainilaini kuwa wana haiba ya kike au ni mashoga.
Hapo
ndipo mwanamke anapolazimika kufikiria kwa makini, kuhusu mwanaume anayetumia
muda mwingi kujipodoa na fedha nyingi kwa mambo ya urembo na vipodozi kuliko
hata mwanamke, kama kweli anamvutia na anamfaa.
Na kitu
kingine ni kwamba, mwanamke humpenda mwanaume anayesaidia kufanya kazi za
nyumbani. Kwa kufanya hivyo, mwanamke huamini kwamba, mwanaume huo anamjali na
kumthamni.
Kwa kumalizia
ni kwamba, mambo mengi yanayomchanganya mwanamke kuhusiana na mwanaume
anayemtaka, kwa kweli ni ya kipekee sana na wakati mwingine huonekana kuwa ni
kituko, ingawa wakati mwingine yanaweza yakaeleweka vizuri. Mara nyingi vigezo
hivyo huonekana kuwa sahihi, iwapo tu mwanamke huyo atajisikia vizuri na kupata
ridhiko la nafsi yake.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA ESTHER ZACHARIA
WA DAR ES SALAAM TANZANIA, Email- esterzach@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.